Magonjwa ya wanawake

NAMNA YA KUCHUNGUZA MATITI YAKO MWENYEWE

Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko

Maelezo ya jumla

Kuchunguza matiti yako mwenyewe ni sehemu muhimu ya afya kwa wanawake wengi. Inawasaidia kujua matiti yao yalivyo katika hali ya kawaida, ili kunapotokea mabadiliko, wazungumze na mtoa huduma ya afya mapema.
Hata hivyo, hakuna makubaliano ya pamoja ya wataalamu wa tiba kuhusu kujifanyia uchuguzi wa matiti. Haijulikani kwa uhakika kama zoezi hili la kujifanyia uchunguzi wa matiti linasaidia kugundua kansa au kuokoa maisha. Muulize mtoa huduma ya afya kama unatakiwa kujifanyia uchunguzi wa matiti mwenyewe.

Jinsi ya kuchunguza matiti yako mwenyewe

Kama ukiamua kufanya uchunguzi wa matiti yako mwenyewe, fanya zoezi hili siku 3 – 5 baada ya kuingia kwenye kipindi cha hedhi, wakati ambao matiti yako hayaumi sana na hayana uvimbe. Kama damu yako ya hedhi imekata (menopause), fanya uchunguzi wa matiti kila mwezi katika siku uliyoichagua.  .
Kwanza, lalia mgongo.

  • Weka mkono wa kulia kwenye kisogo cha kichwa chako. Kwa vidole vya mkono wako wa kushoto, bonyabonya taratibu na kukagua titi lote la upande wa kulia.
  • Kisha, ukiwa umekukaa au kusimama, chunguza kwapa lako, hii ni kwa sababu tishu za matiti zimeenea mpaka kwenye kwapa.
  • Minya chuchu polepole ili kuangalia kama kutatoka majimaji.
  • Rudia utaratibu huu kwenye titi la upande wa kushoto pia.

Kuchunguza matiti yako mwenyewe

Wanawake wengi wana viuvimbe kwenye matiti, kwa hiyo usiwe na wasiwasi ukivikuta, lengo la zoezi hili ni kutafuta kitu kilicho kipya, kitu au sehemu ambayo si ya kawaida au tofauti ,na kisha mwone mtoa huduma ya afya kwa tathmini.
Baadhi ya wanawake wanapendelea kufanya zoezi hili wakiwa bafuni wakioga, lakini ni bora zaidi kulifanya ukiwa umejilaza kitandani, inasaidia kuchunguza titi lote.
Kisha, simama mbele ya kioo na uyatazame matiti yako. Ukiwa umeweka mikono yako sawa, angalia kama kuna mabadiliko yoyote kwenye mwonekano wa ngozi ya matiti yako (kudumbukia na kukakamaa kwa ngozi au mwonekano wa ngozi kama ganda la chungwa), umbo, au chuchu kurudi ndani.
Fanya hivyo tena ukiwa umeweka mikono juu ya kichwa chako.
Jadili mabadiliko yoyote uliyoyapata na mtoa huduma ya afya mara moja.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/001993.htm

Leave feedback about this

  • Quality
  • Price
  • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X