Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko
Maelezo ya jumla
Saratani au kansa ni ukuaji wa seli sizizo za kawaida mwilini usio na udhibiti.
Dalili za saratani
Dalili za kansa hutegemea ni aina gani ya kansa na eneo la mwili ilipotokea. Kwa mfano, saratani ya mapafu inaweza kusababisha kukohoa, kupata shida kupumua, au maumivu ya kifua. Kansa ya utumbo mara nyingi husababisha kuhara, kuvimbiwa, na damu katika kinyesi. Baadhi ya kansa hazina dalili yoyote. Kansa ya kongosho, dalili hazianzi mpaka ugonjwa umefikia hatua ya juu sana. Dalili zifuatazo zinaweza kutokea kwa kansa nyingi:
- Kuhisi baridi
- Uchovu
- Homa
- Kupoteza hamu ya kula
- Unyonge
- kutokwa jasho usiku
- Kupungua kwa uzito
Kansa husababishwa na nini?
Seli za saratani hutokana na seli za kawaida za mwili. Seli za kawaida za mwili huongezeka mwili unapozihitaji na kufa mwili unapokua hauzihitaji tena. Mfumo huu wa kudhibiti ukuaji wa seli mwilini unapokua umeshindwa kufanya kazi vizuri, husababisha seli kukua na kuongezeka haraka sana kuliko kawaida . Kuna aina nyingi za saratani na zinaweza kutokea katika ogani kama vile mapafu, utumbo, matiti, ngozi, mifupa, au tishu za neva.
Kuna sababu nyingi zakutokea saratani, ikiwa ni pamoja na:
- Benzene na kemikali nyingine
- Unywaji wa pombe uliopitiliza
- Sumu zitokanazo na mazingira, kama vile uyoga wenye sumu na aina ya sumu ambayo inaweza kukua kwenye mimea ya karanga (aflatoxins)
- Kukaa sana kwenye jua kali
- Matatizo ya kimaumbile)
- Uzito uliopitiliza/kitambi
- Mionzi
- Virusi
Hata hivyo, sababu ya kutokea kwa kansa nyingi bado haijulikani.
Sababu ya vifo vingi zaidi vinavyohusiana na kansa ni kansa ya mapafu. Saratani tatu zinazowapata wanaume wengi nchini marekani ni:
Kansa tatu zinazowapata zaidi wanawake nchini marekani ni:
Baadhi ya kansa zinajitokeza zaidi katika sehemu fulani fulani za dunia. Kwa mfano, huko Japan, kuna matukio mengi ya saratani ya tumbo, lakini nchini Marekani, aina hii ya saratani siyo ya kawaida. Tofauti ya mlo au mazingira vinaweza kuleta tofauti hii.
Aina nyingine za kansa ni pamoja na:
- Saratani ya
- Ubongo
- Kizazi
- Figo
- Damu
- Ini
- Ovari
- Ngozi
- Korodani/pumbu
- Kikoromeo
- Mji wa mimba
Utambuzi wa saratani
Kama ilivyo kwa dalili, ishara za kansa zinatofautiana kulingana na aina na eneo ilipotokea. Vipimo vya kawaida vinavyofanyika ni pamoja na:
- Kukata nyama ndogo kutoka katika eneo lenye saratani kwa ajili ya kupima.
- Vipimo vya damu (vinafanyika kuaangalia kemikali zinazoashiria kuwepo kwa aina fulani ya kansa katika damu-alama za kansa)
- Kupima uboho wa mifupa (kwa saratani ya damu)
- Picha ya mionzi (X-ray) ya kifua
- Picha ya damu
- CT scan
- Vipimo vya kazi ya ini (LFT)
- MRI scan
Kansa nyingi hugunduliwa kwa kuchukua nyama ndogo na kuipima . Kuchukua nyama ndogo kwa ajili ya kuipima inaweza kuwa kwa upasuaji mdogo na rahisi au operesheni kubwa. Wagonjwa wengi wenye kansa hufanya CT scan kujaribu kutambua eneo halisi na ukubwa wa saratani.
Utambuzi kuwa una saratani ni vigumu kukabiliana nao. Lakini ni muhimu, kujadiliana na daktari kuhusu aina, ukubwa, na mahali ilipo saratani. Pia utahitaji kuuliza kuhusu uchaguzi wa matibabu, pamoja na faida na hatari zake. Ni wazo zuri kuwa na mtu mwingine unaemwamini kwenye ofisi ya daktari unapokwenda kupokea majibu ya uchunguzi wa saratani ili kukusaidia . Ikiwa utapata shida kuuliza maswali baada ya kusikia kuhusu utambuzi/ugunduzi wa kuwa una saratani, mtu uliyeenda nae kwa daktari atasaidia kuuliza maswali hayo.
