Uzazi wa mpango

KONDOMU ZA KIUME

Kondomu za Kiume ni Nini?

Kondomu za kiume ni kifuko au kifuniko, ambacho huvalishwa kwenye uume unaposimama.

  • Pia zinajulikana kama “mpira”, “soksi”, “salama” na kinga; zinajulikana kwa majina mbalimbali ya uzalishaji.
  • Nyingi hutengenezwa kwa mpira mwembamba laini (latex).
  • Hufanya kazi kwa kuweka kizuizi kinachofanya mbegu ya kiume isiingie ukeni, na kuzuia mimba. Pia huzuia maambukizi katika manii, kwenye uume, au kwenye uke yasimwambukize mwenza.

Mambo Muhimu kuhusu kondomu za kiume

  • Kondomu za kiume husaidia kinga dhidi ya magonjwa ya ngono, pamoja na VVU. Kondomu ni njia pekee ya uzazi wa mpango inayokinga dhidi ya kupata mimba na magonjwa ya ngono.
  • Zinahitaji kutumiwa kwa usahihi kwenye kila tendo la ngono ili kuwa na ufanisi mkubwa.
  • Zinahitaji ushirikiano wa wenza wote wawili mwanaume na mwanamke. Kuzungumza kuhusu matumizi ya kondomu kabla ya tendo kunaweza kuongeza uwezekano kuzitumia.
  • Zinaweza kuondoa hamu ya ngono kwa baadhi ya wanaume. Majadiliano baina ya wenza mara nyingine yanaweza kusaidia kuondoa vikwazo

Kondomu za kiume zinafanyaje Kazi?

Ufanisi unategemea mtumiaji: Hatari ya kupata mimba au magonjwa ya ngono ni kubwa zaidi kama kondomu hazitatumiwa kwa kila tendo la ngono. Mimba au maambukizi machache sana hutokea kutokana na matumizi yasiyo sahihi, kuteleza au kuchanika.

Kinga kuzuia mimba:

  • Kama kawaida ilivyozoeleka, karibu mimba 15 hutokea kwa wanawake 100 ambao wenzi wao wametumia kondomu mwaka wa kwanza. Hii ina maana kuwa wanawake 85 kati ya kila 100 ambao wanaume wao wametumia kondomu hawatapata mimba.
  • Ikitumiwa kwa usahihi kwa kila tendo la ngono, kutakuwa na karibu mimba 2 kwa wanawake 100 ambao wanaume wao wametumia kondomu mwaka wa kwanza.
  • Kurudi kuwa na uwezo wa kuzaa baada ya kuacha kondomu: Bila kuchelewa

Kinga dhidi ya VVU na magonjwa ya ngono:

  • Kondomu za kiume hupunguza kwa kiasi kikubwa hatari ya kuambukizwa VVU kama itatumiwa kwa usahihi kwa kila tendo la ngono.
  • Zikitumiwa wakati wote na kwa usahihi, kondomu huzuia 80% hadi 90% ya maambukizi ya VVU ambayo yangetokea bila kutumia kondomu.
  • Kondomu hupunguza hatari ya kuambukizwa magonjwa mengi yanayoambukizwa kwa ngono kama zitatumika kila wakati na kwa usahihi.
    • Huzuia vizuri magonjwa ya ngono kwa njia ya usaha kama vile VVU, kisonono na klamidia.
    • Pia huzuia magonjwa yanayoambukizwa kwa ngono kwa kugusana ngozi, kama vile hepesi na virusi papiloma (papillomavirus).

