UGONJWA WA KIMETA:Sababu,dalili,matibabu,kuzuia

Maelezo ya jumla

Dalili hutofautiana kulingana na aina ya kimeta. Ugonjwa huu haumbikizwi kutoka kwa mtu moja mpaka mwingine kama ilivyo mafua. Watu walio kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi ni wataalamu wa maabara na watu wanashughulika na wanyama. Utambuzi wa ugonjwa huu utafanyika kwa kuangalia dalili na kufanya vipimo. Matibabu yanaweza kuwa antibiotics na antitoksini. Kuna chanjo iliyoidhinishwa kuzuia ugonjwa huu, hata hivyo, chanjo hii hutolewa tu kwa watu walio kwenye hatari ya kupata kimeta.

Kidonda cha kimeta

Je,Ni nini dalili za kimeta?

Dalili za kimeta zinaweza kuwa tofauti, kulingana na aina ya ugonjwa:
Ngozi

 • Hii ndio aina inayowapata watu wengi zaidi, mara nyingi mtu huipata baada ya chembe (spore) kuingia mwilini kupitia kidonda kwenye ngozi.
 • Dalili ya kwanza ni mchubuko kwenye eneo la uambukizo na kisha lengelenge (blister) hutokea. Baada ya muda lengelenge litatengeneza kidonda chenye weusi katikati. Mchubuko,lengelenge na kidonda haviumi. Katika hali nyingine, dalili kama vile kichwa kuuma, maumivu ya misuli, homa na kutapika, huweza kutokea
 • Kuna uwezekano mdogo wa maambukizi ya moja kwa moja kutoka kwenye kidonda cha mtu mmoja kwenda kwenye mwili wa mtu mwingine

Utumbo
Kwa ujumla aina hii hotokea baada ya kula nyama kutoka kwa mnyama aliyeambukizwa. Dalili za kwanza ni sawa na za kula chakula chenye sumu, na zinaweza kujumuisha:

Mapafu

 • Aina hii ya kimeta haipatikani kwa urahisi, na ni mara chache sana inawapata watu,lakini ndio yenye kusababisha vifo vingi zaidi kuliko aina nyingine.
 • Kwa kawaida maambukizi hutokea baada ya kuvuta hewa yenye chembe (spores) ya kimeta
 • Dalili za kwanza baada ya kuvuta hewa yenye chembe za kimeta ni sawa na mafua,na zinaweza kujumuisha:

Kimeta cha sindano

 • Dalili zake ni sawa na kimeta cha ngozi, lakini ugonjwa huu, unaweza kuenea kwa kasi mwili mzima
 • Homa na kuhisi baridi
 • Malengelenge au vipele vidogo vinavyowasha kwenye eneo ilipochomwa sindano.
 • Kidonda kwenye ngozi chenye sehemu ya katikati yenye rangi nyeusi, sehemu hii nyeusi hutokea baada ya malengelenge na vipele.
 • Uvimbe kuzunguka kidonda
 • Kunaweza kukatokea jipu kwenye sehemu iliyochomwa sindano
kimeta
Usile nyama isiyoiva vizuri

Ni nini husababisha kimeta?

Wanadamu wanaweza kuambukizwa kimeta kutoka katika vyanzo viwili:

 • Kimeta kutoka kwa wanyama
 • Wanadamu wanaweza kuambukizwa kimeta kwa kushughulikia bidhaa kutoka kwa wanyama walioambukizwa au kwa kuvuta hewa yenye chembe za kimeta toka kwenye bidhaa za wanyama walioambukizwa,kama Manyoya.
 • Watu wanaweza pia kuambukizwa aina ya kimeta inayoathiri utumbo kwa kula nyama ya wanyama walioambukizwa.
 • Kimeta ikitumika kama silaha
 • Kimeta inaweza kutumiwa kama Hii ilitokea Marekani mwaka 2001. Kimeta ilienezwa kwa makusudi kupitia mfumo wa posta, kwa kutuma barua zenye poda iliyokua na kimeta. Hii ilisababisha kesi 22 za maambukizi ya kimeta.

Kimeta haisambazwi kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.

Nani yuko kwenye hatari zaidi?

Watu wengine wanaweza kuwa katika hatari kubwa zaidi ya kuambukizwa:

 • Watu wenye kazi fulani:
  • Daktari wa wanyama/Veterinari
  • Wataalam wa maabara
  • Wazalishaji wa mifugo
  • Watu wanaoshughulikia bidhaa za wanyama
  • Wafanyakazi wa posta, wafanyakazi wa kijeshi, na wafanyakazi wa huduma ya dharura ,hawa wanaweza kuambukizwa kama kuna tukio la kigaidi la kutumia kimeta kama silaha
 • Wasafiri, hasa waendao kwenye maeneo kama vile:
  • Amerika ya Kati na Kusini
  • Afrika – kusini mwa Jangwa la Sahara
  • Asia ya Kati na kusini-magharibi
  • Ulaya ya Kusini na mashariki
  • Caribbean
 • Watu wanaotengeneza au kucheza ngoma zinazotengenezwa kwa ngozi ya Mifugo

