KIBWIKO

KIBWIKO

 • December 20, 2020
 • 0 Likes
 • 40 Views
 • 0 Comments

Maelezo ya jumla

Mtoto mwenye kibwiko (clubfoot) huzaliwa na miguu au mguu wenye wayo uliogeukia ndani au nje. Hali hii huwepo wakati mtoto anapozaliwa.

Ni nini dalili za kibwiko?

Mwonekano wa mguu hutofautiana. Mguu mmoja au yote inaweza kuathirika.

Wayo wa mguu hugeukia ndani au nje anapozaliwa, na inaweza kuwa ngumu kuinyoosha ili ikae vizuri.

Ni nini husababisha kibwiko?

Kibwiko ndio tatizo la miguu linaloathiri watoto wengi zaidi wakati wa kuzaliwa. Tatizo linaweza lisiwe kubwa na miguu isikaze au linaweza kuwa kubwa na miguu iliyokakamaa.

Sababu haijulikani, lakini hali hii inaweza kurithiwa ndani ya familia kwa hali fulani. Watoto wanaozaliwa kwenye familia yenye historia ya kuwa na kibwiko na watoto wa kiume wako kwenye hatari zaidi. Hali hii humpata mtoto 1 kati ya 1000 wanaozaliwa.

Utambuzi

Hali hii inatambuliwa kwa kufanya uchunguzi wa mwili pekee. Eksirei ya mguu inaweza kufanywa.

Wakati gani utafute huduma ya matibabu kwa haraka?

Kama mwanao anapata tiba ili kurekebisha kibwiko, mwone mtoa huduma ya afya kama:

 • Vidole vya miguu vimevimba au vimebadilika rangi baada ya kuwekewa hogo (cast)
 • Kama hogo alilowekewa mtoto linasababisha maumivun makali
 • Kama vidole vimepotelea kwenye hogo/hogo limeteleza na kufunika vidole
 • Kama hogo limeteleza na kuchomoka
 • Kama wayo wa mguu umeanza kugeukia ndani tena baada ya matibabu.

Uchaguzi wa matibabu

 • Mtoto anaweza kunyooshwa miguu ili kuiweka sawa na kisha kuishikiza kwa hogo ili usipinde tena. Mara nyingi shughuli hii hufanywa na daktari wa mifupa.

  Matibabu yanapaswa kuanza mapema iwezekanavyo—hasa baada tu ya kuzaliwa—wakati huu ndio rahisi kunyoosha miguu.

 • Kuivuta na kuionyoosha miguu polepole na kisha kuiwekea hogo hufanyika kila wiki ili kuiweka miguu sawa. Kwa kawaida, mtoto anaweza kuwekewa hogo mara tano mpaka kumi hivi. Hogo la mwisho linaweza kukaa hapo kwa wiki 3. Baada ya mguu kukaa sawa, mtoto atapaswa kuvaa viatu maalum vyenye vishikiza (braces) kwa angalau miezi mitatu usiku na mchana. Kisha, ataendelea kuvivaa usiku pekee na wakati analala kwa angalau miaka 3.
 • Mara nyingi, shida huwa kwenye kano (tendon) za kisigino na utaratibu hufanyika ili kuzilegeza
 • Kama tatizo ni kubwa sana, kesi nyingine za kibwiko huhitaji upasuaji ili kurekebika kama matibabu mengine yameshindwa au kama tatizo linajirudia. Mtoto anapaswa kufuatiliwa kwa ukaribu na mtaalamu wa huduma za afya mpaka atakapokuwa mtu mzima.

Nani yuko kwenye hatari zaidi?

 • Watoto wa kiume wako kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata kibwiko

Nini cha kutarajia?

 • Matokeo huwa mazuri baada ya matibabu.

Matatizo yanayoweza kutokea

Kasoro zingine zinaweza zisiweze kurekebika kabisa. Lakini, matibabu yanaweza kuboresha mwonekano na uwezo wa miguu kufanya kazi. Matibabu yanaweza yasifanikiwe sana kama kibwiko kimetokea sambamba na tatizo jingine la miguu.

 • Share:

Leave Your Comment