Other

KUCHOMA SINDANO ZA SUMU YA BOTULINUM – Botox

Kuchoma sindano za sumu ya botulinum kupunguza mikunjo ya ngozi?

Sindano za sumu ya botulinum ni bidhaa zinazotumika kupunguza au kuondoa kabisa mikunjo kwenye ngozi. Kiwango kidogo cha sumu kinachomwa kwenye misuli maalumu ya uso. Sindano hizi husababisha misuli kulegea, na kusababisha mikunjo kuondoka. Baadhi ya majina yanayotumika kutambulisha bidhaa za sumu ya botulinum ni pamoja na Botox, Dysport, na Xeomin.

Ni maeneo gani ya uso yanatibiwa kwa sumu ya botox?

Mikunjo ya sehemu ya mbele ya kipaji cha uso (ndita), na mikunjo inayotokea pembezoni mwa jicho ndiyo maeneo yanayotibiwa zaidi.

Nani ni mtu sahihi anayeweza kutumia sindano za sumu ya botulinum?

  • Watu wenye mikunjo inayokuja na kuondoka (mikunjo inayoonekana misuli inapokaza na kuondoaka inapolegea) ndio hupata matokeo mazuri zaidi.
  • Watu wenye mikunjo isiyoondoka (watu amabo mikunjo inaonekana hata wakati ambao uso umelegea) pia wanapata matokeo, lakini matokeo yanakuja taratibu zaidi.

Ni lini nitaanza kuona matokeo baada ya kuchoma sindano za sumu ya botulinum?

Inachukua muda wa mpaka wiki mbili toka ulipochoma sindano za sumu ya botulinum kuanza kuona matokeo

Matokeo ya sindano za sumu ya botulinum yanadumu kwa muda gani?

Matokeo yanadumu kwa muda wa miezi mitatu mpaka minne. Sindano za sumu ya botulinum zinazofuata zinapendekezwa kutolewa baada ya misuli ya mahali hapo kuanza kukaza na kuweka mikunjo tena,

botoxNijiandae vipi kabla ya kupokea sindano za sumu ya botox?

Haupaswi kumeza dawa ya Aspirin, ibuprofen, au naproxen kwa wiki mbili kabla ya miadi ya kuchomwa sindano ili kupunguza damu kuvia chini ya ngozi. Hakikisha una mtaarifu daktari dawa zozote ulizotumia, zikiwemo dawa za asili na virutubisho mbalimbali unazotumia, kwa sababu hizi nazo zinaweza kuongeza hatari ya kupata ya damu kuvia chini ya ngozi.

Ni mtu wa aina gani hapaswi kuchoma sindano za sumu ya botulinum?

Kama una ujauzito au kama una nyonyesha, haupaswi kuchama sjindano hizi. Kama una ugonjwa wa mfumo wa fahamu na misuli unapaswa pia kutokuchomwa sumu hii. Daktari atakuchunguza ili kutambua kama unafaa kuchomwa sindano za sumu ya botulinum

Ni zipi athari za kuchoma sindano za sumu ya botulinum?

Athari zinatokea mara chache sana, baadhi ni pamoja na kulegea na kushuka chini kwa nyusi na kope za macho (drooping). Dalili zinaweza kuisha zenyewe au zinaweza kuondolewa kwa kuweka matone ya dawa malumu au kuchomwa tena sindano ya sumu ya botulinum kwenye msuli wa karibu.

Kunaweza kukawepo kuvia kwa damu na kuvimba kidogo baada ya kuchomwa sindano. Unaweza kuweka barafu eneo lililovimba au kuvia damu kila baada ya dakika 10 mpaka 15 kwa saa kadhaa mpaka utakapoisha.

sindano za sumu ya botulinumNifanye nini baada ya kuchoma sindano za sumu ya botulinum?

Usilale kwa angalau masaa manne baada ya matibabu. Siku ya kuchoma sindano hizi, usichue (massage) au kuwea joto kwenye ngozi yako, usifanye shughuli zitakazokufaya utokwe jacho jingi (kwa mfano, kunywa pombe, kufanya mazoezi makali, au kuoga maji ya moto sana)

Angalizo

Taarifa zilizotolewa katika ukurasa huu zimetoa muhtasari na zinaweza zisimfae kila mtu. Ongea na daktari ili kung’amua kama taarifa hizi zinakufaa na wewe au jaribu kutafuta habari zaidi kuhusu shida hii.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/botulism.html

Leave feedback about this

  • Quality
  • Price
  • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X