Utambuzi

Ni watu waliokutana na chembe za kimeta pekee wanaoweza kuambukizwa kimeta. Utambuzi utafanyika baada ya uchunguzi wa mwili na vipimo. Vipimo vinaweza kujumuisha: [2]

(Katika kesi fulani ya kimeta ya mapafu)

 • Ili kuthibitisha utambuzi, vipimo vifuatavyo vinaweza kufanywa:
  • Gram stain na culture
  • Upimaji wa kingamwili (antibodies) au sumu katika damu

Magonjwa yenye dalili zinazofanana na kimeta

 • Homa ya mafua (Influenza)

Wakati gani utafute matibabu ya haraka?

Kama unaonyesha dalili za maambukizi ya kimeta, mwone mtoa huduma wako wa afya mara moja.

Pata matibabu mapema 

Uchaguzi wa matibabu

Antibiotics huhitajika katika mpango wa kutibu aina yoyote ya kimeta. Antibiotcs zinaweza kuzuia kutokea kwa ugonjwa kwa watu waliokutana na chembe za kimeta ,kabla hawajaanza kuonesha dalili. Kwa hiyo, ni muhimu kutambua na kuanza matibabu mapema.

 • Kuzuia ugonjwa baada ya kukutana na chembe ya kimeta
  • Matibabu ni tofauti kwa mtu ambaye amekutana na chembe za kimeta ,lakini hajaanza kupata dalili yoyote.
  • Watoa huduma ya afya watatumia antibiotics (kama vile ciprofloxacin, levofloxacin, doxycycline, au penicillin) pamoja na chanjo ya kimeta ili kuzuia maambukizi ya kimeta
  • Chembe (spores) za kimeta zinaweza kukaa mwilini mwa mtu hadi siku 60 bila kusababisha maambukizi yoyote. Watu ambao wamekutana na chembe za kimeta,wanapaswa kutumia antibiotics kwa kipindi hiki chote. Hii itawalinda kutokana na chembe (spores) yoyote iliyodumaa mwilini.
 • Matibabu baada ya maambukizi
  • Kwa kawaida,matibabu ni kutumia antibiotics kwa siku 60
  • Mafanikio hutegemea aina ya kimeta, na ni mapema kiasi gani tiba ilianza baada ya maambukizi
  • Antitoksini inapaswa kutumika pamoja na chaguzi nyingine za matibabu, ili kupambana na sumu ya kimeta mwilini. Kwa bahati mbaya antitokisini ni chache na hazipatikani kwa urahisi.
Pata chanjo ya kimeta kama uko kwenye hatari

Kuzuia

Kuna chanjo ( Anthrax Vaccine Adsorbed) inayoweza kukukinga dhidi ya kimeta ya ngozi na mapafu , hata hivyo haipatikani kwa umma. Chanjo hii haina bakteria yoyote na haiwezi kuambukiza kimeta. Mtu yeyote ambaye anahisiwa kuwa amekutana na chembe za kimeta anaweza kupewa chanjo hii. Watu kama wafanyakazi wa jeshi,wataalamu wa maabara,watu wanaosafiri kwenda kwenye maeneo yenye kimeta,wanaweza kupewa chanjo hii.
Matumizi ya dharura

 • Katika hali fulani, kama vile shambulizi la kigaidi linalohusiana na kimeta, chanjo inaweza kupendekezwa ili kuzuia ugonjwa kutokea kwa watu waliokutana na chembe za kimeta.
 • Kama hili litatokea, watu waliokutana na chembe za kimeta watapata sindano 3 za chanjo katika kipindi cha wiki nne ,pamoja na kozi ya antibiotics kwa siku 60.
 • Wakati wa dharura, watu pekee ambao hawapaswi kupewa chanjo, ni wale ambao wamepata athari kubwa za mzio (allergy) baada ya chanjo ya mwanzo.

Mimba

 • Wanawake wajawazito wanapaswa kupewa matibabu ya kinga sawa sawa na watu wengine,hii ni pamoja na antibiotics na chanjo.

Matumizi kwa watoto

 • Chanjo ya kimeta haipaswi kutolewa sambamba na chanjo nyingine za utotoni wakati wa tukio la kimeta

Nini cha kutarajia ?

Matarajio ya kupona ugonjwa wa kimeta hutegemea mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na:

 • Aina ya kimeta
 • Ni mapema kiasi gani kimeta ilitambuliwa
 • Aina ya bakteria anaesababisha kimeta
 • Umri wa mgonjwa na afya kwa jumla.

Kuanza tiba ya kimeta mapema iwezekanavyo, bila kujali aina ya kimeta, inaboresha matarajio ya ugonjwa kupona.

Matatizo yanayoweza kutokea

 • Kupata shida kupumua

Vyanzo

http://anthrax.emedtv.com/anthrax/anthrax-prognosis.html

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi