Maelezo ya jumla
Kujisikia vibaya baada ya kulewa pombe ni matokeo ya kunywa pombe nyingi, lakini kuna baadhi ya watu wanapata hangover baada ya kunywa hata kidogo tu. Sababu ya hangaover baada ya kunywa pombe huwa inasababishwa na upungufu wa maji mwilini unaosababishwa na pombe, kemikali na viungo vingine vinavyowekwa kwenye vinywaji, hasa vinywaji vyenye rangi nzito kama red wine, brandy, port na sherry. Unaweza kuhisi kichwa kinakuuma, kichefuchefu, kizunguzungu, midomo huwa inakauka na kuhisi kiu kikali sana ambacho kinaweza kusababisha usilale usiku. Watu wengu huwa wanajihisi vizuri tu baada ya kufanya mambo fulani yanayowasaidia.
kujisikia vibaya baada ya kulewa pombe – ufanyeje?
Kama unajiona umekunywa sana, fanya mambo yafuatayo ili kupunguza kujisikia vibaya baada ya kulewa pombe baadae. Mara nyingi karibu dalili zote huwa zimepoa baada ya masaa 24
- Kunywa vinywaji ambavyo havina pombe kwa wingi sana kabla ya kwenda kulala na baada tu ya kuamka ili kupunguza uwezekano wa mwili kuishiwa maji. Ni vizuri ukaweka glass ya maji karibu na kitanda chako ili kama ukiamka usiku unywe. Juisi za matunda ambazo zina-contain kiwango kikubwa cha sukari aina ya fructose zinasaidia mwili wako kuiondoa haraka pombe mwilini. Kunywa juisi kwa wingi na Sali kama ipo. Kula machungwa au juisi ya machungwa itasaidia kupunguza shida yako mapema iwezekanavyo
- Usinywe chai au kahawa, kw sababu zinachachawisha tumbo na zinaongeza uwezekano wa maji kupungua mwilini
- Kama unaweza, kula. Kula haa ndazi tu itasaidia kuongeza sukari mwilini mwako
- Unaweza pia kutumia dawa za kupunguza maumivu ili kutuliza maumivu ya kichwa. Madawa kama ibuprofen au acetaminophen zinasaidia kupooza maumivu ya kichwa.
- Unaweza kutumia dawa ya kupunguza asidi tumboni (antiacid) ili kupunguza kichefuchefu. Anti-acid zinafanya kazi kwa ku-neutralize asidi tumboni ambazo zinachangia kusababisha kichefuchefu. Kuna antiacid ambazo unaweza kunywa, zingine zinakuwa kama kidonge ambacho utapaswa kumeza au kidonge unachopaswa kutafuna, so, hakikisha unatafuna vizuri ili vifanye kazi haraka na kwa ufasaha.
- Usinywe pombe zaidi ili kupunguza dalili zako za hangover – kujisikia vibaya baada ya kulewa pombe, ukifanya hivi , dalili zako zitazidi kuwepo kwa muda mrefu zaidi
- Pumzika mpaka utakapoanza kujihisi vizuri tena
- Usiendeshe gari pia, pombe huwa inabaki mwilini kwa muda mrefu, reflex zako zinaweza kuwa bado hazijarudi vizuri siku moja baada ya kunywa
Unaweza kufanya mambo yafuatayo ili kupunguza uwezekano wa kujisikia vibaya baada ya kulewa pombe
- Kula kwanza kabla ya kunywa pombe
- Jaribu kuchanganya pombe na vinywaji vingine laini
Ni vizuri kuomba ushauri wa daktari kama utaona mambo yafuatayo
- Unapatwa na hangover mara kwa mara na unapata shida kujizuia au kupunguza unywaji wako wa pombe
- Kama unapata hamu kali ya kunywa pombe wakati wa asubuhi
Leave feedback about this