1. Home
  2. Magonjwa ya mifupa & misuli
KUUMIA MAUNGIO:Mguu,goti,kiwiko n.k

Maelezo ya jumla Kuumia maungio ‘’sprain/strain’’ ni jambo la kawaida kwenye michezo. Wakati mwingine kano ‘’ligaments’’ za kwenye maungio kama vile kifundo cha mguu huumia kwa sababu ya kuvutwa sana. Hii inatokea kama mifupa itavutwa ghafla kwa nguvu na kusababisha kuachia au kuchanika kwa tishu zinazozunguka maungio. Kwa...

VIDOLE VINAPATA BARIDI SANA

Maelezo ya jumla Ni kawaida kwa vidole vya miguu au mikono kushikwa na baridi. Lakini kwa baadhi ya watu, vidole vinashikwa na baridi kali sana utadhani vimetoka ndani ya jokofu/friji. Mzunguko usio wa kutosha wa damu kwenda kwenye vidole vya mikono na miguu au upungufu wa homoni zinazotolewa na tezi dundumio ‘’thyroid gland’’ una...

MAUMIVU YA MIGUU

Maelezo ya jumla Mguu ''foot'' unahimili mikwaruzo na shinikizo kubwa sana. Baada ya kusimama au kutembea kwa muda mrefu, unaweza kuwa na maumivu ya miguu na hata kuvimba. Miguu ikitumika sana inaweza kuwa na maumivu ya uwayo, , maumivu ya misuli ya miguu au kukaza kwa kano "tendons" za miguu. Viatu ambavyo havikutoshi, vinavyobana au amb...

MAUMIVU YA KISIGINO

Maelezo ya jumla Kuvimba kwa wayo wa mguu ‘’plantar facitis’’ ndio sababu kubwa ya maumivu ya kisigino ‘’heal pain’’, mgonjwa anapata maumivu makali sana akikanyaga chini baada tu ya kuamka asubuhi au baada ya kukaa bila kutembea kwa muda mrefu. Tatizo hili linaweza kutokana na shughuli kama kukimbia, na unaweza kujihisi v...

KUVIMBA KWA VIFUNDO VYA MIGUU

Maelezo ya jumla Kuvimba kwa vifundo vya miguu ‘’swollen ankles’’ kunaweza kutokea baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kufanya lolote, kwa mfano; wakati wa safari ndefu ya gari au ndege au kama unatumia muda mrefu ukiwa umesimama, hasa katika mazingira ya joto kali. Kuvimba kwa vifundo vya miguu hutokana na kutwama kwa majimaji mig...

KUVIMBA KWA MISHIPA YA VENA MIGUUNI

Maelezo ya jumla Kuvimba kwa mishipa ya vena miguuni ‘’varicose veins’’, ni tatizo la vena za miguu, linalosababisha mishipa ya damu kugeuka rangi na kuwa za bluu, kuvimba na kujikunja kunja chini ya ngozi. Mara nyingi utazikuta sehemu ya ndani ya mguu, kwenye ndama ya mguu au kwenye kifundo cha mguu. Mguu uliathirika unakuwa mzit...

KUKAZA KWA MISULI YA MIGUU

Maelezo ya jumla Kukaza kwa misuli ya miguu ''leg cramp'' kunasababisha maumivu kwenye misuli ya mguu au ndama ya mguu. Misuli inakaza na kukakamaa, na inauma ukijaribu kujongea. Maumivu huwa yanadumu kwa dakika kadhaa tu. Misuli inaweza kukaza ukiwa unaamka asubuhi au baada ya kukaa au kulala vibaya. Msuli unapobana ukiwa unafanya kazi n...

MAUMIVU YA BEGA

Maelezo ya jumla Maumivu ya bega yanaweza kuwepo muda wote au yanaweza kuwepo unapoweka mkono katika mkao fulani au kuuchezesha kuelekea uelekeo fulani, kwa mfano unapouzungusha. Maumivu haya yanaweza pia kusambaa kuelekea kwenye mkono. Sababu za kawaida za maumivu ya bega ni kuvimba kwa misuli na kano ‘’tendons’’ zinazozunguka ma...

MAUMIVU YA GOTI

Maelezo ya jumla Magoti ni maungio yanayobeba sehemu kubwa ya uzito wa mwili, na kwa sababu hii ni rahisi sana kuteguka au kuumia. Unaweza kuwa na maumivu ya goti moja au yote, yanaweza kuwa yamevimba, yana joto ukigusa na inakuwa ngumu kujongesha. Ukigeuza kwa nguvu sehemu ya goti ni rahisi sana kuumia, na hii ni moja wapo ya sababu kubw...

MAUMIVU YA NYONGA

Maelezo ya jumla Sababu kubwa zaidi ya mkazo au maumivu ya nyonga ni kulika na kuisha kwa maungio ya nyonga kwa sababu ya ‘’arthritis’’. Tatizo hili huwapata zaidi wazee; kama unalo, utahisi maumivu ya paja, makalio au kwenye kinena pamoja na nyonga. Sababu nyingi...