1. Home
  2. Magonjwa ya ndani ya mwili
UKIMWI

Maelezo ya jumla UKIMWI – Upungufu wa kinga mwilini- ni ugonjwa unaopata mtu baada virusi vya VVU kuharibu mfumo wa kinga yako ya mwili. Kwa kawaida, mfumo wako wa kinga husaidia kupambana na magonjwa. Mfumo wako wa kinga unaposhindwa kufanya kazi yake vyema unaweza kuugua sana na hata kufa. VVU - Virusi vya Ukimwi - ni virusi vinavyoua...

KITAMBI

Maelezo ya jumla Kitambi (obesity) humaanisha kuwa una mafuta mengi mwilini. Kuwa na kitambi si sawa na kuwa na uzito mkubwa (overweight), kuwa na uzito mkubwa humaanisha mtu ana uzito mkubwa sana kuliko ilivyokawaida. Mtu anaweza kuwa na uzito mkubwa kutokana na  ziada ya misuli, mifupa au maji mwilini, mafuta pia yana...

KIBOLE

Maelezo ya jumla Kibole (appendicitis) ni uvimbe wa kidole tumbo (appendix) unaosababishwa na maambukizi. Kidole tumbo ni kiungo kidogo kinachoonekana kama kidole kilichopachikwa kwenye sehemu ya mwanzo ya utumbo mpana. Kidole tumbo kiko tumboni upande wa chini-kulia. Kazi yake haijulikani. Kuziba kwa kidole tumbo husaba...

KUTOKWA DAMU

Maelezo ya jumla Kutokwa damu (bleeding) kunaweza kutokea nje au ndani ya mwili: Ndani ya mwili, damu huvuja kutoka kwenye mishipa ya damu au viungo Nje ya mwili, damu hutoka kupitia kwenye matundu ya asili (kama vile uke, mdomo, au njia ya haja kubwa) au damu inapotoka kupitia kwenye ngozi D...

DAMU KWENYE KINYESI

Maelezo ya jumla Mara nyingi kinyesi kinapokuwa na damu huashiria kuwa kuna tatizo au jeraha kwenye mfumo wa kumeng’enya chakula. Damu kwenye kinyesi inaweza kutoka mahali popote kwenye mfumo wa kumeng’enya chakula, kuanzia mdomoni hadi kwenye sehemu ya kutolea haja kubwa. Damu inaweza kuwepo kwa kiasi kidogo sana kiasi kwamba huwe...

SARATANI YA KIBOFU

Maelezo ya jumla Kibofu (bladder) hupatikana kwenye sehemu ya chini ya tumbo, na kazi yake kubwa ni kuhifadhi mkojo. Saratani ya kibofu (bladder cancer) hutokea kwenye utando wa ndani wa kibofu. Je, nini dalili za kansa ya kibofu? Dalili za kansa ya kibofu ni pamoja na: Mkojo wenye damu (Mkojo huw...

UVIMBE KWENYE UBONGO

Maelezo ya jumla Ubongo ni sehemu ya mfumo mkuu wa neva. Ni chanzo cha mawazo, hisia, kumbukumbu, lugha, kuona, kusikia, kutembea, na kadhalika. Hakuna sababu inayojulikana ya kutokea kwa uvimbe kwenye ubongo. Kwa upande mmoja, uvimbe unaweza kuharibu moja kwa moja seli za ubongo. Kwa upande mwingine, unaweza kuharibu seli za ubongo kwa k...

SARATANI YA MATITI

Maelezo ya jumla Saratani ya matiti ni kansa inayotokea kwenye tishu za matiti. Inatokea kwa wanaume na wanawake. Saratani ya matiti kwa wanaume hutokea kwa nadra. Dalili za saratani ya matiti ni pamoja na; Kuvimba titi, kuchubuka au kubonyea kwa ngozi ya titi, maumivu ya titi/chuchu, kurudi ndani kwa chuchu (retraction), wekundu...

TEZI DUME

Maelezo ya jumla Tezi dume (prostate), ni tezi iliyo kwenye kizazi cha mwanaume inayozalisha maji maji yanayobeba manii/shahawa. Inaizunguka urethra, mrija unaotoa mkojo kwenye kibofu kwenda nje. Tezi dume ya kila mwanaume huongezeka ukubwa kadri umri unavyoongezeka. Kadri tezi inapokua na kuongezeka ukubwa,inaweza kukandamiza...

MAUMIVU YA MGONGO

Maelezo ya jumla Maumivu ya mgongo ni tatizo linalowapata watu wengi sana. Katika kipindi chote cha maisha ya mwanandamu ,watu 8 kati ya 10 huathiriwa na tatizo hili. Maumivu ya mgongo yanaweza kuwa ya kawaida,mengine yanaweza kuwa ya kawaida lakini yanayodumu kwa muda mrefu au yanaweza kuwa maumivu makali ya ghafla. Je! Nini dalili...