Ni wakati gani utafute matibabu ya haraka?
Wasiliana na mtoa huduma wa afya ikiwa unahisi una dalili za saratani.
Uchaguzi wa matibabu
Matibabu yanatofautiana kulingana na aina ya kansa na hatua yake. Hatua inaelezea kiasi gani saratani hiyo imeongezeka na kama imeenea kutoka mahali pake pa awali kwenda sehemu zingine za mwili.
- Ikiwa kansa iko kwenye eneo moja na haijaenea, mbinu ya matibabu ya kawaida ni upasuaji ili kutibu na kuponya kabisa. Hii mara nyingi huonekana kwenye kesi ya kansa ya ngozi, pamoja na kansa ya mapafu, kifua, na utumbo.
- Ikiwa saratani imeenea mpaka kwenye tezi za limfu za eneo hilo hilo, wakati mwingine hizi pia zinaweza kuondolewa.
- Ikiwa upasuaji hauwezi kuondoa kansa yote, chaguzi za matibabu ni pamoja na mionzi, Tibakemikali, au zote mbili. Baadhi ya kansa zinahitaji mchanganyiko wa upasuaji, mionzi, na Tibakemikali.
- Mara nyingi Lymhoma hutibiwa kwa tibakemikali na tiba ya mionzi na mara chache hutibiwa kwa upasuaji.
- Ingawa matibabu yanaweza kuwa magumu, kuna njia nyingi za kukutia moyo.
Ikiwa una matibabu ya mionzi, jua kwamba:
- Tiba ya mionzi haisababishi maumivu yoyote.
- Matibabu hupangwa kila wiki.
- Unapaswa kutenga dakika 30 kwa kila kikao cha matibabu, ingawa matibabu yenyewe huchukua dakika chache tu.
- Unapaswa kupata muda wa  kupumzika na kula chakula vizuri wakati wa tiba ya mionzi.
- Ngozi katika eneo unalopigwa mianzo linaweza kuwa na wepesi wa kuhisi na hii inaweza kukera.
- Â Madhara ya matibabu ya mionzi ni ya muda mfupi na hutofautiana kutegemea na eneo la mwili linalopigwa mionzi.
Ikiwa unatibiwa kwa tibakemikali (chemotherapy), unapaswa kula chakula vizuri. Tibakemikali husababisha mfumo wako wa kinga kudhoofika, hivyo unapaswa kuepuka kukaa karibu na watu wenye mafua. Unapaswa pia kupata wakati wa kutosha wa kupumzika, na usijisikie kuwa unapaswa kukamilisha kazi zako zote kwa mara moja.
Itakusaidia ukizungumza na familia au marafiki kuhusu hisia zako. Jitahidi kufuata masharti na maelekezo ya watoa huduma wa afya wakati wote matibabu . Ni vizuri kujitunza na kufanya mambo madogo madogo mwenyewe .Hii itakufanya ujihisi mwenye udhibiti wa hatma ya maisha yako.
Unawezaje kuzuia/kinga dhidi ya saratani?
Unaweza kupunguza hatari ya kupata kansa kwa:
- Kula chakula cha afya
- Kufanya mazoezi mara kwa mara
- Kupunguza pombe
- Kupunguza uzito
- Kuepuka kukutana na mionzi
- Kuepuka kutumia/kukutana na dawa za sumu/kemikali kali.
- Acha kabisa kuvuta sigara au kutafuna tumbaku.
- Punguza kukaa sana juani, hasa ikiwa jua linakuunguza kirahisi.
- Fanya uchunguzi wa kansa, kama vile mammografia kwa uchunguzi wa kansa ya matiti na picha ya Colonoscopy kwa kansa ya utumbo. Kufanya uchunguzi husaidia kugundua kansa katika hatua ya mwanzo, wakati ambao zaweza kutibiwa kwa urahisi.
Nitarajie nini?
Matarajio hutegemea aina na hatua ya saratani wakati inapogunduliwa.
Saratani nyingine zinaweza kuponywa,nyingine haziwezi kuponywa kabisa ila zinaweza kutibiwa kwa ufanisi mkubwa. Wagonjwa wengine wanaweza kuishi kwa miaka mingi na saratani,lakini aina nyingine za saratani huhatarisha maisha na kifo hutokea baada ya muda mfupi. .
Matatizo yatokanayo na saratani
Matatizo yanayosababishwa na kansa hutegemea aina na hatua ya saratani. Saratani inaweza kuenea kwenda sehemu nyingi za mwili na kuleta madhara makubwa .
Leave feedback about this