1. Home
  2. Magonjwa ya ndani ya mwili
SONONA

Maelezo ya jumla Sonona (Depression) ni hali ya kuhisi huzuni, kushuka moyo na kukosa furaha. Wengi wetu hujihisi hivi kwa wakati mmoja au mwingine kwa muda mfupi. Ugonjwa wa sonona ni tatizo la kihisia, mgonjwa huhisi huzuni mwingi na hasira. Mafadhaiko wa aina hii huvuruga mfumo wa maisha ya kila siku wa mgonjwa. Je! Ni...

USAHAULIFU

Maelezo ya jumla Usahaulifu (amnesia) ni hali isiyo ya kawaida ya kusahau sana. Mgonjwa anaweza asiwe na uwezo wa kukumbuka matukio mapya, anaweza asiwe na uwezo wa kukumbuka tukio au matukio ya zamani, au yote mawili. Sababu ni nini? Kuna maeneo kadhaa ya ubongo yanayosaidia kuunda, kutunza na kurejesha kumbukumbu una...

KIUNGULIA

Maelezo ya jumla Kiungulia (heartburn) ni hali ya kuhisi mchomo (maumivu kama moto) unaotokea nyuma ya mfupa wa kidari. Kwa kawaida maumivu haya huanzia kwenye umio (oesophagus) na kupanda kifuani na yanaweza kuenea mpaka kwenye shingo au koo. Ni nini husababisha kiungulia? Karibu kila mtu hupatwa na kiungulia...

KUSHUKA KWA SHINIKIZO LA DAMU

Maelezo ya jumla Kushuka kwa shinikizo la damu (hypotension), ni hali ya kuwa na shinikizo la damu lililo chini sana kuliko kawaida. Hii humaanisha moyo, ubongo, na sehemu nyingine za mwili hazipati damu ya kutosha. Nini dalili za kushuka kwa shinikizo la damu? Dalili zinaweza kujumuisha: Kuona maluweluwe...

NGIRI

Maelezo ya jumla Ngiri (hernia) ni hali inayotokea kama kuna uwazi au udhaifu kwenye ukuta wa tumbo na kusababisha viungo vya ndani ya tumbo kuchoropoka na kutokeza nje ya ukuta wa tumbo. Ukuta wa tumbo umeundwa na safu imara ya fascia inayoizunguka misuli ya tumbo, na kazi yake kubwa ni kulinda na kuzuia vinavyopaswa ku...

BUSHA

Maelezo ya jumla Busha (hydrocele) ni hali inayosababishwa na kujaa kwa maji katikati ya tabaka mbili za utando unaozunguka korodani na mrija unaobeba manii kutoka kwenye korodani kwenda nje. Je! Nini dalili za busha? Kwa kawaida busha halisababishi maumivu yoyote, korodani huvimba na kuwa kama puto lililojaa maji. Bus...

HOMA YA DENGUE

Maelezo ya jumla Homa ya dengue (dengue fever) ni ugonjwa unaosababishwa na virusi wanaoenezwa na mbu. Je, ni dalili za homa ya dengue? Homa ya dengue huanza na homa ya ghafla, joto la mwili linaweza kupanda hata kufikia nyuzi  joto 40. Mgonjwa anaweza kutokewa na upele mwekundu siku 2-5 baada ya homa kuanza. Upele wa...

TAUNI

Maelezo ya jumla Tauni (plague) ni ugonjwa wa kuambukiza unaowapata  panya, wanyama fulani na binadamu. Ugonjwa huu husababishwa na bakteria wanaoitwa Yersinia pestis. Bakteria hawa hupatikana katika maeneo mengi duniani. Kuna aina tatu za tauni, tauni inayosababisha mtoki (bubonic), tauni inayosababisha nyumon...

KISONONO

Maelezo ya jumla Kisonono (Gonorrhea) ni ugonjwa wa zinaa. Je, Nini dalili za kisonono? Dalili za kisonono huanza kuonekana siku 2 - 5 baada ya kuambukizwa. Hata hivyo, kwa wanaume, dalili zinaweza kuchelewa mpaka mwezi. Watu wengine hawapati dalili kabisa. Wanaweza kuwa hawajui kabisa kwamba wameambukizwa ugonjwa huu, na kwa s...

KIPINDUPINDU

Maelezo ya jumla Kipindupindu (cholera) ni ugonjwa unasababishwa na maambukizi ya bakteria aina ya vibrio cholerae. Mara nyingi maambukizi huwa ya kawaida na yanaweza yasisababishe dalili yoyote. Lakini wakati mwingine  yanaweza kuwa hatari sana. Takribani mtu moja kati ya 20 wanaoambukizwa kipindupindu, huwa na dalili kali, dal...