Magonjwa ya wanaume

KORODANI AMBAZO HAZIJASHUKA KWENYE PUMBU

Korodani ambazo hazijashuka kwenye pumbu ni nini?

Korodani ambazo hazijashuka kwenye pumbu – Korodani ni moja ya kiungo cha mwili wa mwanamme. Korodani zinatengeneza homoni za kiume na manii. Kwa kawaida korodani zote mbili zinahifahiwa ndani ya pumbu. Wakati mtoto wa kiume anapokua ndani ya mji wa mimba, korodani zake huwa ziko tumboni. Kwa kawaida zinashuka na kuingia kwenye pumbu muda mfupi kabla au baada tu ya kuzaliwa. Korodani ambazo hazijashuka ni zile ambazo zinabakia juu bila kushuka kwenye pumbu.

Korodani ambazo hazijashuka kwenye pumbuKorodani ambazo hazijashuka si kitu cha ajabu kwa Watoto wadogo. Karibia 30% ya wavulana wanaozaliwa wakiwa njiti na 5% ya wanaozaliwa wakiwa wametimiza umri wa kuzalliwa, wanazaliwa na angalau korodani moja ambayo haijashuka. Kama mtoto ana korodani ambayo haijashuka kwenye pumbu, huwa inashuka tu yenyewe baada ya miezi kadhaa ya Maisha yake. Kama hazitashuka baada ya miezi mitatu au minne, anaweza kuhitaji kupatiwa matibabu na daktari.

Nitajuaje kuwa ana korodani ambazo hazijashuka kwenye pumbu?

Daktari anaweza kukuambia kama korodani hazijashuka kwa kukagua pumbu za mtoto. Kama daktari hazisikii baada ya kukagua pumbu, atakuambia kuwa hazisikii hata akikagua pumbu. Kama korodani haijashuka inaweza kuwa imebakia ndani ya tumbo, au ni ndogo sana kiasi kwamba ni ngumu kuisikia au kuna uwezekano kuwa haipo kabisa. Kwa kawaida madaktari wanaweza kuhitaji kufanya upasuaji ili kuhakikisha.

Kwa nini ni muhimu kupata tiba kama una korodani ambazo hazijashuka kwenye pumbu?

Kuna sababu mbili za kupata tiba kama una korodani ambazo hazijashuka kwenye pumbu.

  • Kwanza, korodani ambazo hazijashuka zinaweza zisiweze kutengeneza manii. Korodani zinakaa kwenye pumbu kwa sababu joto la mwili sio kali kama ilivyo kwenye mwili. Utengenezwaji wa manii/shahawa huongezeka zaidi kama joto la mwili sio kali. Uwezo wa kutengeneza manii unaweza kupotea kabisa utotoni kama korodani hazitashuka kwenda kwenye pumbu. Mtoto anaanza kupoteza uwezo wa kutengeneza manii anapokuwa na umri wa miezi 12 tu. Kuzirudisha chini korodani katika miezi ya kwanza ya Maisha ni muhimu ili kubakiza uwezo wa mtoto ya kuzaa atakapokuwa mtu mzima.
  • Sababu ya pili, korodani ambazo hazijashuka kwenye pumbu zina uwezekano zaidi wa kupata saratani ya korodani. kinampata mwanamme mmoja kati ya 2,000 wenye korodani ambazo hazijashuka kwenye pumbu. Kiwango hiki ni kikubwa sana ukilinganisha na wanaume ambao korodani zao zilishuka. Korodani zinapokuwa ndani ya pumbu, mwanamme anaweza kuzisikia kwa kuzishika na anaweza kukagua kama kuna saratania au daktari anaweza kusaidia. Kwa hali hii ya kujikagua , kunaweza kusaidia kupunguza uwezekano wa kansa.

Tiba ya korodani ambazo hazijashuka kwenye pumbu inafanyikaje?

Matibabu kuhusu korodani ambazo hazijashuka kwenye pumbu yanategemea korodani iko mahala gani. Watoto wenye korodani unayoweza kuishika (korodani inayokuwa kwenye sehemu ya juu ya mapaja) kwa kawaida wanafanyiwa upasuaji unaoitwa orchiopexy. Watoto wanaofanyiwa upasuaji huu, kwa kawaida wanaruhusiwa na kwenda nyumbani siku hiyo hiyo. Upasuaji unafanyika kwa kupitia tundu dogo kwenye kinena. Inachukua muda kama wa saa moja. Watoto wengi wanajihisi vizuri tu baada ya muda mfupi.

Aina nyingine ya matibabu ni kupatiwa homoni inayoitwa Hcg. Daktari anaweza kumpatia mtoto wako sindano yenye Hcg. HCG husaidia korodani kutengeneza homoni. Kiwango kikubwa cha homoni za kiume zinaweza kusababisha korodani kushuka kwenye pumbu. Aina hii ya matibabu inafaa sana kama korodani iko karibu na pumbu.

Kama wewe ni mtu mzima na una korodani ambayo haijashuka, kushusha korodani kwenda kwenye pumbu hakutasaidia kuboresha uwezo wa kutengeneza manii. Kwa hiyo kwa wanaume watu wazima, korodani ambayo ilikuwa imebakia juu inaondolewa kabisa ili isilete hatari ya kupata kansa. Madaktari mara nyingi hawafanyi jambo lolote kama una korodani ambayo haijashuka kama una umri wa miaka 40 au zaidi. Kama wewe ni mtu mzima na korodani zako hazijashuka, daktari atakusaidia kufanya maamuzi sahihi.

Angalizo

Taarifa zilizotolewa katika ukurasa huu zimetoa muhtasari na zinaweza zisimfae kila mtu. Ongea na daktari ili kung’amua kama taarifa hizi zinakufaa na wewe au jaribu kutafuta habari zaidi kuhusu shida hii.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/003002.htm

Leave feedback about this

  • Quality
  • Price
  • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X