Uzazi wa mpango

KUFUNGA KIZAZI MWANAMKE

Nini Maana Kufunga Kizazi Mwanamke?

Kufunga kizazi mwanamke ni njia ya kudumu ya kuzuia mimba kwa wanawake ambao hawahitaji kupata watoto tena.

  • Kuna njia 2 za upasuaji zinazotumika zaidi:
    • Upasuaji ujulikanao kama “minilaparatomy” unaofanyika kwa kufanya upasuaji mdogo kwenye fumbatio. Mirija ya falopio huvutwa kupitia kwenye sehemu iliyopasuliwa na kukatwa au kuzibwa.
    • Laparoskopi inajumuisha kuingiza neli ndefu nyembamba yenye lensi kupitia mkato mdogo kwenye ukuta wa fumbatio.
  • Pia inajulikana kwa Kiingereza kama “tubal sterilization, tubal ligation, voluntary surgical contraception, tubectomy, bi-tubal ligation, tying the tubes na the operation.
  • Hufanya kazi kwa sababu mirija ya falopio imezibwa au kukatwa. Mayai yanayopevuka na kuachiwa kwenye ovari hayawezi kutoka kupitia kwenye mirija, na hivyo hayakutani na mbegu za kiume.

Mambo Muhimu Kuhusu kufunga kizazi mwanamke

  • Kudumu. Kimekusudiwa kutoa kinga ya muda mrefu, ya kudumu, na inayofanya kazi vizuri kuzuia mimba. Kurudisha uwezo wa kupata watoto baada ya kufunga kizazi kawaida haiwezekani.
  • Inajumuisha uchunguzi wa mwili na upasuaji. Shughuli hii hufanywa na mtoa huduma mwenye utaalamu wa kutosha.
  • Haina madhara ya muda mrefu.

Kufunga kizazi mwanamke kuna Ufanisi Kiasi Gani?

Ni moja ya njia zenye ufanisi sana lakini ina hatari kidogo ya kushindwa kufanya kazi:

  • Chini ya mimba 1 hutokea kwa wanawake 100 kwa mwaka wa kwanza baada ya kufanyiwa upasuaji wa kufunga kizazi (5 kwa 1,000). Hii ina maana kuwa wanawake 995 kati ya kila 1,000 wanaotegemea kufunga kizazi hawatapata mimba
  • Uwezo wa kushika mimba haurudi kwa sababu kawaida haiwezekani kuzuia au kubadili ufungaji wa kizazi baada ya kufanyika. Ufungaji wa kizazi umekusudiwa kuwa wa kudumu. Upasuaji wa kurejesha uwezo wa kushika mimba ni mgumu, ghali, na hauwezi kufanyika katika maeneo mengi. Ukifanyika, upasuaji huu mara nyingi hausaidii kupata mimbakufunga kizazi mwanamke

Faida Kiafya, Hatari Kiafya, na Matatizo

Faida Kiafya Zinazojulikana

  • Husaidia kukinga dhidi ya: Hatari ya kupata mimba na Ugonjwa wa uvimbe wa nyonga
  • Inaweza kukinga dhidi ya: Saratani ya ovari

Hatari Kiafya Zinazojulikana

  • Hazijulikani;; kama zipo hutokea kwa nadra sana: Matatizo ya upasuaji na dawa za nusu kaputi

Matatizo ya upasuaji

Hutokea kwa nadra sana:

  • Kufunga kizazi mwanamke ni njia salama ya kuzuia mimba. Hata hivyo, inahitaji kufanya upasuaji kwa kutumia ganzi, ambayo inaleta hatari fulani ya kupata maambukizi au kidonda kupata usaha.

Hatari ya kupata matatizo yatokanayo na ganzi ni ndogo sana. Matatizo yanaweza kupunguzwa kama mbinu sahihi zitatumika na kama upasuaji utafanyika mahali sahihi.

Nani Anaweza Kufungwa Kizazi

Ni salama kwa wanawake wote. Ukifanyika ushauri sahihi na mwanamke kueleza kukubali wake, anaweza kufungwa kizazi kwa usalama, ikiwa ni pamoja na wanawake ambao:

  • Hawana watoto au wana watoto wachache
  • Hawajaolewa
  • Hawajapata ruhusa ya mume
  • Vijana
  • Wamejifungua muda si mrefu (angalau ndani ya siku 7)
  • Ananyonyesha
  • Wameambukizwa VVU, kama wanatumia au hawatumii vidonge vya kupunguza makali ya UKIMWI

Katika baadhi ya hali hizi, ushauri makini ni muhimu hasa ili kuhakikisha mwanamke hatajutia kuchukua uamuzi wake.

Wanawake wanaweza kufungwa kizazi:

  • Bila kupima damu au vipimo vyovyote vya maabara
  • Bila kuchunguzwa saratani ya kizazi
  • Hata kama mwanamke hapati hedhi wakati huo, kama kutakuwa na uhakika wa kutosha kuwa hana mimba

Mambo muhimu ya kufikiri kabla ya kufunga kizazi mwanamke

Mwanamke au mwanaume anayeamua kufunga kizazi afikiri kwa makini kwa makini na kujiuliza:

  • “Je unataka kupata watoto siku za baadae?”
  • “Kama hapana, je unafikiri utabadili mawazo baadaye?
  • Jambo gani linaweza kubadili mawazo yako? Kwa mfano, kama ikitokea mmoja wa watoto wako akafariki?”
  • “Kama ikitokea kumpoteza mwenza wako, na ukaolewa tena?”
  • “Je mwenza wako anahitaji watoto zaidi siku za baadae?”

