Uzazi wa mpango

KITANZI CHENYE KICHOCHEO KIMOJA (LEVONORGESTREL)

Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko

Kitanzi Chenye Levonorgestrel ni Nini?

Kitanzi chenye kichocheo kimoja (levonorgestrel) ni kiplastiki chenye umbo la T ambacho hutoa kiasi kidogo cha kichocheo cha levonorgestrel kila siku. (Levonorgestrel ni projestini inayotumika sana kwenye vipandikizi au vidonge vya kumeza kuzuia mimba).

 • Mtoa huduma ya afya aliyepata mafunzo maalum huingiza kitanzi kwenye kizazi cha mwanamke kupitia ukeni na shingo ya kizazi (seviksi).
 • Pia kinajulikana kama Kitanzi chenye kichocheo kimoja.
 • Kimsingi hufanya kazi kwa kuzuia ukuaji wa tabaka la ndani la uterasi (endometria)

Mambo Muhimu kuhusu kitanzi chenye kichocheo kimoja

 • Huzuia mimba kwa muda mrefu. Kinafanya kazi vizuri sana kwa miaka 5, na baada ya hapo hakiwezi kuzuia mimba.
 • Huingizwa kwenye kizazi na mtoa huduma aliyepata mafunzo maalum.
 • Mteja hatakiwi kufanya lolote mara kitanzi kikishawekwa.
 • Mabadiliko ya hedhi ni ya kawaida lakini hayana madhara. Kawaida, damu za hedhi huwa kidogo na hutoka kwa siku chache, au kupata hedhi mara chache au isiyotabirika.

Kitanzi chenye kichocheo kimoja kina Ufanisi Kiasi Gani?

Ni Moja ya njia zenye ufanisi mkubwa na wa muda mrefu:

 • Chini ya mimba 1 hutokea kwa wanawake 100 wanaotumia kitanzi chenye levonorgestrel kwa mwaka wa kwanza (2 kwa wanawake 1,000). Hii ina maana kuwa wanawake 998 kati ya kila 1,000 wanaotumia kitanzi chenye levonorgestrel hawatapata mimba.
 • Hatari kidogo ya mimba inaendelea kuwepo baada ya mwaka wa kwanza wa kutumia kitanzi na kuendelea ikiwa mwanamke anatumia kitanzi chenye levonorgestrel.
  • Zaidi ya miaka 5 ya kutumia kitanzi chenye levonorgestrel: Chini ya mimba 1 hutokea kwa wanawake 100 (5 hadi 8 kwa wanawake 1,000).
 • Imethibitishwa kutumika kwa muda unaofi ka miaka 5.

Uweza wa kushika tena mimba baada kitanzi kutolewa: Bila kuchelewa Kinga dhidi ya magonjwa yanayoambukizwa kwa ngono: Hakuna kitanzi chenye kichocheo kimoja

Kuhusu Athari za kitanzi chenye kichocheo kimoja

Madhara yanayofahamika zaidi Mabadiliko ya mpangilio wa hedhi; Hapati hedhi, Hedhi kidogo, hedhi ya mara chache au isiyotabirika
Chunusi, maumivu ya kichwa, kujaa na maumivu ya matiti, kichefuchefu, kuongezeka uzito, kizuguzungu, mabadiliko ya hisia na madhara mengine yanayoweza kutokea.
Mabadiliko mengine ya mwili yanayoweza kutokea: Uvimbe wa ovari (sisti ya ovari)
Ufafanuzi kuhusu madhara haya Mabadiliko ya hedhi kwa kawaida si dalili za ugonjwa.
Kawaida hupungua baada ya miezi michache ya mwanzo baada ya kuwekwa kitanzi.
Unaweza kurudi kutafuta msaada kama madhara yanamsumbua.

 

Faida, Hasara na Matatizo ya kutumia kitanzi chenye kichocheo kimoja

Faida za kiafya

 • Husaidia kukinga dhidi ya:
  • Hatari ya kushika mimba
  • Anemia kutokana na upungufu wa madini ya chuma
 • Inaweza kukinga dhidi ya:
  • Ugonjwa wa uvimbe wa nyonga
 • Hupunguza:
  • Maumivu ya tumbo wakati wa hedhi
  • Dalili za endometria (maumivu ya nyonga, hedhi isiyotabirika)

Hasara kiafya

 • Hakuna

Matatizo

 • Nadra: Kutobolewa ukuta wa uterasi na kitanzi au kifaa kinachotumika kuingiza kitanzi. Kwa kawaida hupona bila matibabu.
 • Nadra sana: Mimba kuharibika, kujifungua kabla ya wakati, au maambukizi hutokea mara chache sana ambapo mwanamke anaweza kushika mimba akiwa na kitanzi

Nani hawezi kutumia kitanzi chenye kichocheo kimoja?

Ikiwa jibu ni “Ndio”, kwa maswali yafuatayo, haupaswi kutumia kitanzi chenye kichocheo kimoja

 1. Je umejifungua muda usiozidi wiki 4 zilizopita? NDIYO Anaweza kuwekwa kitanzi wiki 4 baada ya kujifungua
 2. Je kwa sasa una tatizo la damu kuganda kwenye vena za ndani ya miguu au mapafu? NDIYO Kama ataripoti kuwa na tatizo la kuganda damu kwa sasa (isipokuwa kuganda kidogo), msaidie kuchagua njia isiyokuwa na vichocheo.
 3. Je unaugua sirosisi kali ya ini, ugonjwa wa ini, au uvimbe wa ini? (Je macho au ngozi yake ina umanjano usio kawaida? [dalili za umanjano] NDIYO Kama ataripoti kuwa na ugonjwa mkali wa ini (umanjano, hepatitisi, sirosisi kali, uvimbe wa ini), usimweke kitanzi chenye levonorgestrel. Msaidie kuchagua njia isiyo na vichocheo.
 4. Je una au umewahi kuwa na saratani ya matiti? NDIYO Usimweke kitanzi chenye levonorgestrel. Msaidie kuchagua njia isiyokuwa na vichocheo.

Kwa kawaida, mwanamke mwenye hali yoyote kati ya hizo zilizoorodheshwa hapa asitumie kitanzi chenye levonorgestrel. Hata hivyo, katika mazingira maalum, ambapo hakuna njia nyingine inayofaa au kukubalika kwa hali yake, mtoa huduma mwenye ujuzi wa kutosha ambaye anaweza kuchunguza kwa makini tatizo maalum ya mwanamke huyo anaweza kuamua kuwa atumie kitanzi chenye levonorgestrel.

Lini Uanze Kutumia kitanzi chenye kichocheo kimoja

Mara nyingi mwanamke anaweza kuanza kutumia kitanzi chenye levonorgestrel wakati wowote kama kutakuwa na uhakika wa kutosha kuwa hana mimba.

Hali ya mwanamke (Maalumu) Aanze lini kutumia
Asiyepata hedhi Wakati wowote kama kutakuwa na uhakika wa kutosha kuwa hana mimba. Atahitaji kutumia kinga kwa siku 7 za mwanzo baada ya kuwekwa kitanzi.
Aliyejifungua na ananyonyesha wakati wote chini ya miezi 6 Kama bado hajaanza kupata hedhi, anaweza kuwekwa kitanzi wakati wowote kati ya wiki 4 na miezi 6 baada ya kujifungua. Hakuna haja ya kutumia kinga
Aliyejifungua na hanyonyeshi au ananyonyesha kidogo chini ya miezi 6 Chelewesha uwekaji wa kitanzi mpaka angalau wiki 4 baada ya kujifungua
Kama hajaanza kupata hedhi, anaweza kuwekwa kitanzi wakati wowote kama kutakuwa na uhakika wa kutosha kuwa hana mimba. Atahitaji kutumia kinga kwa siku 7 za mwanzo baada ya kuwekwa kitanzi.
Aliyejifungua baada ya miezi 6 Kama bado hajaanza kupata hedhi, anaweza kuwekwa kitanzi wakati wowote kama kutakuwa na uhakika wa kutosha kuwa hana mimba. Atahitaji kutumia kinga kwa siku 7 baada ya kuwekwa kitanzi
Baada ya kutoa au mimba kuharibika Kitanzi kinaweza kuweka ndani ya siku 7 (hata baada tu ya mimba kutoka) Hakuna haja ya kutumia kinga.
Kama ni zaidi ya siku 7 baada ya mimba kutoka, atahitaji kutumia kinga kwa siku 7 baada ya kuweka kitanzi.
Kitanzi kisiwekwe kama mwanamke ana maambukizi baada ya kujifungia
Kubadili kutoka njia yenye vichocheo Kara moja, kama amekuwa akitumia njia hiyo wakati wote na kwa usahihi au kama kuna uhakika wa kutosha kuwa hana mimba. Hakuna haja ya kusubiri kupata hedhi. Hakuna haja ya kutumia kinga.
Kama anabadili kutoka njia ya sindano, anaweza kuwekwa kitanzi wakati wa kurudia kuchoma sindano nyingine utakapofi ka. Atahitaji kutumia kinga kwa siku 7 za mwanzo baada ya kuwekwa kitanzi.

 

Baada ya kumeza vidonge vya dharura kuzuia mimba Kitanzi kinaweza kuwekwa ndani ya siku 7 baada ya kuanza hedhi au wakati wowote ikithibitishwa vya kutosha kuwa hana mimba. Mpatie kinga au vidonge vyenye vichocheo viwili aanze kutumia baada ya kumaliza kumeza vidonge vya dharura kuzuia mimba, atumie mpaka atakapowekwa kitanzi.

 

Kama mtoa huduma ya afya hatokuwa na uhakika kuwa mwanamke hana ujauzito, atapaswa kupewa njia mbadala mpaka pale atakapokuwa na uhakika kuwa hana ujauzito

Jinsi ya Kuweka Kitanzi chenye kichocheo kimoja

Kabla ya kuweka kitanzi Atakuelekeza utaratibu wa kuweka kitanzi.
Atakuonesha spekulamu, tenakulamu, na kitanzi na kifaa cha kuingizia kwenye paketi.
Atakueleza kuwa utajisikia vibaya au misuli kukakamaa wakati wa kuweka, na kuwa hili ni la kutarajiwa.
Atakuomba umwambie wakati wowote utakapojisikia vibaya au maumivu.
Wakati mwingine atakupatia Iburprofen (200-400 mg), paracetamol (325-1000 mg), au dawa yoyote ya kupunguza maumivu dakika 30 kabla ya kuweka kitanzi ili kusaidia kupunguza kukakamaa kwa misuli na maumivu.
Wakati wa kuweka kitanzi Mtoa atakueleza kila kinachoendelea, hatua kwa hatua.
Atakujulisha kabla ya kuanza hatua ambayo itasababisha maumivu au mshtuko.
Atakuuliza  kila wakati kama unasikia maumivu

Kufafanua Utaratibu wa kuweka Kitanzi

Mwanamke ambaye amechagua kutumia kitanzi anahitaji kujua kutatokea nini wakati wa kukiweka.

 1. Mtoa huduma anafanya uchunguzi wa nyonga ili kujua kama anaweza kuitumia. Kwanza mtoa huduma anafanya uchunguzi kwa macho na kisha kuingiza spekulamu kwenye uke ili kukagua seviksi.
  • Je kuna aina yoyote ya kidonda kwenye vulva, uke au shingo ya kizazi (seviksi)? – NDIYO Inawezekana una ugonjwa wa ngono
  • Je anasikia maumivu kwenye tumbo lake la chini unapochezesha shingo ya kizazi?NDIYO – Inawezekana mimba imetunga nje ya kizazi
  • Je anapata maumivu kwenye kizazi, ovari, au mrija wa fallopio (maumivu ya adneksa)?- NDIYO -Inawezekana mimba imetunga nje ya kizazi.
  • Je anatokwa usaha kutoka kwenye shingo ya kizazi?NDIYO – Inawezekana ugonjwa wa ngono au mimba imetunga nje ya kizazi.
  • Je Shingo ya kizazi inatoa damu kirahisi ikiguswa? NDIYO Inawezekana ugonjwa wa ngono au saratani ya shingo ya kizazi.
  • Je kuna mabadiliko yasiyo kawaida ya anatomia ya mvungu wa uterasi ambayo yatakwamisha kuweka kwa usahihi kitanzi? NDIYO Iwapo mabadiliko yasiyo kawaida ya anatomia yamevuruga mvungu wa uterasi, itashindikana kuweka vizuri kitanzi. Msaidie kuchagua njia nyingine.
  • Je ulishindwa kujua ukubwa na/au mahali ilipo uterasi (mji wa mimba)? NDIYO Kujua ukubwa na mahali ilipo uterasi kabla ya kuweka kitanzi ni muhimu ili kuhakikisha unaweka vizuri kitanzi na kupunguza hatari ya kuichana. Iwapo itashindikana kujua ukubwa na mahali ilipo uterasi, usiweke kitanzi. Msaidie kuchagua njia nyingine.
 1. Mtoa huduma anasafi sha seviksi na uke kwa kutumia dawa za kuua vijidudu.
 2. Mtoa huduma anaingiza taratibu tenakulamu kupitia spekulamu na kufunga tenakulamu ili iweze kushikilia vizuri seviksi na uterasi.
 3. Mtoa huduma kwa taratibu anapitisha kipima uterasi kupitia kwenye seviksi ili kupima kina na mahali ilipo uterasi.
 4. Mtoa huduma anaweka kitanzi kwenye kifaa cha kuingizia wakati vyote vikiwa kwenye paketi iliyofungwa iliyotasishwa.
 5. Mtoa huduma kwa taratibu anaingiza kitanzi na kuondoa kifaa cha kuingizia.
 6. Mtoa huduma anakata nyaya zilizo kwenye kitanzi na kuacha karibu sentimeta 3 zikining’inia kwenye seviksi.
 7. Baada ya kuweka kitanzi, mwanamke apumzike. Abaki kwenye meza ya uchunguzi mpakaatakapojisikia yupo tayari kuvaa nguo.

Maelekezo Maalum baada ya kuwekewa kitanzi

Tarajia misuli kukakamaa na maumivu Tarajia mkakamao wa misuli na maumivu kwa siku chache baada ya kuwekwa kitanzi.
Unaweza ktumia iburprofen (200-400 mg), paracetamol (325-1000 mg), au dawa nyingine za kupunguza maumivu.
Pia, tarajia kupata hedhi au matone matone mara baada ya kuwekwa kitanzi. Hii inaweza kuendelea kwa miezi 3 hadi 6.
Unaweza kuangalia nyaya Kama unataka, unaweza kukagua nyaya za kitanzi chako mara kwa mara, hasa katika miezi michache ya mwanzo na baada ya hedhi ili kuthibitisha kuwa kitanzi chako bado kipo mahali pake.
Muda wa kinga kuzuia mimba Ni vizuri kujadili namna ya kukumbuka tarehe ya kurudi kliniki.
Unaweza ukapewa kadi yenye taarifa ifuatayo kwa maandishi kwenye kadi ya kukumbushia: Aina ya kitanzi ulichonacho, Tarehe ya kuweka kitanzi, Mwezi na mwaka kitanzi kitakapotakiwa kutolewa au kubadilishwa, Uende wapi kama utakuwa na matatizo au maswali kuhusu kitanzi chako

Sababu za kurudi kituo cha afya

 • Rudi kama unafikiri kitanzi kinaweza kuwa kimetoka. Kwa mfano:
  • Unahisi nyaya hazipo.
  • Unahisi plastiki ngumu ya kitanzi imetoka nje kiasi fulani.
 • Una dalili za ugonjwa wa uvimbe wa nyonga (PID) (maumivu yanayozidi kuongezeka au makali tumboni, maumivu wakati wa kufanya ngono, kutokwa uchafu usio wa kawaida ukeni, homa, kuhisi baridi, kichefuchefu, na kutapika), hasa katika siku 20 za mwanzo baada ya kuwekwa kitanzi.
 • Unafikiri unaweza kuwa na mimba.
 • Ushauri wa afya kwa ujumla

Kuondoa Kitanzi

MUHIMU: Mtoa huduma hawezi kumkatalia au kumchelewesha mwanamke anapotaka kutolewa kitanzi, bila kujali sababu zake, hata kama ni sababu binafsi au za kiafya. Watalamu wote wa afya wanafahamu kuwa, haipaswi kushinikzwa au kulazimishwa kuendelea kutumia kitanzi.

Iwapo utaona ugumu kuvumilia athari za kitanzi, jadili matatizo unayopata na daktari. Atakusaidia kuangalia kama ingefaa ujaribu kushughulikia tatizo au utolewe kitanzi mara moja.

Kazi ya kutoa kitanzi kawaida ni rahisi. Inaweza kufanyika wakati wowote wa mwezi. Utoaji unaweza kuwa rahisi zaidi wakati wa hedhi, wakati shingo ya kizazi inapokuwa imelainika.

Maelezo ya Taratibu za Utoaji wa Kitanzi

Kabla ya kutoa kitanzi, mtaalamu atakuelekeza kutatokea nini wakati wa kukitoa:

 1. Mtoa huduma ataingiza spekulamu ili kuona shingo ya kizazi (seviksi) na nyaya za kitanzi na kusafisha kwa makini seviksi na uke kwa kutumia dawa ya kuua vijidudu, kama vile iodine.
 2. Mtoa huduma atamwomba mwanamke avute ndani hewa taratibu na kutulia na aseme kama anasikia maumivu wakati wa kutoa kitanzi.
 3. Kwa kutumia koleo nyembamba, mtoa huduma atavuta waya za kitanzi taratibu na kwa makini mpaka kitanzi kitoke kabisa nje ya shingo ya kizazi (seviksi).

Kurekebisha Mambo Yaliyoeleweka Vibaya

Vitanzi:

 • Mara chache husababisha ugonjwa wa uvimbe wa nyonga.
 • Haviongezi hatari ya kupata magonjwa yaambukizwayo kwa ngono, pamoja na VVU.
 • Haviongezi hatari ya mimba kuharibika wakati mwanamke anaposhika mimba baada ya kitanzi kuondolewa.
 • Haviwasababishi wanawake wagumba.
 • Havisababishi mtoto kuzaliwa na kasoro.
 • Havisababishi saratani.
 • Haviendi kwenye moyo au akili.
 • Havisababishi kukosa raha au maumivu kwa mwanamke wakati wa kujamiiana.
 • Kiasi fulani hupunguza hatari ya mimba kutunga nje ya kizazi

Vyanzo

https://medlineplus.gov/birthcontrol.html

Leave feedback about this

 • Quality
 • Price
 • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X