KIPANDAUSO:Sababu,dalili,matibabu

Maelezo ya jumla

Kipandauso ni maumivu makali ya kichwa, unahisi kama kinadunda na kinagonga upande mmoja tu hasa nyuma ya jicho au pembeni kidogo mwa jicho. Unaweza kuhisi kichefuchefu au kutapika  ,kuumizwa na kelele na macho yanashindwa kuhimili mwanga mkali. Maumivu ya kichwa yanayosababishwa na kipandauso yanaweza kudumu kwa masaa kadhaa mpaka siku 3, na yanaweza kuwa makali mpaka ukashindwa kufanya shughuli zako za kawaida.
Muda mfupi kabla haujapata tukio hili la kipandauso, kuna baadhi ya watu huona dalili za kuashiria kuwa tukio la maumivu ya kipandauso linakuja, kwa baadhi ya watu wanaanza kupata shida kuona vizuri na wengine wanapoteza uwezo wa kuonja ladha ya chakula au hata kusikia harufu yake. Kuna baadhi ya mambo na vitu ambavyo vinaweza kuongeza uwezekano wa kupata tukio la kipandauso kwa watu wenye shida hii, mambo kama msongo wa mawazo, kubadili utaratibu wa kulala, baadhi ya vyakula na vinywaji na kwa wanawake, mabadiliko ya kiwango cha homoni mwilini.

Mwone daktari kama

Ni vizuri kumwona daktari ili ahakikishe kuwa maumivu ya kichwa uliyonayo yanatokana na kipandauso na si sababu nyingineKipandauso

Unachoweza kufanya mwenyewe ukiwa na kipandauso

Tumia njia zifuatazo ili kujisaidia mwenyewe punde tu unapoanza kupata tukio la maumivu ya kichwa

  • Tumia dawa za kupunguza maumivu punde tu maumivu yanapoanza. Madawa ya kupunguza maumivu kama vile ‘’Acetaminophen’’, ‘’aspirin’’ au ‘’ibuprofen’’yanapaswa kutumiwa mara tu unapoanza kuhisi maumivu au mara tu unapoanza kuona dalili za kuashiria kuwa utapata tukio maumivu ya kichwa. TAHADHARI: Watoto na vijana wadogo walio kwenye balehe wasitumie ‘’aspirin’’ bila kushauriana na daktari kuhusu uwezekano wa tatizo hatari linaloitwa ‘’Reyes syndrome’’
  • Kama inawezekana, jaribu kujilaza sehemu yenye giza, iliyotulia, isiyo na kelele na purukushani nyingi, tumia mto kutegemeza kichwa na ujaribu kusinzia
  • Piga pafu za maji kila mara siku nzima, hasa kama unatapika
  • Vaa miwani myweusi ya kukukinga na mwanga wa jua unapokuwa nje kwenye mwanga mkali

Kuzuia kipandauso

Ili kupunguza makali au kuepusha kupata matukio ya kipandauso mara kwa mara, jaribu kufanya mambo yafuatayo

  • Tunza kumbukumbu kwa kuandika kwenye kitabu, angalau kwa wiki kadhaa, angalia ni kipindi gani unapata maumivu ya kichwa na ujaribu kuangalia ni vitu au mambo gani yanayochangia. Vyakula kama vile ‘’red wine’’, ‘’chocolate’’ na jibini/cheese ni vyakula vinavyoongeza uwezekano wa kupata tukio. Kama unatumia vinywaji vyenye ‘’caffeine’’ kama vile cola, kahawa au chai, ukiongeza au kupunguza sana kiwango unachotumia kuliko ilivyo kawaida yako, inaongeza pia uwezekano wa kupata tukio
  • Kama msongo wa mawazo ni sababu moja wapo, tafuta njia za kuupunguza (Angalia hapa)
  • Kula mara kwa mara na kunywa angalau glass 6-8 za maji kwa siku
  • Kuwa na utaratibu maalumu wa kupata usingizi. Ukipata usingizi kidogo au ukipata usingizi mwingi sana, vyote vinaweza kuongeza uwezekano wa kupata tukio la kipandauso

Mwone daktari kama una kipandauso

Omba msaada wa kimatibabu kama

  • Tukio la kipandauso halipoi hata baada ya kujaribu kujisaidia mwenyewe
  • Kama unapata matukio ya maumivu ya kichwa mara kwa mara au kama ni makali sana

Yapo madawa maalumu yanayoweza kupunguza matukio na ukali wa maumivu, mwone daktari akuandikie dawa (Dawa hizo zinapatikana ukiandikiwa na daktari pekee)

Vyanzo

https://medlineplus.gov/migraine.html

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi