1. Home
  2. ELECTROCARDIOGRAM
ELECTROCARDIOGRAM

ELECTROCARDIOGRAM

  • November 17, 2020
  • 0 Likes
  • 298 Views
  • 0 Comments

Ni nini?

Electrocardiogram – Hufupishwa kama EKG au ECG – ni kipimo kinachopima shughuli ya umeme kwenye moyo. Kwa kila pigo la moyo, wimbi la umeme husafiri kwenye moyo. Wimbi hili la umeme husababisha misuli ya moyo kukaza na kusukuma damu. Wakati wa pigo la moyo la kawaida, ECG huonesha ni muda gani anaotumika kwa wimbi hilo kusafiri kutoka kwenye vyumba vya juu vya moyo, mpaka vyumba vya chini.

Vyumba viwili vya juu (atria) hutengeneza wimbi la kwanza linaloitwa “Wimbi P” – Kisha hufuatiwa na  mstari mlalo wakati umeme ukivuka kwenda kwenye vyumba vya chini.Vyumba vya chini (ventrikali ya kulia na kushoto) hutengeneza wimbi linalofuata linaloitwa “QRS complex”. Wimbi la mwisho au “Wimbi T ” huwakilisha kuishilia kwa wimbi la umeme au wakati wa kupumzika kwa ventrikali, wakati ambao moyo hausukumi damu.

Kwa nini kipimo hiki kifanyike?

ECG hutoa aina mbili ya taarifa . Kwanza, kwa kupima muda kwenye ECG, daktari anaweza kutambua muda unaotumika kwa wimbi la umeme kusafiri toka sehemu moja ya moyo mpaka nyingine. Hii humsaidia daktari kutambua kama shughuli ya umeme kwenye moyo ni ya kawaida, polepole, harakaharaka au isio kawaida. Pili, kwa kupima kiasi cha umeme unaopita kwenye misuli ya moyo, mtaalamu wa moyo anaweza kujua kama sehemu ya moyo imepanuka, kubwa au inafanyishwa kazi zaidi ya ilivyo kawaida.

Je, kipimo hiki kinasababisha mamivu?

Hapana. Hakuna maumivu au hatari yoyote inayotokana na kufanyiwa electrocardiogram. Wakati stika za ECG zinapoondolewa, kunaweza kuwa na usumbufu mdogo.

Je, ni hatari?

Hapana. Mashine ya ECG hurekodi umeme pekee. Haitoi umeme.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/003868.htm

  • Share:

Leave Your Comment