KUHARA BAADA YA KULA CHAKULA KILICHOHARIBIKA

KUHARA BAADA YA KULA CHAKULA KILICHOHARIBIKA

 • February 20, 2021
 • 0 Likes
 • 109 Views
 • 0 Comments

Maelezo ya jumla

Matukio mengi ya kuhara baada ya kula chakula kilichoharibika au kichafu, husababishwa na usafi duni wakati wa kuandaa, mapishi na utunzaji wa chakula. Kwa sababu ya mazingira haya ya uchafu, inaruhusu bakteria na virusi kuzaliana na kuharibu chakula. Vyakula vinavyoharibika kwa urahisi ni samaki, maziwa, mayai ambayo hayajapikwa vizuri na nyama ya ndege. Dalili za tatizo hili ni pamoja na kichefuchefu, kutapika, kuhara na maumivu ya tumbo, na wakati mwingine unaweza kuwa na homa, maumivu ya kichwa au kizunguzungu.

Mwone daktari haraka kama

Ni vizuri kutafuta usaidizi wa kitabibu haraka sana kama:

 • Kama unaona maluweluwe au unaona misuli ya mwili inalegea baada ya kula chakula kilichochafuliwa

Panga kumwona daktari kama:

 • Una maumivu makali sana ya tumbo na unatapika
 • Kuna damu au kamasikamasi kwenye kinyesi

Unachoweza kufanya wewe mwenyewe

Unaweza kujitibu mwenyewe kama hali ni ya kawaida baada kuhara baada ya kula chakula kilichoharibika / kichafu kwa kufuata utaratibu ufuatao. Utajisikia vizuri kabisa baada ya siku 1 au 2 baada ya kufanya mambo yafuatayo

 • Pumzika, jipatie muda wa kupumzika ili kurejesha nguvu na afya mwilini
 • Kunywa angalau glass 8 za maji kwa siku. Piga pafu ndogondogo ili usitapike. Kama ni muhimu, unaweza kunywa mchanganyiko maalumu wa kurejesha chumvichumvi inayopotea unapotapika au kuhara ‘’Oral rehydration solution [ORS]’’
  • Mchanganyiko huu hurejesha chumvi, sukari na madini yanayopotea kutoka mwilini. Unaweza kununua pakiti kutoka duka la dawa, unaweza kuichanganya na maji au na kinywaji kingine unachopendelea.
 • Mara tu ukiweza kula, vyakula vyepesi, laini na visivyo na nyuzinyuzi nyingi, kama vile mayai ya kuchemsha, tambi au viazi mviringo vilivyopikwa. Anza kula kidogokidogo, na kisha anza kurudi kwenye mlo wa kawaida baada kuweza kulavyakula hivi vizuri. Epuka kunywa chai, kahawa, bidhaa za maziwa, pombe na vyakula vyenye mafuta, viungo na pilipili nyingi mpaka siku kadhaa baada ya kuacha kuhara.
 • Kuwa makini na usafi ili usiwambukize wengine. Nawa mikono vizuri kila baada ya kutoka chooni na tumia taulo yako mwenyewe. Usipike chakula kwa ajili ya watu wengine na ikiwezekana usichangie vyombo, vikombe na sahani. Kaa mbali nawatu ambao unajua wako kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa, kama vile watoto, wazee na wanawake wajawazito.
 • Unaweza kutumia madawa ya kuzuia kuharisha kama unataka kuacha kuhara haraka. Dawa hizi unatakiwa kuzitumia pale tu inapobidi na kama hakuna njia nyingine, kwa sababu kuhara ni njia ya mwili kuondoa na kuafisha maamubukizi kutoka tumboni. Unaweza kutumia ‘’Loperamide’’ kuzuia kuhara kama unaona unaweza kuaibika, kwa mfano, kazini.

Kuzuia

Ili kulinda chakula kisichafuliwe na vimelea, fuata mbinu zifuatazo ili kuepuka kuharisha baada ya kula chakula kichafu

 • Kabla ya kuandaa chakua, nawa mikono vizuri kwa maji ya uvuguvugu na sabuni, na kisha ikaushe kwa taulo safi
 • Tenga vyakula ambavyo havijapikwa na vilivyopikwa. Tunza nyama ambayo haijapikwa kwenye eneo la chini kabisa kwenye jokofu ‘’fridge’’ ili kuepuka majimaji yake kudondokea chakula kingine.
 • Tumia vibao tofauti tofauti vya kukatia unapokuwa unakata nyama mbichi, nyama iliyopikwa au mbogamboga. Safisha vibao vya kukatia chakula vizuri baada ya kuvitumia
 • Pika chakula kiive vizuri, hasa nyama, samaki au mayai
 • Unapokuwa unapasha chakula, hakikisha kimepashwa na kuwa na moto wa kutosha kuua vimelea. Usipashe chakula zaidi ya mara 1.

Mwone daktari kama

Panga kuonana na daktari kama una tatizo la kuhara baada ya kula chakula kilichoharibika na unaona dalili zinaendelea kuwa mbaya zaidi au kama hazijaondoka baada ya masaa 28 -48.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/001652.htm

 • Share:

Leave Your Comment