AMIBA:Sababu,dalili,matibabu,kuzuia

Maelezo ya jumla

Amiba (Amoebiasis) ni ugonjwa wa matumbo unaosababishwa na vimelea vya Entamoeba histolytica.

Je! Ni nini dalili za Amiba?

Kwa kawaida, ugonjwa huu hudumu kwa wiki mbili, lakini unaweza kurudi ikiwa hautatibiwa vyema.
Dalili zisizo kali ni:

Dalili kali:

Kumbuka: 90% ya watu wote wenye amiba hawana dalili yoyote.

Ni nini kinachosababisha Amiba?

Entamoeba histolytica ni kimelea anaeweza kuishi kwenye utumbo mkubwa (koloni) bila kusababisha ugonjwa. Hata hivyo, wakati mwingine, huvamia kuta za koloni na husababisha uvimbe, kuhara damu au kuhara kwa muda mrefu. Maambukizi yanaweza pia kuenea kupitia damu mpaka kwenye ini na, kwa mara chache, kwenye mapafu, ubongo na viungo vingine. Hali hii inapatikana mahali popote ulimwenguni, lakini inapatikana zaidi katika maeneo ya kitropiki, yenye msongano mkubwa wa watu wanaoishi katika mazingira duni na yenye usafi hafifu. Afrika, Mexiko, sehemu za Amerika ya Kusini, na India zina matatizo makubwa ya kiafya yanayohusiana na ugonjwa huu. Entamoeba histolytica inaenea kwa njia ya chakula au maji yaliyochafuliwa na kinyesi. Hii inatokea zaidi kama kinyesi cha binadamu kinatumika kama mbolea.

Nani yuko kwenye hatari zaidi ya kupata amiba?

Sababu zifuatazo zinakuweka katika hatari zaidi ya kupata amiba kali :

 • Ulevi
 • Saratani
 • Utapia mlo
 • Uzee
 • Mimba/Ujauzito
 • Kuishi katika maeneo ya kitropiki kama Tanzania
 • Kutumia dawa aina ya corticosteroid zinazopunguza kinga ya mwili

Utambuzi wa amiba

Uchunguzi wa tumbo unaweza kuonesha ini lililovimba au tumbo linalouma sana likiguswa. Vipimo hujumuisha :

 • Vipimo vya damu ili kutambua amiba (serology)
 • Uchunguzi wa sehemu ya ndani ya utumbo mkubwa kwa kutumia kamera (sigmoidoscopy)
 • Uchunguzi wa kinyesi kwa kutumia darubini

Ukiwa na amiba ni wakati gani utafute matibabu ya haraka?

Mwone mtoa huduma wako wa afya ikiwa unaharisha.

Kuzuia Amiba

Weka mazingira yako kuwa safi , kunywa maji yaliyosafishwa au yaliyochemshwa, usile mboga ambazo hajipikwa vyema na osha matunda kabla ya kuyala. Maji yanayotumiwa na wanajamii yanapaswa kutibiwa na mfumo wa maji taka kudhibitiwa.

amibaUchaguzi wa matibabu

Madawa hutumika kutibu amiba. Uchaguzi wa madawa hutegemea ukali wa maambukizi. Dawa za kumeza za Metronidazole hutumiwa kwa siku 10 kwa maambukizi yasiyo makali. Kama unatapika, unaweza kuchomwa sindano kwenye mshipa mpaka utakapoweza kumeza dawa. Dawa za kupunguza kuharisha mara nyingi hazipendekezwi maana zinaweza kusababisha hali kuwa mbaya zaidi. Baada ya matibabu, kinyesi kinatakiwa kupimwa tena ili kuhakikisha kuwa umepona.

Nitarajie nini nikiwa na amiba?

Matokeo ni mazuri baada ya matibabu.

Matatizo yanayoweza kutokea

 • Jipu la ini
 • Madhara yanayotokana na madawa, ikiwa ni pamoja na kichefuchefu
 • Kuenea kwa vimelea kupitia damu mpaka kwenye ini, mapafu, ubongo, au viungo vingine

Vyanzo

http://www.nlm.nih.gov/medlineplus/ency/article/000298.htm

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi