1. Home
  2. Magonjwa ya ndani ya mwili
KIUNGULIA

Maelezo ya jumla Kiungulia (heartburn) ni hali ya kuhisi mchomo (maumivu kama moto) unaotokea nyuma ya mfupa wa kidari. Kwa kawaida maumivu haya huanzia kwenye umio (oesophagus) na kupanda kifuani na yanaweza kuenea mpaka kwenye shingo au koo. Ni nini husababisha kiungulia? Karibu kila mtu hupatwa na kiungulia kwa wakati fulani...

KUSHUKA KWA SHINIKIZO LA DAMU

Maelezo ya jumla Kushuka kwa shinikizo la damu (hypotension), ni hali ya kuwa na shinikizo la damu lililo chini sana kuliko kawaida. Hii humaanisha moyo, ubongo, na sehemu nyingine za mwili hazipati damu ya kutosha. Nini dalili za kushuka kwa shinikizo? Dalili zinaweza kujumuisha: Kuona maluweluwe...

NGIRI

Maelezo ya jumla Ngiri (hernia) ni hali inayotokea kama kuna uwazi au udhaifu kwenye ukuta wa tumbo na kusababisha viungo vya ndani ya tumbo kuchoropoka na kutokeza nje ya ukuta wa tumbo. Ukuta wa tumbo umeundwa na safu imara ya fascia inayoizunguka misuli ya tumbo, na kazi yake kubwa ni kulinda na kuzuia vinavyopaswa ku...

MABUSHA

Maelezo ya jumla Mabusha (hydrocele) ni hali inayosababishwa na kujaa kwa maji katikati ya tabaka mbili za utando unaozunguka korodani na mrija unaobeba manii kutoka kwenye korodani kwenda nje. Je! Nini dalili ya mabusha? Kwa kawaida busha halisababishi maumivu yoyote, korodani huvimba na kuwa kama puto lililojaa maji....

HOMA YA DENGUE

Maelezo ya jumla Homa ya dengue (dengue fever) ni ugonjwa unaosababishwa na virusi wanaoenezwa na mbu. Je, ni dalili za dengue? Homa ya dengue huanza na homa ya ghafla, joto la mwili linaweza kupanda hata kufikia nyuzi  joto 40. Mgonjwa anaweza kutokewa na upele mwekundu siku 2-5 baada ya homa kuanza. Upele wa pili un...

TAUNI

Maelezo ya jumla Tauni (plague) ni ugonjwa wa kuambukiza unaowapata  panya, wanyama wengine na binadamu. Ugonjwa huu husababishwa na bakteria wanaoitwa Yersinia pestis. Kuna aina tatu za ugonjwa huu, tauni inayosababisha mtoki (bubonic), tauni inayosababisha nyumonia (pneumonic) na tauni inayosambaa kwenye damu (sep...

KISONONO

Maelezo ya jumla Kisonono (Gonorrhea) ni ugonjwa wa zinaa. Je, Nini dalili za kisonono? Dalili za kisonono huanza kuonekana siku 2 - 5 baada ya kuambukizwa. Hata hivyo, kwa wanaume, dalili zinaweza kuchelewa mpaka mwezi. Watu wengine hawapati dalili kabisa. Wanaweza kuwa hawajui kabisa kwamba wameambukizwa ugonjwa huu, na kwa s...

KIPINDUPINDU

Maelezo ya jumla Kipindupindu (cholera) ni ugonjwa unasababishwa na maambukizi ya bakteria aina ya vibrio cholerae. Mara nyingi maambukizi huwa ya kawaida na yanaweza yasisababishe dalili yoyote. Lakini wakati mwingine  yanaweza kuwa hatari sana. Takribani mtu moja kati ya 20 wanaoambukizwa kipindupindu, huwa na dalili kali, dal...

KICHWA KUUMA

Maelezo ya jumla Kichwa kuuma ni neno linalotumika kuelezea maumivu ya kichwa au sehemu ya juu ya shingo. Kichwa ni eneo linalopata maumivu ya mara kwa mara. Maumivu ya kichwa yana sababu nyingi,nyingine ni za kawaida lakini nyingine ni hatari kama vile , maambukizi kwenye ubongo, , ya shingo au mgongo, , baadhi ya madawa, pombe na mabad...

UGONJWA WA POLIO

Maelezo ya jumla Ugonjwa wa polio ni ugonjwa unaoathiri mishipa ya fahamu na kusababisha kupooza. Ugonjwa huu husababishwa na virusi (poliovirus) wanaoishi kwenye mfumo wa kumeng’enya chakula. Si kila mtu anayeambukizwa virusi hivi vya polio hupooza, watu wengi huwa na dalili za kawaida tu, kama;, , , maumivu ya mgongo, maumivu...