Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko
Maelezo ya jumla
Chuchu ya titi iliyopasuka – kina mama wengi waliojifungua siku za hivi karibuni, wanapatwa na maumivu kwenye chuchu katika wiki za kwanza kwa sababu ya kunyonyesha. Chuchu moja au zote zinaweza kuuma, zikawa nyekundu na kukunjamana na zinaweza kuvuja damu kwa kurahisi kama ngozi itapasuka. Chuchu ya titi iliyopasuka huwa inatokana na kushindwa kumshika mtoto vizuri wakati wa kunyonya na kwa sababu hiyo, mtoto ananyonya chuchu pekee badala ya titi. Wanawake wenye chuchu zilizo sawia ‘’flat’’ au zilizoingia kwa ndani wako kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata shuda hii. Kwa wakati fulani, chuchu ya titi iliyopasuka husababishwa na maambukizi ya fangasi.
Kama una chuchu ya titi iliyopasuka mwone daktari kama
Panga kumwona dakatri kama:
- Chuchu ni nyekundu, zinang’aa na kama zina vidude au uchafu mweupe mweupe
- Kuna eneo kwenye titi lililo jekundu na linauma
Unachoweza kufanya mwenyewe kama una chuchu ya titi iliyopasuka
Chuchu ya titi iliyopasuka hupona baada tu ya kuanza kumshika vizuri mtoto wakati wa kunyonya, jifunze mbinu bora za kunyonyesha
- Angalia unavyomshika mtoto wakati wa kunyonyesha. Ukimshikilia na kumwinua mwanao juu zaidi na kumtegemeza vizuri wakati wa kunyonya itasaidia kupunguza maumivu
- Mkumbatie mtoto, kichwa kikiwa juu kwenye sehemu ya mkunjo wa kiwiko cha mkono huku tumbo la mtoto likielekea tumbo lako na mdomo wa mtoto ukiwa usawa wa chuchu.
- Pitisha mkono wa mtoto uzunguke mwili wako na kumbuka kutegemeza vizuri sehemu ya matako.
- Hakikisha kuwa mtoto anaweka mdomo kuzunguka chuchu na mdomo wa mtoto umefunika kabisa sehemu nyeusi inayozunguka chuchu ‘’areola’’
- Ni vizuri kunyonyesha ukiwa umekaa mahala salama unapojisikia huru. Kaa kwenye kiti, weka mto nyuma ya mgongo na kisha egemea vizuri. Unaweza kukunja mguu kutegemeza mkono uliomkumbatia mtoto ili usichoke kama ilivyooneshwa hapo chini
- Nyonyesha mtoto kila anapohitaji ukimpatia chuchu ambayo ina afadhali kwanza, kwa sababu mwanzoni mtoto anavuta maziwa kwa nguvu sana. Vuta pumzi ndefu mtoto anapoiendea chuchu, chuchu ya titi iliyopasuka huwa inauma zaidi mwazoni mtoto anapoanza kunyonya.
- Unaweza kutumia ‘’lanolin ointment’’ ili kusaidia mipasuko iliyoingia ndani sana kupona. Mchanganyiko huu umetengenezwa maalumu kwa ajili ya kina mama wanaonyonyesha ili kupooza chuchu ya titi iliyopasuka. Paka kidogo ili kuikinga ngozi na kusaidia mipasuko kuona. Hauna haja ya kuifuta dawa hii kabla ya kunyonyesha.
- Kila baada ya kunyonyesha, osha chuchu kwa kutumia maji ya uvuguvugu na ukaushe vizuri.
- Kama chuchu zinauma sana tumia ‘’acetaminophen’’. Hii ni dawa ya maumivu na itakupunguzia maumivu na kukufanya ujilegeze ‘’relax’’ ili mwanao anyone vizuri. Tumia dozi angalau dakika 30 kabla ya kuanza kunyonyesha.
Kama una chuchu ya titi iliyopasuka omba ushauri zaidi wa daktari kama
Panga kuonana na daktari kama:
- Chuchu haziponi baada ya siku 2-3
Leave feedback about this