1. Home
 2. BRONCHIECTASIS (KUHARIBIKA KWA MFUMO WA HEWA)
BRONCHIECTASIS (KUHARIBIKA KWA MFUMO WA HEWA)

BRONCHIECTASIS (KUHARIBIKA KWA MFUMO WA HEWA)

 • October 23, 2020
 • 0 Likes
 • 160 Views
 • 0 Comments

Maelezo ya jumla

Bronchiectasis ni uharibufu unaosababisha kupanuka kusiko kwa kawaida kwa njia ya hewa.

 • Mtoto anapozaliwa na hali hii, inaitwa congenital bronchiectasis.
 • Hali hii inapotokea baadae maishani, inaitwa acquired bronchiectasis.

Ni nini dalili za bronchiectasis?

Dalili mara nyingi hutokea polepole na hatua kwa hatua, zinaweza kutokea miezi au miaka baada ya tukio lililosababisha bronchiectasis.

Zinaweza kujumuisha:

 • Rangi ya ngozi ya bluu
 • Pumzi inayonuka/yenye harufu
 • Kikohozi cha muda mrefu, kinachotoa makohozi mengi yanayonuka vibaya
 • Kupanuka kwa kucha
 • Kukohoa damu
 • Kikohozi kinachokuwa kibaya zaidi mgonjwa anapolalia upande mmoja
 • Uchovu
 • Kupumua kwa shida kunakoongezeka wakati wa mazoezi
 • Kupungua kwa uzito
 • Kukorota (wheezing)

Ni nini kinachosababisha Bronchiectasis?

Bronchiectasis mara nyingi husababishwa na uvimbe au maambukizi ya mara kwa mara kwenye njia ya hewa. Mara nyingi huanza utotoni kama matokeo ya maambukizi au kupaliwa na kitu fulani.

Cystic fibrosis husababisha nusu ya kesi zote za bronchiectasis nchini Marekani.

Hali hii pia inaweza kusababishwa kwa kuvuta/kupaliwa na vipande vya chakula wakati wa kula

Nani yuko kwenye hatari zaidi?

 • Wagonjwa wenye maambukizi makali ya mapafu ya mara kwa mara,kama nyumonia, kifua kikuu, na maambukizi mengine ya vimelea
 • Watu wenye ulinzi usio wa kawaida wa mapafu
 • Kuziba kwa njia ya hewa kwa vitu vigeni
 • Saratani

Ni wakati gani utafute matibabu ya haraka?

Mwone mtoa huduma wa afya ikiwa:

 • Maumivu ya kifua au kupumua kwa shida kunaongezeka zaidi
 • Kuna mabadiliko katika rangi au kiasi cha makohozi unapokohoa
 • Makohozi yana damu
 • Dalili nyingine zinazidi kuwa mbaya au hazipungui baada ya matibabu.

Utambuzi

Wakati wa kusikiliza kifua kwa stethoscope, daktari anaweza kusikia sauti za mikwaruzo,kukorota na zingine sehemu za chini za mapafu.

Vipimo vinavyoweza kufanyika hujumuisha:

 • Eksirei ya kifua – picha za eksirei humpa daktari fursa ya kukagua sehemu ya ndani ya kifua
 • CT Scan ya kifua – picha za CT scan hutoa maelezo ya ziada kwa daktari
 • Sputum culture– kupandikiza makohozi katika mazingira maalumu ili kuruhusu vimelea kuota ili iwe rahisi kuvitambua
 • Complete blood count (CBC) – kipimo hiki husaidia kutambua kama kuna maambuki yoyote kwenye damu
 • Makohozi yanaweza kuchukuliwa kwa ajili ya kupima kifua kikuu
 • Kipimo cha jasho au vipimo vingine vinavyotumiwa kupima cystic fibrosis

Uchaguzi wa matibabu

Matibabu yanalengo la kudhibiti maambukizi na kupunguza makohozi, ili kuifungua njia ya hewa iliyoziba na kuzuia kutokea kwa matatizo zaidi.

kupunguza makohozi kwenye njia ya hewa ni zoezi la kila siku na ni sehemu ya matibabu. Daktari bingwa wa mfumo wa upumuaji, atamwonesha mgonjwa mazoezi kadhaa ya kukohoa, yatakayosaidia kuondoa makohozi kifuani ili yasizibe njia ya hewa.

Antibiotics (viuavijasumu), bronchodilators (dawa za kupanua njia ya hewa), na expectorants (dawa za kusaidia kutoa makohozi) mara nyingi hutolewa kama kuna maambukizi.

Upasuaji ili kuondoa sehemu ya pafu unaweza kuhitajika kama dawa hazifanyi kazi vizuri au kama  mgonjwa anavuja damu sana.

Nini cha kutarajia?

Kwa matibabu sahihi, watu wengi wanaweza kuishi maisha ya kawaida bila matatizo makubwa.

Matatizo yanayoweza kutokea

 • Cor pulmonale – huu ni ugonjwa wa moyo unaotokea baada ya mapafu kuharibika, hii ina maana mapafu mabovu hatimaye huharibu moyo.
 • Kukohoa damu
 • Kiwango cha chini cha oksijeni mwilini (hii ni katika hali kali sana)
 • Nyumonia ya mara kwa mara

Kuzuia

Hatari ya kupata bronchiectasis inaweza kupunguzwa kwa kutibu maambukizi ya mapafu mapema iwezekanavyo.

Chanjo za watoto husaidia kupunguza uwezekano wa kupata baadhi ya maambukizo. Kuepuka kuvuta sigara na uchafuzi wa hewa inaweza kupunguza hatari ya maambukizo.

Vyanzo

 http://www.nlm.nih.gov/medlineplus/ency/article/000144.htm

 • Share:

Leave Your Comment