BAWASIRI

BAWASIRI

 • February 21, 2021
 • 0 Likes
 • 72 Views
 • 0 Comments

Maelezo ya jumla

Bawasiri ni ugonjwa ambao unatokana na kuvimba kwa mishipa ya damu ndani au kuzunguka njia ya kutolea haja kubwa ‘’mkundu’’. Tatizo hili mara nyingi linawaathiri zaidi watu ambao wana tatizo la kufunga choo, ambalo linasababisha wanajikamua sana wakiwa chooni au kama wanapata matukio ya kuhara ya mara kwa mara. Dalili kubwa ya bawasiri ni kuwepo kwa michirizi myekundu ya damu kwenye karatasi za kujitawadha ‘’tissue paper’’ au unaweza kuiona kwenye bakuli la choo baada ya kujisaidia. Unaweza kujihisi maumivu wakati wa kujisaidia na ukaendelea kujihisi kama hujajisaidia kinyesi chote kikaisha. Unaweza kujisikia vibaya ukikaa kitako. Ngozi kuzunguka njia ya kutolea haja kubwa inaweza kuwa inawasha na yenye harara. Mishipa ya damu iliyovimba inaweza kutokeza nje kwenye njia ya haja kubwa na kutengeneza uvimbe ambao unauma. Tatizo hili linawapata sana kina mama wajawazito na watu ambao wana uzito mkubwa kuliko kawaida.

Mwone daktari kama

Panga kumwona daktari kama:

 • Kama unatokwa damu kutoka kwenye njia ya kutolea kinyesi au kama una uvimbe karibu au ndani ya mkundu.

Unachoweza kufanya wewe mwenyewe

Bawasiri zinaweza kukutia karaha, lakini kuna mambo unayoweza kufanya ili kupunguza uvimbe na kutegemeza matibabu yatakayotolewa na daktari.

 • Hakikisha unatibu tatizo la kufunga choo mapema kabla halijasababisha au kuongeza zaidi tatizo la bawasiri
 • Nenda choo mara tu unaohisi haja ya kujisaidia. Usijikamue unapokua unajisaidia na usizibe au kushikilia pumzi unapokuwa ukijisaidia, na usiwe na haraka. Hata kama unajihisi kuwa haujatoa kinyesi chote, jitahidi na epuka kujikamua unapokuwa umefikia mwisho wa shughuli.
 • Jisafishe vizuri eneo la mk*ndu kila baada ya kujisaidia kwa kutumia kitambaa laini au karatasi laini za kujitawadha
 • Kama ukiweza, weka maji ya uvuguvugu kwenye besini, na kisha kaa kwenye hayo maji kwa muda wa dakika 15, mara 3 mpaka 4 kwa siku. Usitumie sabuni kuosha eneo linalozunguka njia ya kutoa haja. Jikaushe vizuri baada ya kujisafisha
 • Unaweza kutumia madawa ya kupunguza maumivu ili kupunguza karaha. Madawa kama ‘’acetaminophen’’ au ‘’ibuprofen’’yanapunguza maumivu na karaha. Kama maumivu yakiendelea kuwepo kwa zaidi ya siku kadhaa, ACHA, kumeza dawa za maumivu ukaonane na daktari.
 • Kama una maumivu na unaona uvimbe mkubwa umejitokeza, pumzika kwa siku moja kitandani. Chukua barafu iliyo kwenye mfuko, itwange na kisha ifunike kwa kitambaa laini na ishikilie karibu na mkundu kwa dakika 15-20 angalau mara 4 kwa siku.
 • Kuna madawa yanayotumika kudhibiti bawasiri, unaweza kuyatumia. Unaweza kwenda kwenye duka la dawa ukaulizia, mtaalamu wa dawa atakushauri jinsi ya kuitumia. Madawa haya yanapooza maumivu na kusababisha iwe rahisi kujisaidia. Madaw haya yanaweza kuwa na ‘’phenylephrine’’ ambayo inasaidia kupunguza uvimbe, kuwashwa na harara au inaweza kuwa na ‘’hydrocortisone’’ inayopunguza uvimbe. USITUMIE aina hizi za dawa za kutibu Bawasiri kwa zaidi ya siku 6, kwa sababu unaweza kupatwa na tukio baya linalokana na viambata vya dawa ‘’reaction’’.

Mwone daktari kama

Ni vizuri kupanga kumwona dakatari kama:

 • Unaona kuvuja damu kunaendea kuwa kubaya zaidi
 • Kuvuja damu, kuwashwa ua kama maumivu yayajapoa baada ya siku kadhaa za matibabu

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/000292.htm

 • Share:

Leave Your Comment