JIPU LA INI

JIPU LA INI

 • August 15, 2020
 • 0 Likes
 • 288 Views
 • 0 Comments

Maelezo ya jumla

Jipu la ini (liver abscess) ni eneo kwenye ini lililojaa usaha.

Je! Nini dalili za jipu la ini?    

 • Maumivu ya kifua ( hasa sehemu ya chini-kulia)    
 • Kinyesi chenye rangi ya udongo mfinyanzi
 • Mkojo wenye rangi nzito  
 • Homa, kuhisi baridi    
 • Kupoteza hamu ya kula    
 • Kichefuchefu, kutapika    
 • Kwa kawaida mgonjwa huwa na maumivu kwenye sehemu ya juu ya tumbo –kulia au kwa mara chache maumivu yanaweza kuena katika tumbo lote    
 • Kupungua kwa uzito bila sababu maalumu   
 • Uchovu   
 • Ngozi kubadilika kuwa rangi ya manjano (jaundice)

Ni nini husababisha jipu la ini?

Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha jipu kwenye ini, ni pamoja na:    

 • Maambukizi ya kwenye tumbo kama vile ugonjwa wa kidole tumbo/kibole (appendicitis) au kutoboka kwa utumbo
 • Maambukizi kwenye damu    
 • Maambukizi kwenye mirija inayotoa nyongo kwenye mfuko wa nyongo    
 • Kipimo cha endoscopy kilichofanyika hivi karibuni ili kuchunguza mirija inayotoa nyongo kwenye mfuko wa nyongo
 • Jeraha kwenye ini

Bakteria wanaosababisha majipu kwenye ini ni pamoja na:    

 • Bacteroides    
 • Enterococcus    
 • Escherichia coli    
 • Klebsiella pneumoniae    
 • Staphylococcus aureus    
 • Streptococcus

Mara nyingi, zaidi ya aina moja ya bakteria husababisha kutokea kwa jipu kwenye ini.

Utambuzi

Vipimo vinaweza kujumuisha:    

 • CT scan ya tumbo –hiki ni kipimo kinachotumia nguvu ya mionzi kupiga picha sehemu ya ndani ya tumbo, ili kumpa daktari nafasi ya kuchunguza bila kufanya upasuaji.
 • Ultrasound ya tumbo –hiki ni kipimo kinachotumia mawimbi ya sauti kupiga picha sehemu ya ndani ya tumbo.   
 • Kipimo cha bilirubin kwenye damu – kipimo hiki huonesha kama ini linafanya kazi yake vyema ya kuondoa bilirubin mwilini.
 • Blood culture – damu ya mgonjwa hupandwa katika mazingira yatakayoruhusu bakteria walio kwenye damu kukua ili watambuliwe kwa urahisi.
 • Complete blood count (CBC) – kipimo hiki huhesabu seli zote kwenye damu, aina fulani za seli huongezeka kama kuna maambukizi mwilini
 • Liver biopsy– Utaratibu mdogo hufanyika ili kuchukua sampuli ya nyama kidogo kwenye ini ili kupima
 • Liver function tests– kipimo hiki hufanyika ili kugundua kama ini linafanya kazi yake vyema (vipimo vya kazi ya ini)

Wakati gani utafute matibabu ya haraka?

Mwone mtoa huduma wa afya ikiwa una:    

Uchaguzi wa matibabu

Matibabu ya kawaida hujumuisha kuweka tube kupitia kwenye ngozi ili kunyonya usaha kutoka kwenye jipu. Kwa mara chache sana upasuaji huhitajika. Utapewa viuavijasumu (antibiotics) pia kwa wiki 4 hadi 6. Wakati mwingine, antibiotics peke yake zinaweza kutibu kama maambukizi ni kidogo.

Kuzuia

Matibabu ya haraka ya maambukizi ya tumbo na maambukizi mengine yanaweza kupunguza hatari ya kutokea kwa jipu la ini. Matukio mengi hayawezi kuzuilika.

Nini cha kutarajia?

Hali hii inaweza kuwa hatari kwa maisha ya wagonjwa wengine. Hatari ya kupoteza maisha ni kubwa zaidi kwa watu ambao wana majipu mengi kwenye ini.

Matatizo yanayoweza kujitokeza

Maambukizi yanaweza kusambaa mwili mzima na kutishia maisha 

Vyanzo    

http://www.nlm.nih.gov/medlineplus/ency/article/000261.htm

Leave Your Comment