
Maelezo ya jumla Kipindupindu (cholera) ni ugonjwa unasababishwa na maambukizi ya bakteria aina ya vibrio cholerae. Mara nyingi maambukizi huwa ya kawaida na yanaweza yasisababishe dalili yoyote. Lakini wakati mwingine yanaweza kuwa hatari sana. Takribani mtu moja kati ya 20 wanaoambukizwa kipindupindu, huwa na dalili kali, dal...