Magonjwa ya ngozi, kucha, nywele

CHUNJUA | VIGWARU | MASUNDOSUNDO

Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko

Maelezo ya jumla

Chunjua /vigwaru / masundosundo (warts) ni viuvimbe vidogo ambavyo huwa vinaota kwenye ngozi, vinamwonekano kama wa mkoliflawa (cauliflower) na wakati mwingine vinakuwa na kidoti cheusi katikati. Huwa vinasababishwa na virusi na mara nyingi huwa vinawapata watoto na vijana wadogo. Chunjua mara nyingi hutokea kwenye mikono au kwenye unyayo wa mguu, zinazotokea kwenye miguu zinaitwa plantar warts

Kama una chunjua mwone daktari

  • Panga kumwona daktari kama hauna uhakika kabisa kwamba huu uvimbe ambao umeanza kuota ni kigwaru
  • Kama zimeota kwenye uso au kuzunguka sehemu ya kutolea haja kubwa au sehemu za siri. Aina hii inahitaji matibabu maalumu

Unachoweza kufanya kuondoa chunjua

Chunjua mara nyingi huwa zinaondoka zenyewe, ila inaweza kuchukua muda mrefu na hata miaka. Ila matibabu ya mapema yatasaidia kuzuia zisisambae au kuzuia zisiume na kuziondoa kabisa

Kuna wart removers ambazo zina Salicylic acid, gels, lotions na mafuta ambayo hulainisha chunjua na inakuwa rahisi kuziondoa. Bidhaa zenye salicylic acid huwa zinaweza kuunguza ngozi kwa hiyo kuwa makini unapozipaka. Hakikisha kuwa unazipaka juu ya chunjua pekee, usipake kwenye ngozi inayozungukachunjua

  • Unaweza kutumia jiwe la kuogea na na maji ya uvuguvugu mpaka chujua itakapoondoka.
    1. Unaweza kuondoa chujua kwa kuiloweka kwenye maji na kisha kuisugua taratibu kwa kuumia jiwe la kuogea (pumice stone). Kwanza loweka chujua yako kwenye maji ya uvuguvugu kwa dakika kadhaa ili ilainike. Kisha tumia jiwe la kuogea kuisugua taratibu ili kuondoa tabaka la juu la ngozi yake.
    2. Ili kuhakikisha ngozi inayoizunguka chujua haiumizwi na dawa unayoiweka, paka mafuta (petroleum jelly) sehemu ya ngozi inayoizunguka. Kisha paka wart remover , baada ya hapo pafunike kwa bandage
    3. Mara 1 kwa wiki, sugua ngozi ya juu ya chujua kwa kutumia jiwe la kuogea. Endelea kutibu mpaka chujua itakapopotea.
  • Kwa wale ambao wana vigwaru kwenye miguu (plantar warts), unaweza kutumia insole laini ndani ya viatu ili kukupunguzia karaha unapotembea
  • Usikune au kuchuna chunjua zako, hii inaweza kusababisha zikasambaa zaidi. Usitafune au kuuma uma kucha zako, unaweza kuzisambaza kwa njia hii pia

    jiwe la kuogea
    Jiwe la kuogea

Ni vizuri kumwona dakitari kama una chunjua na:

  • Chunjua zako haziitikii matibabu unayozipatia
  • Kama chunjua zinabadilika rangi, zinavuja damu au zinakuwa nyekundu, za moto/zenye joto au zinauma

Vyanzo

https://medlineplus.gov/warts.html

Leave feedback about this

  • Quality
  • Price
  • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X