ATHARI ZA MABADILIKO YA HALI YA HEWA KWA AFYA

Mabadiliko ya hali ya hewa nini?

Mabadiliko ya hali ya hewa yanatokana na kupanda kwa joto katika uso wa dunia. Kwa sababu hii, joto la dunia linaendelea kuongezeka kwa kila muongo unaopita. Wanasayansi wamegundua kuwa hali hii inasababishwa na shughuli za binadamu zinazochangia uchafuzi wa hewa.

Watu wanapochoma mafuta ili kupata umeme (kwa mfano: kuendesha magari yanayotumia mafuta), yanatoa gesi ambazo huingia kwenye hewa. Wakati mwingine gesi hizi husababisha tatizo linaloitwa kitaalamu greenhouse effect.

Greenhouse ni nyumba inayotengenezwa ili kukuzia mimea. Kwa kawaida inakuwa na paa la kioo na kuta zinazoruhusu mwanga kuingia ndani. Mwanga wa jua unapita kwa urahisi kuingia ndani ya jongo kuliko kutoka. Hii inasababisha joto linaongezeka ndani ya greenhouse kuliko ilivyo jje. Gesi zinazotolewa kwa kuchoma mafuta ya petrol na mengine, zinasababisha kuongezeka kwa joto la dunia kwa kufanya kazi kama kioo cha jingo la greenhouse. Gesi hizi zinapotoka kwenye magari, viwanda, ndege n.k. zinapaa na kutengeneza paa kuzunguka uso wa dunia. Na hii inasababisha miale inayoingia kwenye uso wa dunia haitoki – hivyo kusababisha ongezeko la joto duniani.

Kwa sababu ya shughuli za kibinadamu, miti mingi pia imekatwa, ambayo ingekuwa msaada kwa kufyonza gesi ya ukaa (carbondioxide) zinazotolewa na viwanda. Kwa hiyo kuongeza tatizo.

Mabadiliko ya hali ya hewa yataathiri vipi afya yangu?

Kadri joto kwenye uso wa dunia linavyoongezeka linaweza kuongeza hatari ya matatizo ya kiafya. Ongezeko la joto la dunia linaweza kusababisha madhara ya moja kwa moja na yasiyo ya moja kwa moja kwa afya. Madhara ya moja kwa moja yatakuwa rahisi kuonekana na yanawea kuanza kuonekana kwanza, lakini madhara yasiyo ya moja kwa moja ni hatari zaidi.

Athari za moja kwa moja za mabadiliko ya hali ya hewa kwa afya

 • Matukio ya joto kali (heat waves) yanatokea mara kwa mara, na yanaongezeka ukali na kudumu kwa muda mrefu zaidi
  • Matukio ya joto kali yanasababisha watu kuugua
  • Matukio ya joto yanaweza kusababisha watu wakafa
  • Kila mtu anaweza kuathiriwa na matukio haya ya joto kali, lakini wazee na Watoto wanaathirika zaidi

 • Joto la kila siku linaongezeka na kipindi cha kiangazi kinadumu kwa muda mrefu zaidi kuliko kawaida
  • Maambukzi ya magonjwa yanaongezeka, haya yanayoenezwa na wadudu

Kila mtu yuko hatarini kuambukizwa magonjwa, hasa watu wanaoishi maeneo ya vijijini yasiyo na mfumo bora wa huduma za afya

 • Uchafuzi wa hali ya hewa unaongezeka zaidi
  • Hatari ya kupata magonjwa ya moyo na mapafu inaongezeka, kama vile pumu na mshtuko wa moyo
  • Kila mtu yupo kwenye hatari, kaini watu wenye magonjwa ya moyo au ya mapafu wako kwenye hatari zaidi

Athari zisizo za moja kwa moja za mabadiliko ya hali ya hewa kwa afya

 • Kuongezeka kwa kina cha maji ya bahari kunakotokana na kuyeyuka kwa barafu iliyoko kwenye pembe za dunia
  • Watu, vitu, makazi na kazi za watu zinaharibiwa na maji, na kusababisha ugumu kiuchumi
  • Kila mtu anaweza kuathirika, ila watu wanaoishi katika mwambao wa bahari wako kwenye hatari zaidi

 • Mabadiliko ya hali ya joto na unyevunyevu unaosababishia madhara mazao
  • Hii inasababisha kiwango cha chakula kupungua na kusababisha ongezeko la bei ya chakula
  • Kila mtu yuko kwenye hatari, hasa watu masikini
 • Mabadiliko ya hali ya joto na unyevunyevu unaosababisha kuwepo kwa ukame mkali mara kwa mara
  • Vyanzo vya maji vinakuwa hatarini kukauka na ubora wa maji unapungua
  • Kila mtu yuko hatarini, hasa watu wanaoishi maeneo ambao tayari ni makavu

mabadiliko ya hali ya hewa

 • Mifumo ya dunia ya kusambaza hewa safi, maji safi, na chakula inaweza kuzidiwa na hata kuvurugika kabisa
  • Hii inaweza kusababisha matatizo zaidi ya upatikanaji wa chakula na maji, na kusababisha mamilioni ya watu kubadili makazi, hii inaweza kutishia usalama wa dunia.
  • Watu wote wako hatarini

Naweza kufanya nini ili kusaidia kupunguza mabadiliko ya hali ya hewa na athari kwa afya

Karibia 1/5 ya gesi zote zinazosababisha ongezeko la joto la dunia zinatokana na uzalishaji wa nyama ya kula. Kufuga ng’ombe kwa ajili ya nyama kunaongoza kwa kutoa gesi hizi kwa wingi. Daktari anaweza kuwa amekwambia kuhusu kupunguza kiwango cha mafuta unayokula kwenye mlo wako, kupunguza gesi zinazosababisha ongezeko la joto duniani inaweza ikawa sababu nyingine ya kupunguza kula nyama. Watanzania wengi wanakula wastani wa 350gm ya nyama kwa siku. Jaribu kula kama 85gm ya nyama kwa siku. Lakini pia hakikisha kula chini ya 1/3 ya nyama ya ng’ombe.

Njia nyingine ya kusaidia ni kutumia gari yako mara chache kadri inavyowezekana. Kuendesha kuelekea mahala pa karibu kunaongeza zaidi gesi za ukaa hewani kuliko safari za mbali. Badala ya kuendesha kwenda sehemu za karibu, jaribu kutembea au kuendesha baiskeli. Hii itasaidia kupunguza uchafuzi na kuifanya hewa iliyo kwenye jamii kuwa safi. Pia, mazoezi ya ziada yanawea kusaidia ukawa na afya bora zaidi.

Angalizo

Taarifa zilizotolewa katika ukurasa huu zimetoa muhtasari na zinaweza zisimfae kila mtu. Ongea na daktari ili kung’amua kama taarifa hizi zinakufaa na wewe au jaribu kutafuta habari zaidi kuhusu shida hii.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/environmentalhealth.html

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi