JIWE / MAWE KWENYE FIGO :Dalili,sababu,matibabu

Jiwe/mawe kwenye figo ni nini?

Jiwe/mawe kwenye figo ni vijiwe vidogo vinavyotengenezwa na mwili kwa kuunganisha mabaki ya taka mwili kwenye mkojo. Kama vijiwe hivi vikiwa vikubwa sana, vinaweza kuziba njia ya mkojo na hata kibofu. Na hii inaweza kusababisha maumivu makubwa.

Nani anapata jiwe/mawe kwenye figo?

Jiwe/mawe huwapata zaidi wanaume, lakini wanawake wanaweza kuyapata pia. Watu wengi wanaopata jiwe/mawe kwenye figo huwa kati ya miaka 30 na 50 kiumri. Jiwe/mawe kwenye figo yanasababishwa na kutokunywa maji ya kutosha na kula nyama kwa wingi au vyakula vyenye chumvi nyingi. Uko kwenye hatari zaidi ya kupata jiwe/mawe kwenye figo kama kuna mwanafamilia napata shida hii. Jiwe/mawe kwenye figo yanaweza pia kusababishwa na maambukizi kwenye njia ya mkojo.Mawe kwenye figo

Nitajuaje kama nina jiwe/mawe kwenye figo?

Jiwe/mawe kwenye figo kwa kawaida yanasababisha maumivu makali kwenye upande yaliyopo. Maumivu yatakuwa yanasogea kutoka juu kwenda chini kwenye kinena. Utajisikia kuumwa sana na unaweza kupata mkojo uliochanganyikana na damu. Unaweza pia kuwa na homa. Daktari anaweza kuagiza kupiga picha za eksirei au kufanya vipimo vya mkojo ili kutambua kama una jiwe/mawe kwenye figo.

Tatizo la jiwe/mawe kweny kibofu hutibiwa vipi?

Unaweza kukojoa jiwe/mawe yaliyokuwa kwenye kibofu kama ni madogo. Daktari anaweza kukupatia dawa ili kukupunguzia maumivu. Kama jiwe ni kubwa sana, daktari anaweza kutumia mashine maalumu ili kulivunjavunja katika vipande vidogo ili litoke. Daktari anaweza pia kupitisha kamera ndogo kupitia kwenye mrija wa urethra (njia ya mkojo) ili kulitafuta jiwe lilipo. Baada ya hapo atalitoa au kulivunjavunja kuwa vipande vidogo. Kama daktari ataamua kufanya utaratibu huu, atakupatia dawa ya kupunguza maumivu ili usiumie. Kwa visa vingine, upasuaji ndiyo tiba pekee inayoweza kuondoa mawe kwenye figo.jiwe kwenye figo

Nifanyeje kuzuia kupata jiwe/mawe kwenye figo tena?

Watu wengi wenye jiwe/mawe kwenye figo wana uwezekano wa 50% wa kupata tena jiwe jingine ndani ya miaka 10. Lakini kuna mambo unayoweza kufanya ili kupunguza hatari hii:

  • Kunywa maji ya kutosha ili kutengeneza angalau lita 2 za mkojo kwa siku
  • Usile zaidi ya 1500mg za chumvi kwa siku ( sawa na kijiko 1 cha chai). Hii inajumuisha pia chumvi inayokuwa kwenye vyakula vya makopo 9viwandani). Angalia vibandiko (lables), ili kuona kuna chumvi kiasi gani kwenye chakula chako.
  • Usile nyama nyingi kwa siku moja. Usile zaidi ya 170 -270g (sawa na ukubwa wa fungu za kadi za kuchezea (karata) 2 – 2 decks
  • Kula chakula chenye kiwango cha kadri cha kalsiamu, kama vile maziwa, jibini (cheese), na vyakula vingine vilivyotengenza kwa maziwa. Kama mawe ya kwenye figo yametokana na kalsiamu, hauhitaji kuacha kula vyakula vya maziwa. Kula kwa kadri inatosha.

Kama umepata mawe zaidi ya mara moja, daktari anaweza kukupatia rufaa uonane na mtaalamu wa figo ili atambue sababu mahususi inayosababisha upate mawe hayo. Baadhi ya watu wanahitaji kutumia dawa ili kuzuia / kuwakinga kupata jiwe/mawe kwenye figo.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/000458.htm

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi