KASWENDE: Sababu, dalili, matibabu, kuzuia

Kaswende ni nini?

Kaswende ni ugonjwa wa ngono unaosababishwa na bakteria anyeitwa Treponema pallidum. Kama ugonjwa wa kaswende hautatibiwa unaweza kusababisha matatizo makubwa. Habari njema ni kwamba, kaswende inaweza kutibiwa vyema na penicillin au aina nyingine za antibiotiki.kaswende

Ni zipi hatua na dalili za kaswende?

Kaswende ina hatua nne inazopitia, kutegemea ni kwa muda mtu amaekuwa na huu ugonjwa. Kila hatua inaweza kuwa na dalili tofauti.

kaswende

Hatua ya mwanzo ya ugonjwa – kama umeambukizwa hivi karibuni, unaweza kuwa na kidonda kigumu kwenye mlango wa uke au uume. Kidonda hiki kinaitwa chacre. Kwa kawaida kuna kidonda kimoja kisicho na maumivu, lakini kunaweza kuwepo na vingi.

Kama usipotibu hatua ya mwanzo ya ugonjwa wa kaswende, inaingia katika hatua ya pili. Unaweza kuwa na dalili kama za mafua na upele mwili mzima. Unaweza kuwa na vijinyama vinavyoota kwenye Ngozi vinavyoitwa condyloma latuma. Mara nyingi vijinyama hivi huota karibu na uke au uume au karibu na mkundu. Unaweza pia kuwa na matatizo kwenye figo, ini, na viungo vingine

Hatua inayofuata ni hatua ya tatu ya ugonjwa. Katika hatua hii hakuna dalili zozote za ugonjwa, lakini ukipima vipimo vya damu vinaonesha kuwa bado una maambukizi ya kaswende.

Hatua inayofuata ndiyo hatua ya mwisho ya ugonjwa. Ni hatua inayoonesha kuwa ugonjwa umekuwepo kwa miaka mingi sana. Kama umefikia hatu ya mwisho unaweza kuwa na vidonda vikubwa visivyopona. Vidonda hivi vikubwa vinaweza kuwa kwenye Ngozi au ndani ya mwili.

Unaweza pia kuwa na matatizo kwenye mishipa ya moyo na mishipa yad amu. Moja ya tatizo kubwa zaidi linaloweza kutokea ni ugonjwa wa kaswende kufika na kuharibu ubongo na mfumo wa fahamu. Ugonjwa huu unaweza kusababisha ukashindwa kusikia, kuona, kufikiri, na hata kifo.

Ugonjwa wa huu unatambuliwaje?

Kama una vidonda kwenye ngozi, daktari atakwangua gamba kutoka kwenye kidonda ili kuangalia chini ya darubini

Mara nyingi, madaktari wanategemea zaidi vipimo. Vpimo kadhaa vinaweza kuhitajika ili kuwa na uhakika kuwa una kaswende

Mji maji ya uti wa mgongo yanaweza kuchukuliwa kwa sindano ili kuyapima (spinal tap) kama kuna wasiwasi kuwa kaswende imefikia mfumo wa fahamu.

Kaswende inatibiwaje?

Ugonjwa wa kaswende unawea kutibiwa kwa sindano ya penicillin. Kama una mzio na penicillin, daktari anaweza kukupatia aina nyingine ya antibiotiki.

Jambo jingine la msingi la kukumbuka kama una kaswende?

Kwa sababu kaswende ni ugonjwa unaoenezwa kwa ngono, ni muhimu kuwa mwenzi wako akapimwe na kutibiwa pia. Ni vizuri pia kuongea na dakatari ili akupime na magonjwa mengine ya zinaa. Ongea na daktari ili utambue ni lini unaweza kuanza kushiriki ngono tena kwa usalama baada ya matibabu.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/000861.htm

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi