KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA

KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA

 • December 20, 2020
 • 0 Likes
 • 34 Views
 • 0 Comments

Maelezo ya jumla

Kichefuchefu (nausea) ni hisia ya kuwa na hamu ya kutapika. Kutapika ni hali ya kutupa yaliyomo tumboni kupitia kinywani.

Nini husababisha kichefuchefu na kutapika?

Matatizo mengi ya kawaida yanaweza kusababisha kichefuchefu na kutapika:

 • Mzio wa chakula
 • Maambukizi ya tumbo au utumbo, kama vile homa ya matumbo au sumu kwenye chakula
 • Madawa au matibabu, kama vile tiba ya kansa au matibabu ya mionzi
 • Kipandauso
 • Kichwa kuuma wakati wa ujauzito
 • Ukimwi au ugonjwa wa mwendo
 • Maumivu makali, kama vile yanayotokana na mawe kwenye figo

Kichefuchefu na kutapika kunaweza kuwa ishara ya mapema ya matatizo makubwa zaidi, kama vile:

Utambuzi

Mtoa huduma ya afya atakuchunguza mwili na kuangalia kama una ishara za kuishiwa maji mwilini.

Mtoa hudumam ya afya atakuuliza maswali kuhusu dalili zako, kama vile:

 • Kutapika kulianza lini? Kumekuwepo kwa muda gani? Umetapika mara ngapi?
 • Je! Hutokea baada tu ya kula, au ukiwa na njaa?
 • Je, kuna dalili zozote nyingine – maumivu ya tumbo, homa, kuhara, au maumivu ya kichwa?
 • Je! Unatapika damu?
 • Je! Unatapika chochote ambacho kinaonekana kama kahawa?
 • Je! Unatapika chakula ambacho hakijamen’genywa?
 • Je, mara ya mwisho ulikojoa lini?

Maswali mengine ambayo unaweza kuulizwa ni pamoja na:

 • Umekuwa ukipungua uzito?
 • Je, Ulikuwa safarini? Wapi?
 • Je, Unatumia dawa gani?
 • Je, Watu wengine waliokula mahali ulipokula wana dalili sawa kama zako?
 • Je! Una ujauzito au unaweza kuwa na ujauzito?

Vipimo vya uchunguzi vinaweza kufanywa, ikiwa ni pamoja na:

 • Vipimo vya damu (kama vile picha ya damu, vipimo vya kuangalia kazi ya ini n.k)
 • Kipimo cha mkojo
 • Eksirei ya tumbo
 • Kulingana na sababu na kiasi cha maji kilicho mwilini mwako, unaweza kulazwa hospitalini kwa muda. Unaweza kuhitaji kuongezewa maji.

Wakati gani utafute matibabu ya haraka?

Mwone daktari au fika  kwenye chumba cha dharura kama:

 • Unafikiri kutapika kumetokana na kula, kunywa au kuvuta sumu.
 • Unaona damu au rangi kama ya kahawa kwenye matapishi.

Fika kitua cha huduama za dharura kwa ajili ya matibabu kama wewe au mtu mwingine:

 • Amekuwa akitapika kwa masaa 24 au zaidi
 • Kama ameshindwa kunywa chochote bila kwa masaa 12 au zaidi.
 • Kama unapata maumivu ya kichwa au shingo kukakamaa.
 • Kama una maumivu makali ya tumbo
 • Kama haujakojoa kwa masaa 8 au zaidi
 • Kma umetapikamara 3 au zaidi kwa siku moja

Ishara za kuishiwa na maji mwilini ni pamoja na:

 • Kulia bila kutokwa na machozi.
 • Midomo kuwa mikavu
 • Kuongezeka kwa kiu.
 • Macho yanayoonekana kama yamedumbukia ndani
 • Mabadiliko ya ngozi – kwa mfano, kama ukiigusa haijirudi kama kawaida
 • Kukojoa mkojo wa njano au kukojoa mara chache zaidi.

Uchaguzi wa matibabu

Katika kipindi chote cha kichefuchefu na kutapika, ni muhimu kuendelea kunywa maji. Jaribu kunywa mara kwa mara, kiasi kidogo kidogo cha maji. Mara baada ya daktari kutambua sababu ya kichefuchefu na kutapika kwako, atakupatia dawa au kuagiza ubadilishe mlo.

Kama kichefuchefu na kutapika kunatokana na  ujauzito, muulize daktari kuhusu matibabu.

Kama kutapika kumetokana na mwendo/safari, matibabu yafuatayo yanaweza kusaidia:

 • Lala chini
 • Madawa – antihistamines (kama vile dramamine)
 • Scopolamine (patch za kubandika kwenye ngozi) hizi ni muhimu kwa safari ndefu, kama vile safari za baharini. Weka patch kwenye ngozi yako masaa 4 – 12 kabla ya kuanza safari. Scopolamine dawa yenye ufanisi mkubwa lakini inaweza kusababisha midomo kuwa mikavu, kutokuona vizuri na kusinzia sinzia. Scopolamine ni kwa watu wazima tu. Haipaswi kutumiwa na watoto.

Vyanzo

http://www.nlm.nih.gov/medlineplus/ency/article/003117.htm

 • Share:

Leave Your Comment