Faida Kiafya, na Hatari Kiafya ya kondomu za kiume

Faida Kiafya Zinajulikana

Husaidia kukinga dhidi ya:

  • Hatari ya kupata mimba
  • Magonjwa ya ngono, pamoja na VVU

Zinaweza kukinga kuzuia:

  • Hali zinazosababishwa na magonjwa ya ngono:

Hatari Zinazojulikaa Kiafya

  • Hutokea kwa nadra sana: Mzio mkali (wa mpira miongoni mwa watu) KONDOMU

Kuanzisha Mazungumzo Juu ya Matumizi ya Kondomu za kiume

Baadhi ya wanawake huona ugumu wa kujadili hamu yao ya kutumia kondomu na wenzi wao. Wengine hupata shida ya kuwashawishi wenzi wao kutumia kondomu kila mara wanapofanya ngono. Wanaume hutoa sababu mbalimbali ili wasitumie kondomu. Wengine hawapendi jinsi kondomu zinavyowaondolea hisia ya ngono. Wakati mwingine sababu za wanaume ni za uzushi au kuelewa vibaya. Kuwa na taarifa za kweli kunaweza kumsaidia mwanamke kujibu pingamizi za mwenzi wake

Kuzungumza Kwanza Kunaweza Kusaidia. Mwanamke anayezungumza na mwenzi wake kuhusu kutumia kondomu kabla ya kuanza ngono anaweza kuongeza uwezekano wa kutumia kondomu. Wanawake wanaweza kutumia njia wanazofi kiri kuwa ni bora zaidi, kutegemeana na mwenza na mazingira. Baadhi ya mambo ambayo yamesisitizwa katika mazingira tofauti ni pamoja na:

  • Kusisitiza kutumia kondomu ili kuzuia mimba kuliko ugonjwa wa ngono.
  • Kudai kujaliana – kwa mfano: “Watu wengi kwenye jamii wana maambukizi ya VVU, hivyo inatubidi kuwa makini.”
  • Kuchukua msimamo wa kutokubali – kwa mfano: “Siwezi kufanya nawe ngono mpaka utumie kondomu.”
  • Kupendekeza kujaribu kutumia kondomu ya kike, kama ipo. Baadhi ya wanaume wanapenda zitumike kondomu za kike badala ya za kiume.
  • Kwa wanawake wajawazito, wajadili hatari ambazo zinaletwa na magonjwa ya ngono kwa afya ya mtoto na kusisitiza jinsi kondomu zinavyoweza kumkinga mtoto dhidi ya magonjwa.

Pia, mwanamke anaweza kupendekeza kuwa mwenza wake au kwa pamoja waende kliniki kwa ajili ya kupata ushauri juu ya umuhimu wa kutumia kondomu.

Vigezo vya Kitabibu vya Kuweza Kutumia Kondomu za Kiume

Wanaume wote wanaweza kutumia kwa usalama kondomu za kiume isipokuwa wale wenye:Mzio mkali wa mpira.

Hatua 5 za msingi za kutumia Kondomu za kiume

Hatua za Msingi Taarifa muhimu
1.      Tumia kondomu mpya kwa kila tendo la ngono Kagua paketi ya kondomu. Usiitumie kama imechanika au kuharibika. Epuka kutumia kondomu iliyopitisha muda wake wa kutumiwa – fanya hivyo kama kuna kondomu mpya.
Chana na fungua paketi kwa uangalifu. Usitumie kucha, meno, au kitu chochote kinachoweza kuharibu kondomu.
2.      Kabla ya kugusana kimwili, weka kondomu kwenye ncha ya uume uliosimika sehemu ya kukunjua ikiwa upande wa nje Kwa kinga kamili, vaa kondomu kabla uume haujagusa via vya uzazi, mdomo au mkundu.
3.      Kunjua kondomu mpaka ifunike uume wote Kondomu lazima ikunjuke kwa urahisi. Ukiilazimisha inaweza kupasuka wakati wa kutumia.
Kama kondomu haikunjuki kwa urahisi, inaweza kuwa imegeuzwa, imeharibika au ni ya siku nyingi sana. Itupe kisha tumia kondomu mpya.
Kama kondomu imewekwa kinyume na hakuna nyingine ya kubadili, igeuze na uikunjue kwenye uume.
4.      Mara baada ya kukojoa, shika shingo ya kondomu na chomoa uume wakati ukiwa bado umesimika Chomoa uume.
Telezesha kondomu ukiitoa, ili kuepuka kumwaga manii nje.
Kama unataka kufanya ngono tena au kubadili kutoka tendo moja la ngono hadi jingine, tumia kondomu mpya.
5.      Tupa kondomu iliyotumika mahali salama Fungasha kondomu kwenye paketi yake na itupe kwenye sehemu ya kutupia taka au choo cha shimo. Usitupe kondomu kwenye choo cha kuvuta maji, kwa kuwa inaweza kusababisha kuziba kwa choo.

Vilainisho vya Kondomu za Mpira

Mafuta ya kulainisha husaidia kuepuka kupasuka kwa kondomu. Kuna njia 3 za kutoa vilainisho – vilainisho asilia vinavyotoka ukeni, vilainisho vya ziada, au kutumia kondomu zilizofungashwa na vilainisho.

Wakati mwingine vilainisho vinavyotokana na glycerine au silikoni hupatikana, ambavyo ni salama kutumiwa kwa kondomu za mpira. Maji safi na mate yanaweza pia kutumika kwa ajili ya kulainishia. Vilainisho vipakwe sehemu ya nje ya kondomu, ukeni, au mkunduni. Vilainisho visipakwe kwenye uume kwa kuwa vitasababisha kondomu iteleze na kuchomoka. Tone moja au mawili ya vilainisho yakipakwa ndani ya kondomu kabla ya kukunjuliwa yanaweza kusaidia kuongeza hisia za ngono kwa baadhi ya wanaume. Hata hivyo, vilainisho vikizidi mno ndani ya kondomu vinaweza kusababisha kondomu kuteleza na kuchomoka.

Usitumie bidhaa zilizotengenezwa kwa mafuta kama vilainisho vya kondomu za mpira. Vinaweza kuharibu mpira. Bidhaa ambazo haziruhusiwi kutumika ni pamoja na: mafuta yoyote (mafuta ya kupikia, mafuta ya nazi, mafuta yatokanayo na madini), mafuta ya kujipaka, losheni, malai baridi, siagi, siagi ya kokoa, na majarini.

Watumiaji wa Kondomu Hawatakiwi Kufanya Nini?

Baadhi ya vitendo vinaweza kuongeza hatari ya kupasuka kwa kondomu inafaa viepukwe.

  • Asikunjue kondomu kwanza kisha ajaribu kuiingiza kwenye uume.
  • Asitumie vilainisho vyenye mafuta kwa sababu yanaharibu mpira.
  • Asitumie kondomu kama rangi yake haiko sawa au imebadilika.
  • Asitumie kondomu ambayo ni ngumu, imekauka, au inanata.
  • Asirudie kutumia kondomu iliyokwishatumika.
  • Asifanye ngono kavu.

Pia, asitumie kondomu moja anapobadili kutoka vitendo tofauti vya kupenya katika ngono, kama vile kutoka ngono ya nyuma kwenda mbele. Kwa hali hii anaweza kuhamisha bakteria ambao wanaweza kusababisha maambukizi.

Imani potofu kuhusu kondomu za kiume

Kondomu za kiume:

  • Haziwafanyi wanaume kuwa wagumba, hanithi au dhaifu.
  • Hazipunguzi hamu ya ngono kwa mwanaume.
  • Haziwezi kupotelea ndani ya mwili wa mwanamke.
  • Hazina matundu yanayoweza kupitisha VVU.
  • Hazijawekwa VVU.
  • Hazisababishi ugonjwa kwa mwanamke kwa sababu huzuia manii au mbegu za kiume kuingia mwilini wake.
  • Hazisababishi ugonjwa kwa wanaume kwa sababu mbegu za kiume “hurudi nyuma.”
  • Hutumiwa na wanandoa. Hazikutengenezwa kwa ajili ya kutumia nje ya ndoa tu.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/birthcontrol.html

Leave feedback about this

  • Quality
  • Price
  • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X