KIFAFA CHA MIMBA

KIFAFA CHA MIMBA

 • January 19, 2021
 • 0 Likes
 • 106 Views
 • 0 Comments

Maelezo ya jumla

Kifafa cha mimba (Eclampsia) ni degedege inayompata mwanamke mjamzito ambayo haihusiani kabisa na tatizo kwenye ubongo.

Dalili za kifafa cha mimba

 • Dalili ni pamoja na:
  • Maumivu ya misuli
  • Degedege
  • Kuwa mkali na mwenye hasira
  • Kupoteza fahamu
 • Dalili zinazoashiria kuwa unaelekea kupata kifafa cha mimba (preeclampsia) ni pamoja na:

Ni nini husababisha tatizo hili?

 • Sababu yake haifahamiki vyema, lakini watafiti wanadhani mambo yafuatayo yanachangia sana kutokea kwake.
  • Matatizo kwenye mishipa ya damu
  • Matatizo kwenye ubongo na mfumo wa neva
  • Mlo
  • Jeni-gene
 • Hata hivyo, hakuna nadharia iliyothibitishwa.
 • Kichaa cha mimba au eclampsia kwa kitaalamu hutokea baada ya viashiria kadhaa – wakati huu wa viashiria huitwa preeclampsia kwa kitaalamu. Kifafa cha mimba ni hali hatari sana wakati wa ujauzito na hutokea sambamba na shinikizo la juu la damu na kuongezeka uzito wa mwili.
 • Ni vigumu sana kutabiri au kujua ni wanawake gani wenye viashiria vya kupata kifafa cha mimba watapata ugonjwa huu baadae.

Nani yuko kwenye hatari zaidi?

Wanawake walio kwenye hatari zaidi ya kupata tatizo hili ni wale wenye dalili kali sana zinazoashiria kuwa watapata tatizo hili na:

Wakati gani utafute huduma ya matibabu haraka?

 • Nenda kituo cha afya kilicho karibu yako kama una dalili yoyote inayoashiria kuwa utapata kifafa cha mimba.
 • Dalili za dharura ni pamoja na degedege au kupoteza fahamu.

Utambuzi

 • Mtoa huduma ya afya atafanya uchunguzi wa mwili na kujiridhisha kuwa degedege uliyopata haijasababishwa na tatizo jingine la kiafya.
 • Utapimwa shinikizo la damu na kasi ya upumuaji wako
 • Vipimo vya damu na mkojo vinaweza kufanywa ili kuangalia:
  • Uwezo wa damu yako kuganda- wakati wa kifafa cha mimba mwanamke hupoteza kiwango kikubwa sana cha protini zinazosaidia damu kuganda kwenye mkojo
  • Kiwango cha creatinine- kiwango hiki kikiongezeka huashiria kwa figo zako zinaanza kuharibiwa na ugonjwa huu
  • Kiwango cha damu mwilini
  • Kiwango cha uric asidi- kiwango kikiongezeka huashiria kuwa figo zako zinaanza kuharibiwa
  • Kama ini lako linafanya kazi-Liver function test
  • Kiwango cha chembe sahani-chembe sahani husaidia damu kuganda
  • Kiwango cha protini kwenye mkojo –kwa hali ya kawaida protini haipaswi kuwa kwenye mkojo

Uchaguzi wa matibabu

 • Kama una viashiria (preeclampia) vya kupata kifafa cha mimba, daktari atafuatilia hali yako kwa ukaribu ili kuhakikisha kuwa dalili zako hazizidi na kupelekea shida hii.
 • Kujifungua ndio tiba thabiti kwa mtu mwenye dalili kali zinazoashiria kuwa atapata degedege, hili hufanyika ili kuzuia kupata kifafa cha mimba. Mwanamke akijifungua tatizo hili linakwisha. Kuendelea kubeba ujauzito ukiwa na tatizo hili inaweza kuwa hatari kwa mama na mtoto.
 • Daktari anaweza kufuatilia hali yako kwa ukaribu wakati wa dalili kali, ili kuruhusu mimba yako kukua mpaka kufikia wiki 32 – 34 au kama dalili sio kali sana mpaka wiki 36 – 37. Kusubiri hivi humpatia muda mtoto aliye tumboni kukua kabla hajazaliwa na kupunguza matatizo yanayotokana na kuzaa mtoto njiti.
 • Unaweza kupewa madawa ili kudhibiti degedege. Magnisium sulfate ni dawa salama kwa mama na mtoto.
 • Daktari anaweza kukupatia dawa ya kupunguza shinikizo la damu, lakini unaweza kutakiwa kuzaa kama shinikizo lako la damu halitashuka hata baada ya kupewa dawa.

Nini cha kutarajia?

Wanawake wengi wanaopata tatizo hili, wakiwahishwa kituo cha afya na kupata usaidizi wa mapema hujifungua salama tu.

Matatizo yanayoweza kutokea

 • Wakati wa kifafa cha mimba kuna uwezekano mkubwa zaidi wa kondo (placenta) kubanduka kutoka kwenye mfuko wa uzazi –placenta abruptio-mwanamke mwenye tatizo hili hutokwa damu nyingi zaidi
 • Uwezekano wa mtoto kuzaliwa akiwa njiti na matatizo yanayoambatana na hali hiyo huongezeka.
 • Mgonjwa anaweza kupata tatizo la damu kushindwa kuganda linaloitwa disseminated intravascular coagulation-DIC- Tatizo hili linaweza kusababisha mama kuvuja damu nyingi na hata kufa.

Kuzuia

 • Ni muhimu kwa wanawake wote wajawazito kupata huduma za matibabu mapema na kwa mwendelezo. Hii itasaidia utambuzi wa mapema na matibabu kwa viashiria vya kifafa cha mimba kabla tatizo halijawa kubwa zaidi.
 • Kutibu viashiria (preeclampsia) kunaweza kuzuia tatizo hili.

Vyanzo

http://www.nlm.nih.gov/medlineplus/ency/article/000899.htm

 • Share:

Leave Your Comment