Kama utashindwa kujibu maswali haya kwa uhakika, tunashauri uendelee kufikiri zaidi kuhusu maamuzi yako ya kufunga kizazi.

Kwa ujumla, watu wanaoweza kujutia kufunga kizazi:

  • Ni vijana
  • Wenye watoto wachache au hawana watoto
  • Waliofiwa na mtoto
  • Hawajaolewa
  • Walio na matatizo ya ndoa
  • Walio na wenza wanaopinga kufunga kizazi

Kufanya Utaratibu wa Kufunga Kizazi mwanamke

Mwanamke ambaye amechagua kufunga kizazi anahitaji kujua kutatokea nini wakati wa kufunga kizazi. Maelezo yafuatayo yanaweza kusaidia kumfafanulia mchakato huo

Upasuaji Mdogo wa Fumbatio (Minilaparatomy)

  1. Mtoa huduma hutumia taratibu sahihi za kuzuia maambukizi wakati wote.
  2. Mtoa huduma afanye uchunguzi wa mwili na uchunguzi wa nyonga. Uchunguzi wa nyonga hufanyika kuchunguza hali na kusogea kwa kizazi (uterasi).
  3. Kwa kawaida mwanamke hupewa dawa kidogo ya kutuliza maumivu (ya vidonge au kuchomwa kwenye mshipa) ili kumfanya atulie. Atabaki kuwa macho. Atachomwa ganzi eneo la upasuaji juu ya kinena.
  4. Mtoa huduma atafanya upasuaji wa wima (sentimita 2 – 5) katika eneo lililochomwa ganzi. Kwa kawaida hii husababisha maumivu kidogo. (Kwa wanawake ambao ndiyo kwanza wamejifungua, upasuaji hufanyika kwa mlalo chini ya kitovu).
  5. Mtoa huduma ataingiza kifaa maalum (uterine elevator) ukeni, kupitia kwenye shingo ya mji wa mimba (seviksi), hadi kwenye kizazi (uterasi) ili kuinyanyua mirija miwili ya falopio ili kuileta karibu na sehemu iliyopasuliwa. Hii inaweza kusababisha kujisikia vibaya.
  6. Kila mrija utafungwa na kukatwa.
  7. Mtoa huduma atafunga sehemu iliyopasuliwa kwa nyuzi na kufunika kwa bendeji.

Upasuaji wa Laparaskopi

  1. Mtoa huduma atatumia utaratibu sahihi wa kuzuia maambukizi.
  2. Kwa kawaida mwanamke hupewa dawa kidogo ya kutuliza maumivu (ya vidonge au kuchomwa kwenye mshipa) ili kumfanya atulie. Atachomwa ganzi eneo la upasuaji chini ya kitovu.
  3. Mtoa huduma ataingiza sindano maalum ndani ya fumbatio la mwanamke na, kupitia sindano, hujaza fumbato gesi au hewa. Hii hunyanyua ukuta wa fumbatio kuachanisha na nyonga.
  4. Mtoa huduma atapasua sehemu ndogo (karibu sentimita moja) kwenye eneo lililotiwa ganzi na kuingiza laparaskopi. Laparaskopi ni mrija mrefu wenye kamera inayosaidia kuona ndani ya mwili.
  5. Mtoa huduma ataingiza kifaa kupitia laparaskopi (au, wakati mwingine, kupitia sehemu ya pili iliyopasuliwa) kuziba nmishipa ya falopio.
  6. Kila mshipa ufungwe kwa kibanio au pete, au kwa kuchomwa na kifaa cha umeme.
  7. Kisha mtoa huduma ataondoa kifaa na laparaskopi. Gesi au hewa inaachiwa kutoka nje ya fumbatio la mwanamke. Mtoa huduma atafunga sehemu iliyopasuliwa kwa kutumia nyuzi na kuifunika kwa bendeji.

Imani potofu zilizopo kwenye jamii

Kufunga kizazi mwanamke:

  • Hakumfanyi mwanamke awe na udhaifu.
  • Hausababishi maumivu ya muda mrefu ya mgongo, uterasi, au fumbatio.
  • Hauondoi kizazi cha mwanamke au kusababisha haja ya kukiondoa.
  • Hausababishi matatizo ya vichocheo.
  • Hausababishi kupata hedhi ya damu nyingi au hedhi isiyotabirika au vinginevyo kubadili mzunguko wa hedhi ya mwanamke.
  • Hausababishi mabadiliko yoyote ya uzito, hamu ya kula, au mwonekano.
  • Haubadili mwenendo au hamu ya ngono kwa mwanamke.
  • Kwa kiasi fulani husababisha hatari ya mimba kutunga nje ya kizazi.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/birthcontrol.html

    • 5 months ago (Edit)

    Mke wangu kafanyiwa huo utaratibu lakini sahv ana mwezi wa pili hajaona siku zake na sahv tumbo linavuta je nini. Ameenda hospital wanasema tuangalie kwa siku 21. Je kunauwezekano wowote kuwa kapokea mimba

      • 5 months ago

      hii ni ngumu kidogo kufahamu, kama umeonana na daktari. fuata ushauri aliokuptaia. polee sana

Leave feedback about this

  • Quality
  • Price
  • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X