KUKATWA MGUU: Sababu, maandalizi, matarajio

Maelezo ya jumla

Kukatwa mguu ni hali ya kukata na kuondoa mguu, kanyagio au vidole kutoka mwilini.

Kukatwa mguu kunafanyikaje?

Kukatwa mguu kunafanyika wakati wa upasuaji au wakati wa ajali au jeraha mwilini.

Ni nani anahitahika kukatwa mguu?kukatwa mguu

Sababu za kukatwa mguu ni pamoja na:

 • Jeraha baya la mguu lililotokea wakati wa ajali
 • Mtiririko wa damu kwenda kwenye mguu ulioathirika
 • Maambukizi kwenye mguu yanayoendelea japo unapata matibabu
 • Saratani kwenye mguu
 • Jeraha baya la moto kwenye mguu
 • Vidonda vikubwa visivyopona vinavyotokana na baridi kali

Ni zipi hatari zinazoletwa na kukatwa mguu?

Hatari zinazoletwa na upasuaji wowote ni pamoja na:

 • Mabonge ya damu yaliyoganda yanaweza kusafiri kutoka kwenye mguu mpaka kwenye mapafu na kusababisha matatizo ya upumuaji
 • Kuvuja damu

Hatari zinazoletwa na aina hii ya upasuaji ni pamoja na:

 • Kuendelea kujisikia/kuhisi kuwa bado mguu upo – hii huitwa “phantom sensation”
 • Kuendelea kujisikia/kuhisi maumivu kwenye mguu japo umeshakatwa – hii hujulikana kama “phantom pain”
 • Maungio yaliyo karibu na sehemu mguu ulipokatiwa yanapoteza uwezo wa kujongea vizuri – inakuwa ngumu kuijongesha
 • Maambukizi ya ngozi au mfupa
 • Kidonda cha mahala mguu ulipokatiwa hakiponi vizuri

Ni nini cha kutarajia kabla ya kukatwa mguu?kukatwa mguu

Kama daktari amepanga siku ya kukatwa mguu, unaweza kuombwa kufanya mambo fulani ili kujiandaa. Hakikisha unamwambia daktari au nesi kuhusu:

 • Dawa zozote unazotumia, hata dawa au dawa za asili ulizokuja nazo bila cheti cha daktari
 • Kama umekuwa unakunywa pombe nyingi sana
 • Siku chache kabla ya upasuaji utaombwa kuacha kutumia dawa ya aspirin, ibuprofen, warfarin, na dawa nyingine zinazosababisha iwe ngumu damu kuganda.
 • Muulize daktari ni dawa gani unapaswa kuendelea kutumia siku ya upasuaji
 • Kama unavuta sigara, ACHA
 • Kama una ugonjwa wa kisukari, endelea kupata mlo wako na dawa kama ilivyo kawaida mpaka siku ya upasuaji
 • Kufika siku ya upasuaji, utaombwa usile wala kunywa kitu chochote kwa masaa 8 mpaka 12
 • Tumia dawa ulizoruhusiwa na daktari kutumia kwa kunywa kwa pafu ndogo ya maji.
 • Kama una ugonjwa wa kisukari, fuata maelekezo uliyopewa na daktari
 • Andaa nyumba yako kabla ya upasuaji:
  • Je, ni usaidizi kiasi gani utahitaji baada ya kurudi kutoka hospitalini?
  • Je, una mwanafamilia, rafiki, au jirani anayeweza kukusaidia?
  • Je, choo an bafu zilizo nyumbani kwako ni salama kwako?
  • Je, utaweza kuingia na kutoka nyumbani mwako salama?

Ni nini cha kutarajia baada ya utaratibu huu?

Mazoezi
Mazoezi na mguu mpya

Baada ya utaratibu wa kukatwa mguu kukamilika, mwisho wa mguu, sehemu ulipokatiwa patafungwa bandeji na kubakia hapo kwa siku 3 au zaidi. Unaweza kuhisi maumivu kwa siku chache za mwanzo. Utaendelea kumeza dawa za maumivu kadri unavyozihitaji.

Unaweza kuwekewa mrija utakaokuwa unatoa majimaji kutoka kwenye kidonda. Mrija huu utaondolewa baada ya siku chache.

Kabla ya kuondoka hospitalini utaanza kujifunza jinsi ya:

 • Kutumia kiti cha magurudumu au fimbo/magongo ya kutembelea
 • Kunyoosha misuli ili kuifanya imara
 • Kuimarisha mikono na miguu
 • Kuanza kutembea kwa kutumia visaidizi kujongea ndani ya chumba cha hospitali, kitandani, kwenye kiti
 • Kujongesha viungo vya mwili, kukaa au kulala katika mikao tofauti ili viungo visikakamae
 • Kudhibiti uvimbe kwenye sehemu mguu ulipokatwa
 • Kuutumia vizuri mguu uliobakia – utaambiwa ni uzito kiasi gani unapswa kubeba mguu uliobakia
 • Unaweza usiruhusiwe kuutumia mguu uliokatwa mpaka utakapopona vizuri
 • Kuweka mguu bandia ulitengenezewa – hii itawezekana baada ya kupona vizuri sehemu mguu ulipokatiwa

Matarajio

Kupona na kuendelea na shughuli za kila siku kunategemea mambo mengi. Baadhi ya mambo haya yanaweza kuwa ndio sababu ya kukatwa mguu, kama una ugonjwa kisukari au kama una mzunguko mbovu wa damu, na umri.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/limbloss.html

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi