FISTULA KWENYE NJIA YA HAJA KUBWA

Maelezo ya jumla

Fistula kwenye njia ya haja kubwa ni mferiji usio wa kawaida unaotengenezeka kuunganisha njia ya haja kubwa na ngozi. Watu waliokuwa na jipu kwenye njia ya haja kubwa wana uwezekano mkubwa wa kupata shida hii. Dalili zake ni maumivu, kutokwa uchafu, damu au usaha, kuwashwa sehemu ya haja kubwa, uvimbe,wekundu na kuchubuka kwa ngozi inayozunguka sehemu ya kutolea haja kubwa.

Kama fistula itapata maambukizi, mgonjwa atapata homa na kuhisi baridi pia. Fistula hutambuliwa kwa kuchunguza eneo lililoathirika. Matibabu ya fistula kwenye njia ya haja kubwa yanatofautiana. Matibabu hujumuisha dawa na upasuaji. Matarajio ya kupona ni makubwa baada ya upasuaji.

fistula kwenye njia ya haja kubwaNi nini dalili za fistula kwenye njia ya haja kubwa?

Wagonjwa wenye fistula kwenye njia ya haja kubwa ,wanaweza kupata dalili zifuatazo:

 • Maumivu
 • Kutokwa uchafu, damu au usaha
 • Kuwashwa kwenye eneo linalozunguka njia ya kutolea haja kubwa
 • Uchovu
 • Uvimbe, wekundu na kuchubuka kwa ngozi inayozunguka njia ya haja kubwa
 • Kama fistula itapata maambukizi, homa na kuhisi baridi

Matatizo mengine ya kiafya yanaweza kusababisha dalili hizi. Ni daktari pekee anayeweza kutofautisha kwa uhakika. Mtu yeyote mwenye dalili hizi ,anapaswa kumwambia daktari ,ili tatizo ligunduliwe na aanze matibabu mapema iwezekanavyo.

Nani yuko kwenye hatari zaidi ya kupata fistula kwenye njia ya haja kubwa?

Sababu zifuatazo huongeza uwezekano wa kupata fistula kwenye njia ya haja kubwa. Ikiwa una moja kati ya sababu hizi zinazoongeza hatari, jadiliana na daktari wako:

 • Kuvimba kwa utumbo mpana au ugonjwa mwingine unaosababisha matumbo kuvimba, kwa mfano ugonjwa unaoitwa crohn’s disease
 • Kupata kinyesi kigumu
 • Kuharisha kwa muda mrefu

Utambuzi wa fistula kwenye njia ya haja kubwa

 • Uchunguzi wa mwili: Utambuzi wa fistula mara nyingi hufanyika kwa kuchunguza eneo linalozunguka njia ya haja kubwa, daktari atatafuta uwazi kwenye ngozi, na kisha kutambua kina na mwelekeo wa fistula.
 • Anoscope: Kama hakuna ishara za fistula kwenye ngozi inayoizunguka njia ya haja kubwa, daktari atatumia chombo kinachojulikana kama anoscope ili kuona ndani ya njia ya haja kubwa na rektamu.
 • Uchunguzi wa damu, x-rays, na colonoscopy: Wakati wowote daktari anapopata fistula, vipimo zaidi kama vile vipimo vya damu, x-rays, na colonoscopy vinahitajika kuhakikisha kuwa hakuna ugonjwa wa crohn

Magonjwa yenye dalili zinazofanana na fistula kwenye njia ya haja kubwa

 • Magonjwa yanayosababisha kuvimba kwa matumbo (Inflammatory bowel disease), kama Crohn’s disease
 • Kaswende
 • Herpes simplex

Wakati gani utafute matibabu ya haraka?

Mwone mtoa huduma ya afya kama unapata dalili za fistula kwenye njia ya haja kubwa. Kama unapata mojawapo ya dalili zifuatazo, fika kwenye kituo cha huduma za afya haraka iwezekanavyo:

Uchaguzi wa matibabu

Mara nyingi, matibabu ya Fistula kwenye njia ya haja kubwa hutofautiana kulingana na uwepo wa ugonjwa wa Crohn au maambukizi. Matibabu hujumuisha dawa na upasuaji.

 • Kama kuna ugonjwa wa Crohn, aina mbalimbali za dawa ikiwa ni pamoja na antibiotics Mara nyingi dawa hizi hutibu maambukizi na kuponya fistula.
 • Ikiwa ugonjwa wa Crohn haupo, bado waweza kutumia antibiotics.
 • Kama antibiotics hazijafanya kazi vyema, upasuaji ni tiba ya kuaminika. Daktari wa upasuaji,ataupasua mfeji wa fistula ili upone.
 • Kama mgonjwa ana maambukizi, yanatakiwa kutibiwa kabla ya upasuaji kufanyika. Mara nyingi daktari huweka uzi toka upande mmoja wa fistula mpaka mwingine ili kuruhusu usaha kutoka nje.

Kuzuia kutokea kwa fistula kwenye njia ya haja kubwa

Hakuna njia ya kuzuia Fistula kwenye njia ya haja kubwa kwa sababu, sababu ya maambukizi huwa haijulikanai .

Nini cha kutarajia?

Matarajio ni mazuri sana baada ya upasuaji .

Matatizo yanayoweza kutokea

Mara nyingi matatizo yanayotokana na fistula kwenye njia ya haja kubwa husababishwa na upasuaji,hii inaweza kuwa maambukizi, kushindwa kuzuia haja au kujirudia rudia kwa fistula kwenye njia ya haja kubwa.

Vyanzo

http://www.fascrs.org/patients/conditions/anal_abscess_fistula/

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi