HOMA YA MAPAFU (NIMONIA):Sababu,dalili,matibabu

Maelezo ya jumla

Ugonjwa wa homa ya mapafu (Nimonia) ni ugonjwa wa mfumo wa upumuaji unaosababisha kuvimba kwa mapafu. Mtu anaweza kupata homa ya mapafu akiwa katika kituo cha afya au akiwa nje ya kituo cha afya – kwenye jamii.

Ni zipi dalili za Ugonjwa wa homa ya mapafu (Nimonia)?Homa ya mapafu

Dalili zinazowapata zaidi wagonjwa wa homa ya mapafu ni kama zifuatazo:

 • Kukohoa (kwa baadhi ya aina za homa ya mapafu, unaweza kukohoa makohozi ya rangi ya kijani au njano, au unaweza kuwa na makohozi yaliyochanganyika na damu)
 • Homa, inaweza kuwa ya kadri au kali
 • Kutetemeka
 • Kupata shida kupumua (inaweza kutokea unapopanda ngazi)

Dalili za nyongeza ni kama zifuatazo:

Ni nini sababu ya Ugonjwa wa homa ya mapafu (Nimonia)?

Ugonjwa wa homa ya mapafu (Nimonia) ni ugonjwa unaowaathiri watu mamilioni kila mwaka. Vimelea wanaoitwa bakteria, virusi, na fangasi wanaweza kusababisha Ugonjwa wa homa ya mapafu (Nimonia).

Namna ambavyo unaweza kupata ugonjwa wa homa aya mapafu:

 • Bakteria au virusi wanaoishi kwenye pua, mianzi ya pua, au mdomo kusambaa kwenda kwenye mapafu
 • Unaweza kuvuta baadhi ya vimelea hawa moja kwa moja mpaka kwenye mapafu
 • Unaweza kuvuta ndani chakula, majimaji, matapishi, au vimeng’enya vingine kutoka mdomoni mpaka kwney mapafu (homa ya mapafu inayosababishwa na kupaliwa)

Ugonjwa wa homa ya mapafu (Nimonia) unaosababishwa na bakteria huwa na dalili kali zaidi. Kwa wazee, bakteria ndio husababisha visa vingi vya Ugonjwa wa homa ya mapafu (Nimonia).

 • Vimelea wanaosababisha zaidi Ugonjwa wa homa ya mapafu (nimonia) kwa watu wazima ni streptococcus pneumoniae
 • Aina nyingine ya Ugonjwa wa homa ya mapafu (nimonia) isiyo ya kawaida (atypical pneumonia) inasababishwa na vimelea kama Legionella pneumophila, Mycoplasma pneumoniae, na Chlamydophila pneumoniae.
 • Watu wenye upungufu wa kinga mwilini (inaweza kuwa kwa sababu ya ugonjwa wa UKIMWI au baada ya kutumia dawa fuani zinazopunguza kinga ya mwili, hupatwa na Ugonjwa wa homa ya mapafu (Nimonia) unaosababishwa na Pneumocystis jiroveci pneumonia
 • Staphylococcus aureus, Moraxella catarrhalis, Streptococcus pyogenes, Neisseria meningitidis, Klebsiella pneumoniae, au Haemophilus influenzae ni aina nyingine za bateria wanaowea kusababisha Ugonjwa wa homa ya mapafu (nimonia).
 • Ugonjwa wa kifua kikuu unaweza kusababisha homa ya mapafu kwa baadhi ya watu, hasa wale wenye upungufu wa kinga mwilini

Virusi pia husababisha ugonjwa wa mapafu mara kwa mara, hasa kwa watoto wachanaga na watoto wadogo.

Ni nani yuko kwenye hatari zaidi ya kupata Ugonjwa wa homa ya mapafu (Nimonia)?

Mambo yanayoongeza hatari ya kupata Ugonjwa wa homa ya mapafu (Nimonia) ni pamoja na:

Ni wakati gani unapaswa kutafuta usaidizi wa daktari?Nimonia

Onana na daktari kama:

 • Unaona dalili za mfumo wa upumuaji zinazidi kuwa mbaya
 • Unapata shida kupumua, kutetemeka au unatapata homa isiyoisha
 • Unapumua haraka haraka au unapata maumivu wakati wa kupumua
 • Una toa kohozi lenye damu au lililobadilika rangi na kuwa kama kutu
 • Mamumivu ya kifua yanayozidi kuwa mabaya zaidi unapokohoa au kuvuta hewa kwa nguvu
 • Kutokwa na jasho jingi au kupungua uzito bila sababu inayofahamika
 • Una dalili za Ugonjwa wa homa ya mapafu (Nimonia) na una upungufu wa kinga mwilini, kama vile UKIMWI au kama unatumia dawa za tibakemikali

Watoto wadogo wenye Ugonjwa wa homa ya mapafu (Nimonia) wanaweza wasiwe na kikohozi. Onana na daktari kama mtoto anatoa sauti za miguno au kama eneo la kifua/mbavu zinabonyea ndani wakati wa kuvuta pumzi.

