Msaada wa Haraka! 255 759 07 960
Kwa Kina
Tafuta
 1. Home
 2. KIPARA

KIPARA

 • August 19, 2020
 • 2 pendwa
 • 66 Wameona
 • 0 Maoni

Maelezo ya jumla

Kipara (alopecia) ni hali ya kupoteza nywele zote au sehemu ya nywele.

Je, Ni nini dalili za kipara?

Kupotea kwa nywele hutokea taratibu, hatua kwa hatua, na nywele zinaweza kuanza kupungua eneo moja la kichwa na kusambaa kichwa kizima. Kwa kawaida mtu anapoteza karibu nywele 100 za kichwa kila siku. Kichwa cha wastani kina nywele kama 100,000 hivi.

Ni nini kinasababisha kipara?

Kutokea kwa ghafla tatizo la kimwili au msongo wa mawazo  kunaweza kusababisha nusu mpaka robo tatu ya nywele zako kupukutika, hii inajulikana kitaalamu kama Telogen effluvium. Utaona nywele zikichomoka, hasa wakati wa kuziosha kwa shampuu, kuchana, au hata ukipitisha mkono kwenye nywele zako. Unaweza usilione hili kwa muda wa wiki mpaka miezi kadhaa baada ya tukio lililo kusababishia msongo. Kuchomoka kwa nywele kutapungua ndani ya miezi 6 mpaka 8.

Ni nini husababisha aina hii ya upotevu wa nywele:

 • Kujifungua
 • Mlo wa kujinyima – aina hii ya mlo huwa na virutubisho vichache na mara nyingi hutumiwa na watu wanaotaka kupunguza uzito/unene haraka. Vyakula hivi havina protini ya kutosha na kwa sababu hii nywele huanza kuchomoka
 • Homa kali au maambukizi makali
 • Baada ya upasuaji mkubwa, ugonjwa mkubwa au kupoteza damu nyingi ghafla
 • Aina fulani za madawa, ikiwa ni pamoja na retinoids, dawa za kupanga uzazi , beta-blockers, baadhi ya dawa za kutibu sonona, NSAIDs (hii ni pamoja na iburpofen) na calcium channel blockers
 • Msongo mkubwa wa mawazo

Sababu nyingine zinazoweza kusababisha kupotea kwa nywele, ni pamoja na:

 • Alopecia areata – hii ni hali ya kitabibu ambayo husababisha nywele za mgonjwa kuchomoka kwa mafungu na kuacha alama za mviringo kama shilingi mahala mahala kichwani,kidevuni na hata kwenye nyusi
 • Upungufu wa damu
 • Magonjwa ya mfumo wa kinga ya mwili kama vile lupus
 • Kuungua moto
 • Magonjwa mengine ya kuambukiza kama vile kaswende
 • Kuosha nywele kwa shampuu kulikopitiliza 
 • Mabadiliko ya homoni
 • Tabia ya kuvuta nywele au kusugua kichwa hasa wakati wa wasiwasi
 • Tiba ya mionzi (radiation therapy)
 • Magonjwa ya tezi dundumio (thyroid disease)
 • Tinea capitis – hawa ni fangasi wanaharibu nywele kichwani na kuacha sehemu za mviringo sizizo na nywele (ringworm of the scalp)
 • Uvimbe kwenye tezi za ovari au adrenal

Nani yuko kwenye hatari zaidi?

Baadhi ya wanawake wenye umri kati ya miaka 30 mpaka 60, hugundua kuwa nywele zao zinakua nyembamba na kuanza kuchomoka. Nywele hupukutika kwa wingi sana mwanzoni na baadae hupungua au kuacha kabisa. Hakuna sababu inayofahamika inayosababisha upotevu wa aina hii wa nywele.

Kadri umri unapoongezeka, nywele za wanaume na wanawake huwa nyembamba.  Upara mara nyingi hausababishwi na ugonjwa. Upara huhusishwa na umri,urithi na mabadiliko ya homoni . Upara wa kurithi huwaathiri zaidi wanaume kuliko wanawake. Karibu nusu ya wanaume huanza kuwa na upara wanapofikia umri wa miaka 30, na wengi huwa na upara au pattern ya upara wakifika umri wa miaka 60.

