CHANJO YA UGONJWA WA POLIO

CHANJO YA UGONJWA WA POLIO

 • January 19, 2021
 • 1 Like
 • 55 Views
 • 0 Comments

Utangulizi

Ugonjwa wa polio ni ugonjwa unaoambukiwa na virusi vijuikanavyo kwa jina la kitaalamu polio virus.  Ugonjwa huu unaweza kumpata mtu yoyote katika umri wowote ila watoto walio chini ya miaka 15 huathirika zaidi. Virusi vya polio humwingia  mtu mwilini kwa kupitia chakula, au maji yaliyochafuliwa. Virusi hivi huishi kwenye utumbo na kuongezeka idadi yake kwa haraka sana. Pia huweza kushambulia maeneo mengine ya mwili yakiwemo ubongo na mishipa ya fahamu. Uambukizo wa mishipa ya fahamu husababisha kupooza sehemu moja au zaidi ya mwili.

Dalili za awali za ugonjwa wa polio ni;

Mtoto huweza kuishia na dalili  hizo au akaendelea na dalili zifuatazo;

 • Kukaza kwa shingo na mgongo
 • Kutoweza kutulia
 • Kuumwa na miguu au mikono

Baadhi ya watoto hupooza miili na wengine hufa kwa kupooza misuli inayosaidia kupumua.

Kinga ya polio

Ugonjwa wa polio unakingwa kwa chanjo ya polio ya matone (OPV) ambayo hutolewa motto anapozaliwa na katika wiki ya 6, 10 na 14. Chanjo ya sindano (IPV) hutolewa mtoto anapotimiza umri wa wiki 14  

Utoaji wa chanjo zaidi ya moja kwenye kila hudhurio;

 • Mtoto hupata chanjo zaidi ya moja wakati wa hudhurio inauhusu mtoto kupata kinga kamili haraka iwezekanavyo. Hii hutoa ulinzi wakati wa miezi ya kwanza ya hatari ya maisha ya mtoto. Kwa kupata chanjo zaidi ya moja kwa kila hudhurio humpunguzia mzazi/mlezi mahudhurio ya mara kwa mara katika kituo cha huduma.
 • Ni salama kwa mtoto kupokea chanjo za sindano zaidi ya moja kwa wakati mmoja.

Umuhimu wa chanjo

 • Chanjo huokoa maisha ya mtoto kwa kumkinga dhidi ya maradhi ambayo yanazuilika kwa chanjo
 • Tafiti mbalimbali zilizofanywa na wataalamu wa afya duniani zimeonesha kwamba chanjo ni salama
 • Jamii iliyopata chanjo huwa imekingwa dhidi ya milipuko ya magonjwa kama vile Surua
 • Chanjo huokoa muda na gharama ambazo zingetumika na mgonjwa/mzazi au mlezi pindi anapopata maradhi ambayo yangeweza kuzuilika hapo awali
 • Chanjo hulinda pia kizazi kijacho dhidi ya magonjwa yanayozuilika kwa chanjo kwani baadhi ya magonjwa yameweza kutokomezwa kama ilivyotokomezwa ndui (small pox)

Je, mtoto wako amekamilisha chanjo?

 • Mpeleke mtoto katika kituo cha kutolea huduma kwa kuzingatia ratiba ili aweze kupewa chanjo zote zinazostahili ikiwemo chanjo ya IPV
 • Chunguza kadi ya chanjo au muulize mhudumu wa afya ili kufahamu kama mtoto amekamilisha ratiba ya chanjo
 • Chanjo ni haki ya kila mtoto, mteja au mlengwa mpeleke mwanao/nenda kwenye kituo cha huduma za afya akapate chanjo

Ratiba ya chanjo

UMRI WA KUTOLEWA AINA YA CHANJO NJIA KIWANGO
Mara baada ya kuzaliwa BCG Ndani ya ngozi, Bega la kulia 0.05mls
OPV 0 Mdomoni Matone mawili
Wiki 6 OPV1 Mdomoni Matone mawili
Pentavalent 1 Ndani ya msuli, paja la kushoto (nje) 0.5mls
PCV 1 Ndani ya msuli, paja la kulia (nje) 0.5mls
Rota 1 Mdomoni 1.5mls
Wiki 10 OPV2 Mdomoni Matone mawili
Pentavalent 2 Ndani ya msuli, paja la kushoto (nje) 0.5mls
PCV 2 Ndani ya msuli, paja la kulia (nje) 0.5mls
Rota 2 Mdomoni 1.5mls
Wiki 14 OPV3 Mdomoni Matone mawili
Pentavalent 3 Ndani ya msuli, paja la kushoto (nje) 0.5mls
PCV 3 Ndani ya msuli, paja la kulia (nje) 0.5mls
IPV Ndani ya msuli, paja la kulia (nje) 0.5mls
Miezi 9 MR 1 Chini ya ngozi, mkono wa kushoto (nje) 0.5mls
Miezi 18 MR 2 Chini ya ngozi, mkono wa kushoto (nje) 0.5mls
Miaka 9 HPV 1 Ndani ya msuli, mkono wa kushoto (nje) 0.5mls
Miezi 6 baada ya HPV1 HPV2 Ndani ya msuli, mkono wa kushoto (nje) 0.5mls

 

Vyanzo

Imetoholewa kutoka katika kipeperushi kilichotayarishwa na wizara ya afya , maendeleo ya jamii, jinsia , watoto na wazee

‘’CHANJO NI ZAWADI YA MAISHA’’

 

 • Share:

Leave Your Comment