HOMA YA MGUNDA:Sababu, dalili, matibabu, kuzuia

Maelezo ya jumla

Homa ya mgunda (Leptospirosis) ni maambukizi yanayotokea unapokutana na bakteria aina ya leptospira.

Ni zipi dalili za ugonjwa wa homa ya mgunda?Homa ya mgunda

Dalili zinaweza kuanza kuonekana baada ya siku 2 mpaka 26 (kwa wastani ni siku 10), na zinaweza kujumuisha:

Dalili zinazotokea mara chache ni pamoja na:

Ni nini sababu ya ugonjwa wa homa ya mgunda?

Bakteria aina ya Leptospira wanapatikana kwenye maji ambayo yamechafuliwa na mkojo wa wanyama. Maambukizi ya aina hii yanapatikana katika maeneo yenye hali ya joto.

Homa ya mgunda haisambai kutoka kwa mtu mmoja mpaka mwingine, isipokua kwa nadra sana, kwa baadhi ya visa. Kwa kawaida homa ya mgunda inasambaa kwa ngono, maziwa ya mama, au kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto aaliye tumboni.

Mambo yanayoongeza hatari ya kupata maambukizi ya homa ya mgunda?

Maji yaliyochafuliwa na mkojo
Maji yaliyochafuliwa na mkojo wa wanyama

Yafuatayo ni mambo yanayoongeza hatari ya kupata maambukizi ya homa ya mguda:

 • Kazi unayofanya – Wakulima, wachungaji wa wanyama, wanaochinja wanyama, wanaotega mitego ya kuwindia, wataalamu wa mifugo, wanaokata miti mwituni, wanaofanya kazi ya kusafisha mitaro ya maji machafu, wanaofanya kazi kwenye mashamba ya mchele, na wanajeshi.
 • Shughuli za kimichezo unazofanya – Kuogelea kwenye maji ya mito au mabwawa, kuendesha mtumbi, kuendesha baiskeli kwenye maeneo yenye joto hasa pemebezi mwa mji.
 • Kukutana na maambukizi nyumbani – kukutana na mbwa, mifugo wa kufugwa, maeneo ya kukusanya maji ya mvua ili yatumike kwa matumizi ya nyumbani, na panya wenye maambukizi.

Ugonjwa wa homa ya mgunda ni nadra sana Tanzania.

Nani yuko kwenye hatari zaidi ya kupata homa ya mgunda?

Milipuko ya ugonjwa wa homa ya mgunda inatokana na kukutana na maji yaliyochafuliwa na mkojo wa wanyama wenye maambukizi. Aina nyingi za wanyama wanaweza kubeba bakteria wanaosababisha ugonjwa huu; baadhi wanaweza kuwa wagonjwa na wengine wanaweza wasiwe na dalili yoyote.

Bakteria aina ya Leptospira amewahi kupatikana kwenye ng’ombe, nguruwe, farasi, mbwa, panya, wanyama wa mwituni.

Wanadamu wanaambukizwa kupitia maji, chakula, au udongo uliochafuliwa na mkojo wa wanyama hawa walioambukizwa.

Hii inaweza kutokea kwa kula chakula au kunywa maji au kwa kupitia kwenye ngozi, hasa maeneo yenye utando ute kama vile macho au pua au kupitia kidonda kwenye ngozi. Aina hii ya ugonjwa sio kawaida kusambaa kutoka kwa mtu mmoja mpaka mwingine.

Utambuzi

Kwa kawaida mgonjwa mwenye homa ya mgunda, dalili huanza kati ya siku 2 – 30 baada ya maambukizi ya bakteria. Dalili kali huanza mapema siku ya 4 – 6 ya ugonjwa kulingana na ukali wa vimelea na kingamwili ya mgonjwa.

Kwa sababu dalili za ugonjwa haziko bayana, sio rahisi kuutambua ugonjwa kwa dalili au ishara pekee. Vipimo vya maabara vinapaswa kufanyika kwa mgonjwa anayepata dalili za ghafla za homa, kutetemeka, wekundu wa macho, maumivu ya kichwa, maumivu ya misuli na manjano kwenye macho au ngozi na wanayo historia ya kukutana na wanyama, mchanga au maji yaliyochafuliwa na mkojo wa wanyama.

Bakteria wanaosababisha ugonjwa huu wanapatikana kwenye damu na majimaji ya uti wa mgongo kwa siku 7 mpaka 10 za mwanzo za ugonjwa na baadae kwenye mkojo. Kwa hiyo, katika hatua za mwanzo za ugonjwa, kipimo cha damu au majimaji ya uti wa mgongo kinapendelewa zaidi kwa ajili ya culture.

Ni wakati gani unapaswa kuomba msaada wa kitabibu?

Onana na mtaalamu wa afya kama una dalili yoyote au jambo lolote linaloongeza hatari ya kupata homa ya mgunda.

MatibabuHoma ya mgunda

Dawa za kupitibu homa ya mgunda ni pamoja na:

 • Ampicillin
 • Azithromycin
 • Ceftriaxone
 • Doxycycline
 • Penicillin

Baadhi ya visa vinaweza kusababisha ugonjwa mkali na mgonjwa akahitaji kuwekwa akatika uangalizi maalumu au katika chumba cha wagonjwa mahututi

Kuzuia

Hatari ya kupata ugonjwa wa homa ya mgunda inaweza kupunguzwa kwa kujizuia kuogelea au kutembea ndani ya maji yaliyochafuliwa na mkojo wa wanyama. Kuvaa nguo za kujikinga au viatu vya kujikinga husaidia kuwalinda watu wanaokutana au wanaogusa maji au udongo kama sehemu ya kazi au sehemu ya michezo wanayoshiriki.

Matarajio

Matarajio kwa ujumla ni mazuri. Hata hivyo, baadhi ya visa vinaweza kusababisha hali kali ya ugonjwa na inaweza kutishia maisha kama homa ya mgunda isipotibiwa vizuri.

Matatizo yanayoweza kutokea

Baadhi ya visa vya homa ya mgunda vinaweza kusababisha matatizo yafuatayo (kwa nadra);

 • Mjibizo mbaya unaotokea baada ya kupewa dawa aina ya penicillin kama sehemu ya matibabu ya ugonjwa – mgonjwa anaweza kuonekana mgonjwa zaidi
 • Kuvimba kwa utando unaofunika uti wa mgongo – meningitis
 • Kuvuja damu sana

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/001376.htm

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi