Kansa ya damu ni nini?
Kansa ya damu ni kansa inayotokea kwenye seli za damu na uboho wa mifupa. Watu wa umri wowote wanaweza kupata kansa ya damu, na sababu ya kutokea kwake hazijulikani vizuri. Unaweza kuwa katika hatari kubwa zaidi ya kupata kansa kama umekutana na mionzi au kemikali na madawa ya kuulia wadudu. Kama umewahi kuwa na kansa yoyote ya damu au uboho wa mifupa, uko kwenye hatari zaidi ya kuipata tena.
Kuna aina ngapi za kansa ya damu?
Kansa ya damu inayowapata zaidi Watoto inaitwa Acute lymphoblastic leukemia. Watu wenye aina hii ya kansa wanapatwa na homa, uchovu, kuvuja damu, damu kuvia chini ya ngozi, maumivu ya mifupa na kuvimba kwa ini na bandama.
Aina ya kansa ya damu inayowapata zaidi watu wazima inaitwa Acute myelogenous leukemia. Hii inasababisha homa, uchovu, upungufu wa uzito wa mwili, kuvuja damu na kuvia kwa damu chini ya ngozi.
Kuna aina nyingine mbili, Chronic lymphocytic na chronic myelogenous leukemia, zinazowatokea zaidi watu wazima. Wengi wa watu wenye aina hizi za kansa hawana dalili zozote, lakini wanaweza kuwa na ini, bandama au tezi za mwili zilizovimba.
Kansa ya damu inatambuliwaje na matibabu?
Kansa ya damu inatambuliwa kwa kufanya vipimo vya damu na uboho wa mifupa. Matibabu yanategemea umri wa mtu mwenye kansa, hali ya afya yake na aina ya kansa aliyonayo. Matibabu yanajumuisha tibakemikali, tiba ya mionzi, kupandikizwa uboho mwingine kwenye mifupa kutoka kwa mfadhili, au kutumia madawa ya kuua seli za kansa.
Watu wenye chronic lymphocytic leukemia wanaweza kuangaliwa kwanza bila kupewa matibabu kama hawana dalili zozote na kama kiwango cha seli za damu ziko sawa.
Leave feedback about this