JIPU KWENYE JINO: Sababu, dalili, matibabu

Maelezo ya jumla

Jipu kwenye jino ni mkusanyiko wa usaha unatokona na maambukizi kwenye sehemu ya kati ya jino.

Ni zipi dalili za jipu kwenye jino?

jipu kwenye jino

Dalili kuu ni maumivu makali ya jino. Ma

Dalili nyingine ni pamoja na:

 • Kuhisi ladha chungu mdomoni
 • Harufu mbaya ya kinywa
 • Kujisikia vibaya au kujihisi unaumwa
 • Homa
 • Maumivu wakati unapotafuna
 • Kujihisi vibaya au maumivu unapopigwa au kula kitu cha moto au baridi
 • Kuvimba kwa tezi za shingo
 • Kuvimba kwa sehemu ya juu au chini ya taya – nidalili ya hatari

Ni nini husababisha jipu kwenye jino?

Jipu kwenye jino ni matokeo ya kuoza kwa meno. Linaweza pia kutokana na jeraha kwenye jino, kama vile wakati jino linapovunjika. Kuwepo kwa tobo kwenye jino kunaruhusu bakteria kuingia na kuambukiza sehemu ya kati kati ya jino. Maambukizi yanaweza kusambaa kutoka kwenye mzizi wa jino na mifupa inayotegemeza jino.

Maambukizi yanasababisha mkusanyiko wa usaha (usaha ni mkusanyiko wa tishu zilizokufa, zilizohai na bakteria waliokufa, na chembe nyeupe za damu) na kuvimba kwa tishu za jino. Hii husababisha maumivu ya jino. Kama sehemu ya ndani ya jino ikifa, maumivu yanaweza kuisha, isipokuwa pale tu, jipu linapoanza. Hii inatokea kama maambukizi yatabakia na kuendelea kusambaa.

Utambuzi

Mgonjwa atahisi maumivu daktari atakapogusa jino. Kuuma meno au kufunga mdomo kwa nguvu pia husababisha maumivu. Fizi zinaweza kuwa zimevimba na kuwa nyekundu na zinaweza kuvuja majimaji mazito.

Ni wakati gani unapaswa kutafuta usaidizi wa kitabibu?

Ongea na daktari kama una maumivu ya jino yasiyoisha na yanayoputaputa.

Uchaguzi wa matibabujipu kwenye jino

Lengo la matibabu ni kuponya maambukizi, kuokoa jino, na kuzuia matatizo mengine yasitokee.

Dawa za antibiotiki zinaweza kutolewa ili kupambana na maambukizi. Maji ya uvuguvugu yaliyoiwa chumvi hupunguza maumivu baada ya kusukutua. Dawa za kupunguza maumivu kama vile “ibuprofen” husaidia kupunguza homa na maumivu.

USIWEKE dawa ya “aspirin” moja kwa moja kwenye jino au fizi, kwa sababu inasababisha usumbuu kwenye tishu na inaweza kusababisha vidonda.

Kama kuna maambukizi makali, jino linaweza kung’olewa au upasuaji unaweza kufanyika ili kukamua jipu. Baadhi ya watu watahitajika kulazwa hospitalini

Matarajio

Kama jipu la jino lisipotibiwa, hali inaweza kuzidi kuwa mbaya na inaweza kusababisha matatizo ambayo yanayweza kutishia maisha. Matibabu ya haraka mara nyingi humponya mgonjwa. Kwa visa vingi, jino linaokolewa.

Matatizo yanayoweza kutokea

Yafuatayo ni matatizo yanayoweza kutokea kwa sababu ya jipu kwenye jino:

 • Kupoteza jino
 • Kusambaa kwa maambukizi kwenye damu
 • Kusambaa kwa maambukizi kuingia kwenye misuli na tishu zinazozunguka jino
 • Kusambaa kwa maambukzi kwenda kwenye mifupa inayozunguka jino
 • Kusambaa kwa maambukizi kwenda kwenye maeneo mengine ya mwili na kusababisha jipu kwenye ubongo, nyumonia, au matatizo mengine

Kuzuia kupata jipu kwenye jino

Pata matibabu haraka sana kipindi tu unapoona una ugonjwa fizi ili kupunguza uwezekano wa jipu kwney jino kutokea. Ukiumia jino, linapaswa kuangalia/kuchunguzwa mapema na daktari wa meno/

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/imagepages/9979.htm

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi