1. Home
 2. JIPU KWENYE NJIA YA HAJA KUBWA
JIPU KWENYE NJIA YA HAJA KUBWA

JIPU KWENYE NJIA YA HAJA KUBWA

 • October 23, 2020
 • 0 pendwa
 • 22 Wameona
 • 0 Maoni

JIPU KWENYE NJIA YA HAJA KUBWA

Maelezo ya jumla

Jipu kwenye njia ya haja kubwa (anal abscess) ni mkusanyiko wa usaha katika eneo la mkundu (anus) na rektamu (rectum).

Je! Ni nini dalili za jipu la njia ya haja kubwa?

zifuatazo ni dalili za jipu kwenye njia ya haja kubwa

 • Kufunga choo (kunaweza kutokea)
 • Kutokwa na usaha kwenye rektamu
 • Homa
 • Uvimbe au kinundu,chekundu,kinachouma kwenye njia ya haja kubwa.
 • Maumivu wakati wa kwenda haja kubwa
 • Maumivu, tishu zilizokakamaa

Kwa watoto wachanga, jipu mara nyingi huonekana kama uvimbe, mwekundu, unaouma kwenye njia ya haja kubwa. Mtoto atakua anahangaika, lakini kwa ujumla hakuna dalili nyingine.

Nini husababisha jipu kwenye njia ya haja kubwa?

Sababu za kawaida ni pamoja na:

 • Kuziba kwa tezi maeneo hayo
 • Ufa kwenye njia ya haja kubwa unaopata maambukizi
 • Maambukizo ya magonjwa ya zinaa

Majipu yanayopatikana ndani sana ya rektamu yanaweza kusababishwa na matatizo ya utumbo kama Crohn’s disease au diverticulitis.

Nani yuko kwenye hatari zaidi?

Sababu zifuatazo zinaongeza hatari ya kupata jipu kwenye njia ya haja kubwa.

Hali hii inaweza kuwatokea watoto wachanga ambao bado wanatumia nepi na wenye historia ya kuwa na ufa kwenye njia ya haja kubwa.

Utambuzi

Uchunguzi wa rektamu utathibitisha kama una jipu kwenye njia ya haja kubwa. Protosigmoidoscopy inaweza kufanyika ili kuhakikisha kuwa hauna magonjwa mengine.

Wakati gani utafute matibabu ya haraka?

Mwone mtoa huduma wa afya kama unahisi una jipu kwenye rektamu. Unapaswa kumwona daktari pia kama unatokwa uchafu kwenye rektamu, unapata homa, baridi, au dalili nyingine mpya baada ya kutibiwa tatizo hili.

Uchaguzi wa matibabu

Tiba ya jipu ni kupasuaji na kulikamua.

Kukalia maji ya uvuguvugu yaliyowekwa kwenye chombo kunaweza kusaidia kupunguza maumivu na uvimbe, na kunaweza kusaidia kufanya jipu liwe rahisi kukamua.

Daktari anaweza kuagiza upewe dawa za maumivu na antibiotics.

Magonjwa yenye dalili zinazofanana

 • Nasuri/fistula kwenye njia ya haja kubwa

Kuzuia jipu kwenye njia ya haja kubwa

Kujikinga au kutibu mapema maambukizi ya magonjwa ya zinaa kunaweza kupunguza uwezekano wa kupata jipu kwenye njia ya haja kubwa. Tumia kondomu wakati wa kujamiiana, hii pia ni kwa watu wanaofanya mapenzi kinyume na maumbile, ili kuzuia maambukizi .

Kubadilisha nepi mara kwa mara na kumsafisha vizuri mtoto kutamkinga asipate ufa kwenye njia ya haja kubwa, hii itamkinga asipate majipu pia .

Nini cha kutarajia ?

Baada ya matibabu ya haraka mgonjwa hupona kabisa. Watoto wadogo mara nyingi hupona haraka sana.

Matatizo yanayoweza kutokea

 • Nasuri/fistula kwenye njia ya haja kubwa
 • Maambukizi ya mwili mzima
 • Jipu linaweza kujirudia tena
 • Makovu

Vyanzo

http://www.nlm.nih.gov/medlineplus/ency/article/001519.htm

 

 • Shirikisha:

Leave Your Comment