KIGUGUMIZI :Ni nini, sababu, matibabu

Kigugumizi ni nini?

Kigugumizi ni tatizo la kuzungumza linalosababisha iwe ngumu kusema baadhi ya maneno au sauti. Watu wenye kigugumizi utakuta wanarudia sauti, maneno au sehemu ya neno. Wanaweza pia kukwama kwa muda mrefu kuliko kawaida kati ya sauti na maneno. Wanaweza kubinyabinya macho, kutikisa midomo, au kutikisa kichwa wanapokuwa na kigugumizi.

Nani anapata kigugumizi?

Mtu yeyote anaweza kupata kigugumizi, lakini mara nyingi inawatokea Watoto wanaoanza kujifunza kuongea. Watoto wengi wanaacha kupata kigugumizi kabla hawajawa watu wazima

KIGUGUMIZI
Mama akizungumza na mwanae

Nitajuaje kama mwanangu ana shida hii

Wazazi kwa kawaida hutambua kuwa Watoto wao wana tatizo kwa namna wanavyoongea. Mara nyingine, daktari anaweza kutambua kuwa kuna tatizo wakati wa kliniki ya Watoto. Daktari anaweza kukuambia kama kinaweza kuondoka chenyewe au kama mtoto atahitaji matibabu.

Kigugumizi kinatibiwa vipi?

Hakuna tiba ya kuponya kigugumizi, lakini kuna matibabu ya kumsaidia mwanao kuongea vizuri zaidi. Hata kama kigugumizi cha mwanao sio kikali sana, daktari anaweza kushauri afanyiwe matibabu ili kisizidi kuwa kibaya zaidi. Unaweza kuhitajika kumpeleka mwanao kwa daktari bingwa wa lugha na kuongea kwa matibabu.

Daktari anaweza pia kukupa mawazo na njia mbalimbali za kumsaidia mwanao kuongea vizuiri zaidi (kwa mfano; usiongee haraka sana au kumkatisha mtoto anapokuwa anaongea)

Vyanzo

https://medlineplus.gov/stuttering.html

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi