Maelezo ya jumla
Kukaza au maumivu ya shingo, mara nyingi yanatokana na kukaza kwa misuli ya shingo kunakotokana na mkao mbaya au jeraha dogo. Unaweza kuwa na tatizo la kukaza au maumivu ya shingo na mabega kama ukikaa unajikuja kuinamia kompyuta kwa muda mrefu.
Unaweza pia kuwa na maumivua au kukaza kwa shingo kama ulilala vibaya wakati wa usiku. Unaweza pia kuhisi maumivu kichwani, kwenye mabega, mikono au hata sehemu ya juu ya mgongo na maumivu yanaweza kuzidi ukigeuza kichwa, ukiangalia juu au chini. Unaweza pia kuwa na maumivu au mkazo wa shingo kama umeumia kwa kutupa kwa nguvu shingo‘’whiplash injury’’ hasa kwenye ajali, au kama una ugonjwa wa yabisi kavu kwenye uti wa mgongo au kama una ugonjwa mwingine au umeumia shingo.
Maumivu ya shingo-mwone daktari kama
Ni vizuri kumwona daktari akushauri
- Kama una tatizo la kukaza au maumivu ya shingo na una moja au nyingi ya dalili zifuatazo pia; Homa, kutapika, maumivu ya kichwa, macho kuumia ukiuangalia mwanga na upele
- Kama kukaza au maumivu ya shingo baada ya kuumia au ajali
- Kama unahisi mkono unapata ganzi, kuwashwa au kulegea/kupungua nguvu au uwezo na kupungua uzito wa mwili
Unachoweza kufanya mwenyewe ukiwa na kukaza au maumivu ya shingo
Tatizo la kukaza au maumivu ya shingo yanayotokana na mkazo wa misuli au kwa sababu ya mkao mbaya, huwa yanaanza kupungua ndani ya siku 2-3 kwa kufanya mambo yafuatayo
- Endelea na shughuli zako kama kawaida kadri maumivu yanavyokuruhusu. Kama maumivu ni makali sana, unaweza kuhitaji kupumzisha shingo kwa angalau siku 1 au 2
- Unaweza kutengeneza ‘’collar’’ ambayo itasaidia kutegemeza shingo. Kutengeneza ‘’collar’’, kunja taulo vizuri, izungushe shingoni na kisha ifunge kwa kamba ili isifunguke. Tumia ‘’collar’’ kwa muda mfupi tu na usiivae wakati wa usiku ukiwa umelala
- Anza kufanya mazoezi ya shingo unapoona maumivu yamepungua, na unaweza kufuata hatua zifuatazo kupunguza mkazo wa shingo
- Simama wima au kaa kwenye kona ya kiti huku ukiangalia mbele. Egemeza kichwa kuelekea kwenye bega huku bega likiwa chini.
- Kiache kichwa hapo kwa sekunde kadhaa kisha nyanyua kichwa chako. Rudia hivi kwa upande mwingine
- Rudia zoezi hilo mara 5 kwa kila upande mara 3 kwa siku. Fanya mazoezi mpaka utakapojisikia vibaya, ila usiendelee na mazoezi kama unahisi maumivu
- Kadri unavyoweza, endelea kuongeza uwezo wa shingo kujikunja taratibu. ACHA MARA MOJA kama unaona maumivu yanaongezeka au yanaanza kusambaa kuelekea kwenye mkono wako.
- Tumia dawa za kupunguza maumivu. Madawa ya kupunguza maumivu yatasaidia kukupunguzia karaha inayosababisha na maumivu ya shingo. Tumia ‘’Acetaminophen’’ au ‘’Ibuprofen’’.
- Ili kupunguza mkazo wa shingo unaweza kuoga / kusimama chini ya bomba la kuogea lenye maji ya moto au ukachukua chupa iliyowekewa maji ya moto, ukaifunika na kitambaa kisha ukaiweka shingoni au ukailalia kama mto kwa dakika 15 kila baada ya masaa machache
- Tumia mto unapokuwa umelala
Mwone daktari kama
Ni vizuri kuomba ushauri wa daktari
- Kama kukaza au maumivu ya shingo yanaendelea kuwa mabaya zaidi
- Kama tatizo halijaanza kupungua baada ya siku 2
Leave feedback about this