JIPU

JIPU

 • August 19, 2020
 • 0 Likes
 • 583 Views
 • 0 Comments

Maelezo ya jumla

Jipu (abscess) ni mkusanyiko wa usaha katika sehemu yoyote ya mwili, ambayo mara nyingi huisababisha ivimbe .

Je! Ni nini dalili za jipu?

Dalili za jipu hutegemea hasa mahali lilipo. Dalili za kawaida ni kama zifuatazo:

 • Maumivu kwenye eneo lenye jipu
 • Kuhisi baridi
 • Homa
 • Kupungua kwa uwezo wa kufanya kazi katika eneo lililoathirika
 • Kujisikia vibaya, wasiwasi, au hisia mbaya
 • Kichwa kuuma
 • Kuvimba katika eneo lenye jipu, tishu za eneo hilo hukakamaa
 • Kupoteza hamu ya kula
 • Kupoteza hisia katika eneo lililoathirika
 • Kichefuchefu na kutapika
 • Kuvimba

Jipu husababishwa na nini?

Majipu hutokea wakati tishu za eneo la fulani la mwili zinapopata maambukizi na mfumo wa kinga ya mwili ukijaribu kupigana nayo. Seli nyeupe za damu hutambaa katika kuta za mishipa ya damu mpaka katika eneo la maambukizi na kujikusanya ndani ya tishu zilizoharibiwa. Wakati wa mchakato huu, usaha hutengenezeka. Usaha ni mkusanyiko wa ugiligili (fluid), seli nyeupe za damu zilizo hai na zilizo kufa, tishu zilizokufa na bakteria au vitu vingine vigeni. Majipu yanaweza kutokea mahali popote mwilini. Kweye ngozi,ndani ya ngozi na kwenye meno ndio maeneo yanayoathirika kwa zaidi. Majipu yanaweza kusababishwa na bakteria,kimelea na kitu kigeni ndani ya mwili. Majipu ya kwenye ngozi ni rahisi kuonekana. Ni mekundu, yanavimba na yanauma. Majipu katika maeneo mengine ya mwili inaweza isiwe rahisi kuyaona, lakini yanaweza kusababisha uharibifu mkubwa. Zifuatazo ni aina maalumu za majipu:

 • Jipu la tumbo (Abdominal abscess)
 • Jipu la ini linalosababishwa na Amoeba
 • Jipu la njia ya haja kubwa (Anorectal abscess)
 • Jipu la ubongo (Brain abscess)
 •  Jipu la tezi ya bartholin (Bartholin’s abscess)
 • Jipu la tukwa (Peritonsillar abscess)
 • Jipu la ngozi (Skin abscess)
 • Jipu la uti wa mgongo (Spinal cord abscess)
 • Jipu la jino (Tooth abscess)

Nani yuko kwenye hatari zaidi?

Watu walio na historia ya maambukizi ya hivi karibuni, wako kwenye hatari kubwa ya kupata jipu.

Wakati gani utafutae matibabu ya haraka?

Mwone mtoa huduma ya afya ikiwa unafikiri una aina yoyote ya jipu.

Utambuzi

Mara nyingi, sampuli ya maji maji itachukuliwa kutoka kwenye jipu na kupimwa ili kuona ni  aina gani ya kimelea imesababisha tatizo.

Uchaguzi wa matibabu

Matibabu yanatofautiana, lakini mara nyingi upasuaji, antibiotics, au yote yanahitajika.

Nini cha kutarajia ?

Matarajio hutegemea eneo la maambukizi, aina ya vimelea vinavyosababisha jipu na hali ya kiafya ya mgonjwa (umri, hali ya kingamwili na kama ana ugonjwa wowote wa kudumu). Lakini mara nyingi majipu hupona baada ya upasuaji mdogo na kozi ya antibiotics

Matatizo yanayoweza kutokea

Jipu linaweza kupasuka na kuenea mwili mzima kupitia damu (septicemia), hii inaweza kuwa hatari

Vyanzo

http://www.nlm.nih.gov/medlineplus/article/001353.htm

 

 • Share:

Leave Your Comment