Magonjwa ya ndani ya mwili

KICHWA KUUMA:Sababu,matibabu,kuzuia

Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko

Maelezo ya jumla

Kichwa kuuma ni neno linalotumika kuelezea maumivu ya kichwa au sehemu ya juu ya shingo. Kichwa ni eneo linalopata maumivu ya mara kwa mara. Maumivu ya kichwa yana sababu nyingi,nyingine ni za kawaida lakini nyingine ni hatari kama vile uvimbe kwenye ubongo, maambukizi kwenye ubongo, wasiwasi, yabisi kavu ya shingo au mgongo, sonona, baadhi ya madawa, pombe na mabadiliko ya kimazingira.

Je, nini dalili za kichwa kuuma?

Kuna aina mbili za maumivu ya kichwa: maumivu ya kichwa yenye chanzo kinachojulikana na maumivu ya kichwa yasiyo na chanzo kinachojulikana. Maumivu ya kichwa yasiyo na chanzo maalumu kinachojulikana ni pamoja na kipandauso, maumivu mkazo ya kichwa na maumivu ya vipindi. Maumivu ya kichwa yenye chanzo kinachojulikana hutokana na matatizo au shida fulani kwenye kichwa au shingo, mfano: uvimbe kwenye ubongo, kiharusi au maambukizi kwenye ubongo. Maumivu ya kichwa yenye chanzo kinachojulikana huambatana na dalili nyingine.

 • Dalili za maumivu ya kichwa yasio na chanzo maalumu:
  • Baadhi ya maumivu ya kichwa huanza baada ya mabadiliko ya kihisia, kula aina fulani za chakula, au mabadiliko ya kimazingira.
  • Maumivu na kukaza kwa misuli ya sehemu ya nyuma ya kichwa na shingo.
  • Maumivu huwa si makali sana
  • Huwa hayaambatani na kichefuchefu au kutapika
  • Wakati mwingine maumivu hutokea kwa vipindi
 • Maumivu ya kichwa yanayosababishwa na tatizo maalumu, huwa na dalili za nyongeza :

Nani yuko kwenye hatari zaidi ya maumivu ya kichwa?

Watu wenye matatizo yafuatayo wako kwenye hatari zaidi ya kuumwa kichwa

Nini husababisha maumivu ya kichwa?

Kuumwa kichwa ni dalili, jambo muhimu zaidi ni kutambua sababu ya kichwa kuuma.

 • Historia na sifa za maumivu ya kichwa husaidia kutambua sababu.
 • Daktari hufanya uchunguzi wa mwili na tathmini ya mfumo wa neva.
 • Uchunguzi wa macho hufanyika ili kutambua kama kuna tatizo kwenye ubongo.
 • Vipimo vya damu kuchunguza figo, ini n.k husaidia kutambua matatizo mengine.
 • Vipimo vya picha kama CT Scan na MRI Scan hutumiwa na madaktari kutambua matatizo ya kimuundo kwenye ubongo.
 • Electroencephalography (EEG): Kipimo hiki huonesha shughuli ya umeme kwenye ubongo na kusaidia utambuzi wa matatizo ya ubongo.

maumivu ya kichwaWakati gani utafute matibabu ya haraka baada ya kichwa kuuma?

Maumivu ya  kichwa ni dalili tu. Ni muhimu kutambua sababu ya kichwa kuuma. Ukiona dalili zifuatazo,fika kwenye kituo cha afya kilicho karibu nawe haraka iwezekanavyo.

 • Maumivu makali ya kichwa ya ghafla
 • Maumivu ya kichwa yanayoambatana na kukaza au kukakamaa kwa shingo.
 • Maumivu ya kichwa yanayoamabatana na kichefuchefu au kutapika
 • Maumivu ya kichwa yanayoambatana na homa, degedege, kuchanganyikiwa au kupoteza fahamu.
 • Maumivu ya kichwa yanayoambatana na maumivu ya jicho au sikio.
 • Maumivu ya kichwa baada ya kupata jeraha kichwani
 • Maumivu ya kudumu ya kichwa kwa mtu ambaye hapo mwanzo hakuwa na tatizo la kuumwa kichwa
 • Maumivu ya mara kwa mara kwa watoto

Uchaguzi wa matibabu baada ya kichwa kuuma

Uchaguzi wa matibabu hutegemea sana sababu ya maumivu ya kichwa.

 • Kuacha kutumia madawa yanayosababisha kichwa kuuma, kama nitrates.
 • Epuka kula aina fulani za vyakula vinavyosababisha kupata maumivu ya kichwa.
 • Mazoezi ya mara kwa mara, kama kuogelea au kutembea, kunaweza kudhibiti aina fulani ya maumivu ya kichwa.
 • Mafunzo ya relaxation
 • Madawa kama sumatriptan, propranolol hydrochloride, methysergide maleate, ergotamine tartrate, amitriptyline, valproic acid, au verapamil yanaweza kupunguza ukali wa maumivu na kuongeza ubora wa maisha ya mgonjwa.
 • Tiba ya chanzo kinachosababisha kichwa kuuma, kama upasuaji kutibu kiharusi, upasuaji, tiba ya mionzi au tibakemikali kutibu uvimbe kwenye ubongo, Antibiotiki kutibu maambukizi kwenye ubongo.

kichwa kuumaKuzuia

 • Epuka kula vyakula fulani ambavyo vinaweza kusababisha kichwa kuuma
 • Epuka matumizi mabaya ya pombe
 • Epuka kupata majeraha kichwani

Nini cha kutarajia?

Matarajio ya kupona hutegemea

 • Sababu ya maumivu ya kichwa

Vyanzo

https://medlineplus.gov/headache.html#:~:text=The%20most%20common%20type%20of,miss%20meals%2C%20or%20use%20alcohol.

Leave feedback about this

 • Quality
 • Price
 • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X