Wakati gani utafute matibabu ya haraka?

Mwone daktari kama:

 • Unapoteza nywele isivyo kawaida (unusual pattern)
 • Unapoteza nywele haraka sana au wakati ukiwa na umri mdogo (kwa mfano, wakati wa balehe au miaka ya ishirini na)
 • Pamoja na kupoteza nywele, unapata maumivu au muwasho.
 • Ngozi ya kichwa katika eneo lililopoteza nywele ni jekundu,lenye ukurutu au haliko kawaida.
 • Una  chunusi, nywele usoni, au mzunguko usio wa kawaida wa hedhi
 • Wewe ni mwanamke na una pattern ya upara unaofanana na wa mwanaume
 • Unapoteza nywele na kusababisha upara kwenye ndevu au nyusi.
 • Uzito wako umekua ukiongezeka au misuli yako imelegea

Uchaguzi wa matibabu

Kupotea kwa nywele kunakotokana na kukatika damu ya mwanamke (menopause) au kujifungua mtoto,hurudi katika hali ya kawaida baada ya miezi 6 mpaka miaka 2.

Upotevu wa nywele unaotokea kwa sababu ya ugonjwa (kama vile homa), tiba ya mionzi, matumizi ya dawa, au sababu nyingine, hauhitaji matibabu. Nywele mara nyingi hukua tena baada ya ugonjwa kupona au tiba ya mionzi ikikamilika. Kwa kipindi hicho unaweza kuvaa Wig,kofia au kifuniko kingine mpaka nywele zitakapokua tena.

Njia isiyo ghali sana ya kukabiliana na upotevu wa nywele ni kutumia Weaves za nywele au kubadilisha mtindo wa kufunga/kunyoa nywele.

Nini cha kutarajia?

Historia ya mgonjwa na uchunguzi makini wa nywele na ngozi ya kichwa unatosha kabisa kutambua sababu ya kupukutika kwa nywele zako.

Daktari wako atauliza maswali ya kina kama vile:

 • Je! Unapoteza nywele kwenye kichwa tu au na sehemu nyingine za mwili pia?
 • Je, kuna pattern yoyote kwenye upotevu wako wa nywele, kamavile  msitari wa nywele za mbele (hairline) unaozidi kurudi ndani, nywele kuzidi kuwa nyembamba au nywele zinazopukutika kichwani mwote?
 • Umeumwa ugonjwa wowote hivi karibuni au kama ulipata homa kali?
 • Je, unapaka rangi (dye) nywele zako?
 • Je,una blow dry nywele zako? Mara ngapi?
 • Ni mara ngapi una shampuu nywele zako?
 • Ni aina gani ya shampuu, dawa ya nywele, gel, au bidhaa nyingine unazoweka kwenye nywele zako?
 • Je,Umekuwa na msongo wa mawazo usio kawaida hivi karibuni?
 • Je, una tabia ya kuvuta nywele au kusugua kichwa unapokuwa na wasiwasi ?
 • Je! Una dalili zingine kama kuwashwa, ukurutu au wekundu kwenye ngozi ya kichwa chako?
 • Je, ni madawa gani unayoyatumia kwa sasa?

Vipimo vifuatavyo vinaweza kufanyika (lakini mara nyingi havihitajiki)

 • Vipimo vya damu ili kuchunguza kama kuna magonjwa
 • Uchunguzi wa unywele ulionyofolewa

Mashilingi shilingi yanayosababishwa na fungus za kichwa yanaweza kuhitaji utumie dawa za kumeza kama vile griseofulvin. Creams na lotions zinazopakwa kwenye ngozi zinaweza kushindwa kuingia ndani ya vinyweleo ili kuvitibu na kuua fungus (kuvu).

Vyanzo

http://www.nlm.nih.gov/medlineplus/ency/article/003246.htm
 • Shirikisha:

Leave Your Comment