Utambuzi wa ugonjwa wa homa ya mapafu (nimonia)

Kama una ugonjwa wa homaya mapafu, unaweza kupata shida au ugumu kupumua, au unapumua haraka haeaka sana. Unaweza kusikia kifua kikipiga kelele unaposikiliza kwa kutumia kifaa cha kusikilizia – stethoscope. Aina nyingine ya sauti zisizo za kawaida zinaweza pia kusikika kupitia stethoscope au kwa kugongagonga kifia kwa kutumia kidole (madktari wanafahamu njia hii). Mtaalamu wa afya anaweza kuagiza upige picha ya eksireu ya kifua kama anadhani una Ugonjwa wa homa ya mapafu (Nimonia). Baadhi ya wagonjwa wanaweza kuhitaji vipimo vingine. Kama vile:

 • Vipimo vya damu vya kuhesabu na kuangalia idadi ya seli kwenye damu – CBC – kipimo hiki hufanyika kuangalia kiwango cha seli nyeupe kwenye damu
 • Kipimo cha kuangalia kiwango cha aina mbalimbali za gesi kwenye damu – Arterial blood gases – hiki husaidia kuangalia kiwango cha hewa ya oksijeni inayofika kwenye damu na mapafu
 • Picha za CT scan za kifua
 • Kipimo cha kuchunguza makohozi kwa kuyaweka katika kiotesho ili kuoteza bakteria waliomo – culture AU kutumia njia nyingine kupaka rangi bakteria ili kuwatambua – gram stain

Uchaguzi wa matibabu ya ugonjwa wa homa ya mapafu

Daktari atahitaji kwanza kuamua kama unahitaji kulazwa hospitalini au akuruhusu na dawa ukatumie nyumbani. Kama ukitibiwa hospitalini, utaongezewa maji kupitia kwenye mishipa na dawa za antibiotiki kupitia kwenye mishipa, utapewa hewa ya oksijeni, na yawezekana ukawekwa katika mashine ya kukusaidia kupumua kama hali yako ni mbaya sana.

Ni muhimusana kwa dawa za antibiotiki kuanzishwa mapema baada tu ya kulazwa. Kuna uwezekano mkubwa kulazwa hospitalini kama:

 • Una tatizo jingine la kiafya na una Ugonjwa wa homa ya mapafu (nimonia)
 • Una dalili kali sana za ugonjwa homa ya mapafu
 • Unashindwa kujihudumia mwenyewe ukiwa nyumbani, au unashindwa kula au kunywa
 • Una umri zaid ya mika 65 au ni mtoto mdogo
 • Umekuwa ukitumia dawa za antibiotiki ukiwa nyumbani lakini hali inazidi kuwa mbaya

Ata hivyo, watu wengi wanaweza kutibiwa nyumbani. Kama ugonjwa wa homa aya mapafu umesababishwa na bakteria, daktari atajaribu kukuponya kwa kutumia antibiotiki. Inaweza kuwa ngumu kwa mtaalamu wa afya kutambua kama una aina ya ugonjwa iliyosababishwa na bakteria au virusi, kwa hiyo unaweza kupewa antibiotiki. Kwa wagonjwa wa homa ya mapafu wasio na dalili kali na wana afya njema, mara nyingi wanatibiwa kwa kupewa dawa za antibiotiki za kumeza (azithromycin, clarithromycin, or erythromycin).

Wagonjwa wa homa ya mapafu wenye matatizo mengine ya kiafya kama vile ugonjwa wa moyo, kuziba kwa njia ya hewa, ugonjwa wa figo, au kisukari mara nyingi wanapatiwa dawa zifuatavyo:

 • Fluoroquinolone (levofloxacin), sparfloxacin), gemifloxacin), au moxifloxacin)
 • Kiwango cha juu cha dose ya amoxicillin au amoxicillin-clavulanate, pamoja na antibiotiki aina ya macrolide (azithromycin, clarithromycin, or erythromycin)
 • Antibiotiki aiana ya Cephalosporin (kwa mfano, cefuroxime or cefpodoxime) pamoja na antibiotiki aina ya macrolide (azithromycin, clarithromycin, or erythromycin)

Kama sababu ya ugonjwa wa homa ya mapfu ni virusi, kumpatia mgonjwa dawa za antibiotiki hazitasaidia kumtibu. Kwa baadhi ya nyakati daktaria anaweza kuamua kukupatia dawa za kudhibiti virusi (antivirals medication).

Unaweza kufanya mambo yafuatayo nyumbani ili kupata nafuu:

 • Kunywa maji ya kutosha ili kufanya kamasi na makohozi kuwa laini ili yatoke
 • Pumzika vizuri. Tafuta mtu akusaidie kufanya shughuli zako kama inawezekana
 • Usitumie dawa za kudhibiti kikohozi bila kuzungumza na daktari. Dawa za kuzuia kikohozi zinaweza kusababisha iwe ngumu kwa mwili kutoa makohozi yanayotakiwa kutoka.
 • Dhibiti homa ya mwili kwa kutumia dawa za Aspirin, ibuprofen, naproxen, au Usitumie dawa za aspirin kwa watoto.

Matarajio ukiwa na homa ya mapafu

Baada ya matibabu, wagonjwa wengi wanapata nafuu ndani ya wiki 2. Wazee au watu wenye matatizo mengine ya kiafya wanaweza kuhitaji muda zaidi ili kupona.

Watu wenye uwezekano mkubwa wa kupata matatizo ya homa ya mapafu ni pamoja na:

 • Wazee au watoto wadogo
 • Watu wenye upungufu wa kinga ya mwili
 • Watu wenye matatizo mengine ya kiafya kama vile kisukari au kuharibika kwa ini (sirosisi)

Daktari anaweza pia kuhitaji upige picha nyingine ya eksirei ya kifua ili kuona kama kifua kimepona vizuri baada ya kutumia dawa za antibiotiki. Hata hivyo, inaweza kuchuku wiki nyingi kwa picha ya eksirei kurusi katika hali ya kawaida.

Matatizo yanayoweza kutokea ukiwa na nimonia

Yafuatayo ni baadhi ya amatatizo yanayoweza kutokana na ugonjwa wa homa aya mapafu:

 • Kushindwa kwa mfumo wa upumuaji – kushindwa kupumua – hii inasababisha kuhitajika kwa mashine ya kusaidia kupumua – ventilator
 • Kutokewa na jipu kwenye mapafu – hii hutokea kwa nadra sana, lakini ni tatizo hatari sana linaloweza kutokana na hoama ya mafu.
 • Kusambaa kwa maambukizi mwilini – hali hii inasababisha mishipa na tishu za mwili kuvimba – na inaweza kusababisha viungo mbalimbali vya mwili kushindwa/kuacha kufanya kazi

Kuzuia ugonjwa wa homa ya mapafu (nimonia)

Osha mikono mara kwa mara, hasa baada ya kupuliza au kupenga kamasi, kutoka chooni, kumsafisha mtoto aiyejinyea, na kabla ya kula au kuandaa chakula. Usivute sigara, tumbaku huharibu uwezo wa mapafu kupambana na maambukizi. Chanjo zinaweza kusaidia kupunguza uwezekano wa kupata Ugonjwa wa homa ya mapafu (Nimonia) kwa watoto, wazee, na watu wenye ugonjwa wa kisukari, pumu, kimwi, saratani, au matatizo mengine sugu ya kiafya.

 • Chanjo aina ya pneumococcal vaccine – inapunguza uwezekano wa kupata Ugonjwa wa homa ya mapafu (Nimonia) unaosababishwa na streptococcus pneumoniae
 • Chanjo ya mafua – flu vaccine – hii inazuia homa ya mapafu au matatizo mengine yanayosababishwa na virusi vya influenza. Chanjo hii inaweza kutolewa kila mwaka kwa sababu ya mabadiliko ya virusi kila mwaka
 • Chanjo – Hib vaccine -inazuia Ugonjwa wa homa ya mapafu (Nimonia) kwa watoto unaosababishwa na Haempphilus influenzae type b

Kama una saratani au maambukizi ya VVU, ongea na daktari kuhusu njia mbadala za kujikinga na homa ya mapafu na maambukizi mengine

Vyanzo

http://www.nlm.nih.gov/medlineplus/ency/article/000145.htm

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi