Uzazi wa mpango

KUFUNGA KIZAZI MWANAUME (VASEKTOMI)

Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko

Kufunga Kizazi Mwanaume (Vasektomi) ni Nini?

Kufunga kizazi mwanaume (Vasektomi) ni njia ya kudumu ya kuzuia mimba kwa mwanaume ambayo hatahitaji watoto zaidi.

  • Kwa kutumia tundu au mkato mdogo kwenye korodani, mtoa huduma ataitafuta mirija miwili ambayo hubeba mbegu za kiume kwenda kwenye uume (vas deferens) na kuikata au kuiziba na kuifunga au kuichoma kwa umeme (cautery).
  • Pia inakulikana kama njia ya kufunga kizazi kwa mwanaume au kufunga kizazi mwanaume kwa upasuaji.
  • Hufanya kazi kwa kufunga kila mrija, kuzuia mbegu za kiume zisiingie kwenye manii. Manii yanaweza kutoka lakini hayasababishi kupata mimba.

Mambo Muhimu kuhusu kufunga kizazi mwanaume (Vasektomi)

  • Imekusudiwa kutoa kinga ya maisha yote, ya kudumu, na inayofanya kazi vizuri sana kuzuia mimba. Kwa kawaida, hauwezi kufungua kizazi baada ya kukifunga.
  • Inajumuisha utaratibu salama, rahisi wa upasuaji.
  • Huchelewa kufanya kazi kwa miezi 3. Mwanaume au wanandoa lazima watumie kondomu au njia nyingine ya uzazi wa mpango kwa miezi 3 baada ya vasektomi. La sivyo, watasababisha ujauzito.
  • Haiathiri uwezo wa mwanaume kufanya ngonoVasektomi

Kufunga kizazi mwanaume (Vaskektomi) ina Ufanisi Kiasi Gani?

Moja ya njia zenye ufanisi zaidi lakini ina hatari kidogo ya kushindwa kufanya kazi:

  • Inapokuwa wanaume hawawezi kufanyiwa uchunguzi wa manii kwa miezi 3 baada ya upasuaji ili kuona kama bado yana mbegu za kiume, viwango vya ujauzito vitakuwa karibu mimba 2 hadi 3 kwa wanawake 100 katika mwaka wa kwanza baada ya mwanaume kufanyiwa vasektomi. Hii ina maana kuwa wanawake 97 hadi 98 katika kila wanawake 100 ambao wenza wao wamefanyiwa vasektomi hawatapata mimba.
  • Vasektomi haifanyi kazi kikamilifu kwa miezi 3 baada ya kufanyiwa upasuaji.
    • Baadhi mimba hutokea ndani ya mwaka wa kwanza kwa sababu wenza hawa hawatumii kondomu au njia nyingine inayofaa wakati wote na kwa usahihi katika miezi 3 ya kwanza, kabla vasektomi haijaanza kufanya kazi kikamilifu.
  • Hatari kidogo ya kupata mimba inabakia baada ya mwaka wa kwanza baada ya kufanyiwa vasektomi na mpaka mwenza wa kike anapofikia kukoma hedhi.
    • Katika miaka mitatu ya kutumia: Kuna uwezekano wa kutokea karibu mimba 4 kwa wanawake 100.
  • Kama mwenza wa mwanaume aliyefanyiwa vasektomi akipata mimba, inaweza kuwa kwa sababu:
    • Wenza hawa hawakutumia njia nyingine za kuzuia mimba kila wakati katika miezi 3 ya mwanzo baada ya upasuaji.
    • Mtoa huduma alifanya makosa.
    • Sehemu zilizokatwa za vasi difarensi zimekuongezeka na kuungana.

Uwezo wa kuzalisha haurudi kwa sababu vasektomi kwa ujumla haiwezi kufunguliwa au kubadilishwa. Kitendo hiki kimekukusudiwa kiwe cha kudumu. Upasuaji wa kurekebisha ni mgumu, ghali, na hauwezi kufanyika katika maeneo mengi. Ukifanyika, upasuaji wa kurekebisha mara nyingi hausababishi kuweza kuzalisha

Matatizo yanayoweza kutokea baada ya kufunga kizazi mwanaume

  • Yasiyo kawaida na hutokea kwa nadra: Maumivu makali ya korodani au pumbu ambayo huendelea kwa miezi au miaka kadhaa.
  • Yasiyo kawaida na hutokea kwa nadra sana: Maambukizi mahali palipopasuliwa (hutokea kwa nadra kutokana na mbinu za kisasa za upasuaji; hutokea kwa nadra bila kutumia kisu kidogo cha kupasulia.
  • Nadra: Kutokwa damu chini ya ngozi ambako kunaweza kusababisha uvimbe au damu kuvilia (hematoma).

Nani Anaweza Kufanyiwa Vasektomi

Kwa ushauri sahihi na kuthibitisha kuelewa, mwanaume yeyote anaweza kufanyiwa vasektomi kwa usalama, ikijumuisha wanaume ambao:

  • Hawana watoto au wanao wachache
  • Hawajaoa
  • Hawakupata ruhusu toka kwa wake zao
  • Vijana
  • Wana ugonjwa wa seli mundu
  • Wako kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi ya VVU au ugonjwa mwingine unaoambukizwa kwa ngono
  • Wameambukizwa VVU, kama wanatumia au hawatumii dawa za kupunguza makali ya UKIMWI

Katika baadhi ya hali hizi, ushauri makini hasa ni muhimu ili kuhakikisha kuwa mwanaume hatajutia uamuzi wake.Kufunga kizazi mwanaume

Wanaume wanaweza kufanyiwa vasektomi:

  • Bila kufanyiwa vipimo vya damu au maabara.
  • Bila kupima shinikizo la damu.
  • Bila kupima wingi wa damu au hemoglobini.
  • Bila kupima kolesteroli au ini linavyofanya kazi.
  • Hata kama manii hayawezi kupimwa na darubini baadaye ili kuona kama yana mbegu za kiume.

Mambo 6 ya kufahamu kabla ya kutoa Taarifa ya Kukubali kufunga uzazi

Ushauri lazima ujumuishe mambo yote 6 ya taarifa ya kukubali. Kwa baadhi ya programu mteja na mshauri pia hutia saini kupewa taarifa ya kukubali. Ili kueleza kukubali kufunga kizazi, mteja lazima aelewe mambo yafuatayo:

  1. Njia za kuzuia mimba kwa muda pia zinapatikana kwa mteja.
  2. Kufunga kizazi kwa hiari ni njia ya upasuaji.
  3. Kuna hatari kiasi fulani ya upasuaji na vilevile faida. (Hatari na faida zote lazima zielezwe kwa njia ambayo mteja ataelewa).
  4. Kama ukifanyika vizuri, upasuaji utamfanya mteja asiweze kupata watoto tena.
  5. Upasuaji huu unachukuliwa kuwa wa kudumu na hauwezi kubadilishwa.
  6. Mteja anaweza kuamua kubadili mawazo kukataa kufungwa kizazi wakati wowote kabla ya kufanyiwa upasuaji (bila kupoteza haki ya huduma nyingine za tiba, afya, au manufaa mengine).

Kufanya Upasuaji wa kufunga kizazi mwanaume (Vasektomi)

Mwanaume ambaye amechagua kufanyiwa vasektomi anahitaji kujua kutatokea nini wakati wa kufanyiwa vasektomi. Maelezo yafuatayo yanaweza kusaidia kumweleza utaratibu

  1. Mtoa huduma atatumia taratibu sahihi za kuzuia maambukizi wakati wote
  2. Mwanaume atachomwa sindano ya ganzi ya eneo la upasuaji kwenye korodani zake ili kuzuia maumivu. Wakati wote wa kufanyiwa vasektomi atakuwa macho.
  3. Mtoa huduma aguse ngozi ya korodani ili kutafuta kila moja ya mirija – mirija miwili iliyo kwenye korodani inayobeba mbegu za kiume.
  4. Mtoa huduma atoboe au kupasua ndani ya ngozi:
    • Kwa kutumia njia isiyo ya upasuaji, mtoa huduma ashike mrija kwa kutumia koleo maalum na kutoboa kitundu kidogo kwenye ngozi katikati ya korodani kwa kutumia kifaa kikali cha upasuaji.
    • Kwa kutumia utaratibu uliozoeleka, mtoa huduma atapasua sehemu 1 au 2 ndogo kwenye ngozi kwa kutumia kisu kidogo cha kupasulia.
  1. Mtoa huduma atavuta nje kila mrija kupitia sehemu iliyopasuliwa au kutobolewa. Watoa huduma wengi hukata kila mrija na kufunga mwisho mmoja au yote miwili kwa kutumia uzi. Baadhi huziba mirija kwa umeme. Pia wanaweza kufunga mwisho mmoja kati ya mirija kwa tabaka jembamba la tishu inayozunguka mrija.
  2. Tundu litazibwa kwa bendeji, au sehemu ya upasuaji inaweza kushonwa kwa nyuzi.
  3. Mwanaume huyo apatiwe maelekezo kuwa afanye nini baada ya kuondoka kliniki au hospitali. Mtu huyo anaweza kujisikia hali ya kupoteza fahamu kwa muda baada ya vasektomi. Kwanza asimame kwa kusaidiwa, na apumzike kwa dakika 15 hadi 30. Kawaida anaweza kuondoka ndani ya saa moja.Kufunga kizazi mwanaume

Imani potofu kwenye jamii kuhusu kufuga uzazi mwanaume

Upasuaji wa Vasektomi:

  • Haufanyiki kwa kuondoa korodani. Katika vasektomi mirija inayobeba mbegu za kiume huzibwa. Korodani hubakia kama zilivyo.
  • Haipunguzi hamu ya ngono.
  • Haiathiri uwezo wa kufanya ngono. Uwezo wa mwanaume kudisa haupungui, huendelea kwa muda mrefu, na kumwaga manii kama ilivyokuwa awali.
  • Haisababishi mwanaume anenepe au awe dhaifu, awe na nguvu kidogo au uwezo mdogo wa kuzalisha.
  • Haisababishi ugonjwa wowote baadaye maishani.
  • Haizuii maambukizi ya magonjwa ya ngono pamoja na VVU.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/birthcontrol.html

Leave feedback about this

  • Quality
  • Price
  • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X