Uzazi wa mpango

DAWA ZA POVU NA JELI ZA KUPANGA UZAZI

Dawa za povu na jeli ni nini?

Dawa za povu na jeli ni dutu ya kuua mbegu za kiume inayoingizwa ndani ya uke, karibu na seviksi, kabla ya kufanya ngono.

  • Zinapatikana katika tembe zinazotoa povu, zinazoyeyuka au povu linalowekwa ukeni, makopo yaliyojazwa povu, utando unaoyeyuka au jeli
    • Jeli na povu kutoka kwenye makopo vinaweza kutumika vyenyewe, au pamoja na kiwambo, au na kondomu.
    • Utando, sapozitori, tembe zinazotoa povu, au sapozitori za povu zinaweza kutumika kipekee au na kondomu.

Hufanya kazi kwa kusababisha membreni ya seli za mbegu za kiume zivunjike na kuziua au kupunguza kasi ya mwendo wao. Hii huzuia mbegu za kiume zisikutane na yai.dawa za povu na jeli

Mambo Muhimu kuhusu dawa za povu na jeli

  • Dawa za povu na jeli huingizwa ndani ya uke muda mfupi kabla ya kufanya ngono.
  • Zinahitaji kutumiwa kwa usahihi kwa kila tendo la ngono ili kupata ufanisi mkubwa
  • Moja kati ya njia za kuzuia mimba zenye ufanisi mdogo zaidi.

Zinaweza kutumiwa kama njia ya msingi ya kuzuia mimba au pamoja na njia nyingine ili kuongeza ufanisi – pamoja na kondomu au viwambo.kuingiza dawa za povu na jeli

Madhara, Faida Kiafya, na Hatari Kiafya

Madhara

Baadhi ya watumiaji wameripoti yafuatayo:

  • Kuwashwa ndani au kuzunguka uke au uume na vidonda ukeni

Faida za kiafya zianzojulikana

Husaidia kuzuia:

  • Hatari ya kupata mimba

Hatari kiafya zinazojulikana

  • Maambukizi kwenye njia ya mkojo, hasa wakati wa kutumia dawa za povu na jeli mara 2 au zaidi kwa siku
  • Kutumia mara kwa mara dawa za povu kunaweza kuongeza uwezekano wa kupata VVU – vidonda

Kwanini Baadhi ya Wanawake Wanasema Wanapenda Dawa za povu na jeli

  • Zinadhibitiwa na mwanamke
  • Hazina madhara ya vichocheo
  • Huongeza kilainisho ukeni
  • Zinaweza kutumiwa bila kumwona mtoa huduma ya afya

Zinaweza kuwekwa kabla ya wakati na haziingilii ngonodawa za povu na jeli

Matumizi ya dawa za povu na jeli?

Namna ya kutumia povu na jeli ukeni

  • Angalia tarehe ya mwisho wa kutumia na epuka kutumia dawa za povu na jeli zilizopitisha muda wake wa kutumika.
  • Safisha mikono kwa sabuni laini na maji safi ikiwezekana.
    • Povu: tikisa kopo la povu vya kutosha. Bonyeza kutoa povu kutoka kwenye kopo au tyubu kumwagia kwenye kifaa cha plastiki cha kuingizia. Ingiza kifaa hicho ndani ya uke, karibu na seviksi, na sukuma kizibuo.
    • Tembe, sapozitori, jeli: Ingiza dawa za povu ndani ya uke, karibu na seviksi, kwa kutumia kifaa cha kuingizia au vidole.
    • Utando: Kunja utando sehemu mbili na ingiza kwa vidole vikavu (au vinginevyo utando utanata kwenye vidole badala ya seviksi).
  • Ni wakati gani wa kuweka dawa za povu na jeli ukeni
    • Povu: Wakati wowote chini ya saa moja kabla ya kufanya ngono.
    • Tembe, sapositori, jeli, utando: Kati ya dakika 10 na saa moja kabla ya ngono, kutegemea aina.
    • Ingiza dawa ya povu na jeli kabla ya kila tendo la ngono
  • Usisafishe uke baada ya ngono
    • Haishauriwi kusafi sha kwa sababu utaondoa dawa za povu na jeli na pia kuongeza hatari ya magonjwa ya ngono.

Kama ni lazima usafishe, subiri angalau kwa saa 6 baada ya ngono kabla ya kusafisha.

Imani potofu kuhusu dawa za povu na jeli

Dawa za povu na jeli:

  • Hazipunguzi majimaji ukeni au kufanya wanawake watokwe damu wakati wa ngono.
  • Hazisababishi saratani ya seviksi au kilema cha kuzaliwa.
  • Hazizuii magonjwa yanayoambukizwa kwa ngono.
  • Hazibadili hamu ya ngono kwa wanaume au wanawake au kupunguza raha ya ngono kwa wanaume wengi.
  • Hazisitishi hedhi kwa wanawake

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/001946.htm

Leave feedback about this

  • Quality
  • Price
  • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X