JINSI YA KUKADIRIA KIASI CHA MLO KWA KUTUMIA MIKONO

Jinsi ya kukadiria kiasi cha mlo kwa kutumia mikono yakoMlo

Mikono yako inaweza kutumika kukadiria kiasi cha chakula unachotakiwa kula kwa mlo mmoja. Ufuatao ni muongozo wa kukadiria kiasi cha mlo kwa kutumia mikono kama kipimo:

  • Vyakula vya nafaka, mizizi na ndizi kama vile ugali, wali, viazi: Kiasi sawa na ukubwa wa ngumi mojaVyakula vya nafaka, mizizi na ndizi kama vile ugali, wali, viazi:
  • Matunda: Kiasi cha matunda ni sawa na ngumi moja; mfano saizi ya kati ya chungwa, embe, kipande cha papai, tikiti-maji, au nanasi.Matundo
  • Mboga-mboga: Kiasi cha mbogamboga kiwe kingi zaidi, kadiria kiasi cha kuweza kujaa katika viganja vya mikono yote miwili. Pendelea kula zaidi mboga mboga ambazo hazina kabohaidreti kama mchicha, kabichi lettuce. Mboga zenye kabohaidreti ni kamaMbogamboga
  • Vyakula vya jamii ya kunde na vile vyenye asili ya wanyama: Kiasi sawa na ukubwa wa kiganja cha mkono wako na unene uwe sawa na wa kidole kidogo cha mkono wakoVyakula vya jamii ya kunde
  • Mafuta: Ncha ya kidole gumba. Endapo unapendelea kunywa maziwa wakati wa mlo, hakikisha unakunywa maziwa yaliopunguzwa mafuta (low fat), kiasi kisizidi millilita 250Mafuta

Vyanzo

https://www.tfnc.go.tz/publications/9

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi