Uzazi wa mpango

KONDOMU ZA KIKE

Kondomu za Kike Ni Nini?

Kondomu za kike ni kifuko kilichotengenezwa kutokana na plastiki nyembamba, laini, inayopitisha mwanga, ambacho huingizwa ukeni.

  • Ina pete zinazobonyea pande zote mbili
  • Pete moja upande uliofungwa husaidia kuingiza kondomu
  • Pete upande ulio wazi hushikilia sehemu ya kondomu ikae nje ya uke
 • Zimewekwa vilainisho vya silikoni ndani na nje.
 • Kondomu za kike za mpira zinaweza kupatikana kwenye baadhi ya nchi.
 • Hufanya kazi kwa kuweka kizuizi kinachozuia mbegu za kiume kuingia ukeni, na kuzuia mimba. Pia huwazuia wasiambukizane magonjwa kutoka kwenye uume, au kwenye uke.

Mambo Muhimu kuhusu kondomu za kike

 • Kondomu za kike husaidia kuzuia magonjwa ya ngono, pamoja na VVU. Kondomu ni njia pekee ya uzazi wa mpango ambayo inaweza kuzuia mimba na magonjwa ya ngono.
 • Inahitaji kutumiwa kwa usahihi kwa kila tendo la ngono ili kuwa na kinga ya kutosha.
 • Mwanamke anaweza kuanza kutumia kondomu lakini njia hii inahitaji ushirikiano wa mwenzi wake.
 • Inaweza kuhitaji kufanya mazoezi. Kuingiza na kutoa kondomu ya kike kutoka ukeni huwa rahisi baada ya kupata uzoefukondomu ya kike

Kwanini Baadhi ya Wanawake Wanasema Wanapenda Kondomu za Kike

 • Wanawake wanaweza kuanza kuzitumia
 • Zina ulaini, unyevunyevu ambao hufanya mtumiaji apate hisia kama mtu ambaye hakutumia kondomu wakati wa tendo la ngono tofauti na kondomu za kiume za mpira.
 • Husaidia kuzuia mimba na magonjwa ya ngono, pamoja na VVU.
 • Pete ya nje huongeza hamu kwa baadhi ya wanawake.
 • Zinaweza kutumiwa bila kumwona mtoa huduma ya afya.

Kwanini Baadhi ya Wanaume Wanasema Wanapenda Kondomu za Kike

 • Zinaweza kuvaliwa mapema hivyo hazileti usumbufu katika ngono.
 • Hazibani au kubinya kama kondomu za kiume.
 • Hazipunguzi hisia za ngono kama kondomu za kiume.
 • Hazihitaji kutolewa mara moja baada ya kukojoa.

Faida Kiafya, na Hatari Kiafya

                Faida zinazojulikana Kiafya Hatari Zinazojulikana Kiafya
Husaidia kuzuia: Mimba na Magonjwa ya ngono, pamoja na VVU Hakuna

Hatua 5 Muhimu za Kutumia Kondomu ya Kike

Hatua muhimu Maelezo muhimu
1.      Tumia kondomu mpya ya kike kwa kila tendo la ngono Kagua paketi ya kondomu. Usiitumie kama imechanika au kuharibika. Epuka kutumia kondomu iliyopitisha tarehe ya mwisho ya kutumika – fanya hivyo kama tu hakuna kondomu mpya.
Ikiwezekana, safi sha mikono yako kwa sabuni laini na kausha mikono yako kabla ya kuingiza kondomu.
2.      Kabla ya kukutana kimwili ingiza kondomu ukeni Inaweza kuingizwa hata saa 8 kabla ya ngono. Ili kupata kinga ya kutosha, ingiza kondomu kabla uume haujagusana na uke.
Chagua mkao ambao hausumbui kuingiza – chuchumaa, nyanyua mguu mmoja, kaa, au lala.
Bana pande mbili za kondomu ya kike ili kusambaza kilainisho kote.
Shika pete mwisho uliozibwa, na ikunje iwe ndefu na nyembamba.
Kwa mkono mwingine, tenganisha mashavu ya nje ya uke (labia) na funua tundu la uke.
Sukuma taratibu pete ya ndani kwenye uke kulingana na jinsi itakavyoingia. Ingiza kidole ndani ya kondomu ili iingie vizuri. Karibu sentimita 2 hadi tatu za kondomu na pete ya nje ibaki nje ya uke.
3.      Hakikisha kuwa uume unaingia kwenye kondomu na kubaki ndani ya kondomu Mwanaume au mwanamke aelekeze kwa makini ncha ya uume iingie ndani ya kondomu – si kati ya kondomu na ukuta wa uke. Kama uume utaenda nje ya kondomu, chomoa kisha jaribu tena.
Iwapo kondomu kwa bahati mbaya ikivutwa nje ya uke au kusukumwa ndani wakati wa ngono, irudishe kondomu mahali pak
4.      Baada ya mwanaume kuchomoa uume wake, shika pete ya nje ya kondomu, izungushe ili kufungia majimaji yaliyo ndani, na taratibu ichomoe kutoka ukeni Kondomu ya kike haihitaji kutolewa haraka baada ya kumaliza ngono.
Chomoa kondomu kabla ya kusimama, ili kuepuka kumwaga manii.
Kama wawili hao watataka kufanya ngono tena, watumie kondomu mpya.
Haishauriwi kurudia kutumia kondomu ya kike
5.      Tupa kondomu iliyotumika mahali salama Fungasha kondomu kwenye paketi yake na itupe kwenye shimo au choo cha shimo. Usitupe kondomu kwenye choo cha kuvuta maji, kwa kuwa inaweza kusababisha matatizo ya kuziba

 

Vilainisho kwa ajili ya Kondomu za Kike

Kondomu za kike za plastiki huja zikiwa zimewekwa vilainisho vya silikoni. Tofauti na kondomu nyingi za kiume, ambazo zimetengenezwa kutokana na mpira, kondomu za plastiki zinaweza kutumiwa na aina yoyote kilainisho – kiwe kinatokana na maji, silikoni, au mafuta.

Baadhi ya kondomu za kike huja zikiwa na kilainisho cha ziada kwenye paketi. Baadhi ya kliniki zinaweza kuwapatia wateja kilainisho cha ziada. Kama mteja atahitaji kilainisho cha ziada, anaweza pia kutumia maji safi , mate, mafuta yoyote au losheni, kilainisho kilichotengenezwa kwa gliserini au silikoni.

Imani potofu kuhusu kondomu za kike

Kondomu za kike:

 • Haziwezi kupotelea ndani ya mwili wa mwanamke.
 • Hazina ugumu wa kutumia, lakini inabidi kujifunza kutumia kwa usahihi.
 • Hazina matundu yanayoweza kupitisha VVU.
 • Hutumiwa na wanandoa.
 • Hazikutengenezwa kwa matumizi nje ya ndoa tu. Hazisababishi ugonjwa kwa mwanamke kwa sababu huzuia manii au mbegu za kiume kuingia kwenye mwili wa mwanamke.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/birthcontrol.html

Leave feedback about this

 • Quality
 • Price
 • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X