Maelezo ya jumla
Kukaza kwa misuli ya miguu ”leg cramp” kunasababisha maumivu kwenye misuli ya mguu au ndama ya mguu. Misuli inakaza na kukakamaa, na inauma ukijaribu kujongea. Maumivu huwa yanadumu kwa dakika kadhaa tu. Misuli inaweza kukaza ukiwa unaamka asubuhi au baada ya kukaa au kulala vibaya. Msuli unapobana ukiwa unafanya kazi nzito au mazoezi, huwa ni kwa sababu umeitumia misuli sana kuliko ilivyozoea, joto kali, upungufu wa maji mwilini au upotevu mkubwa wa chumvi au madini mengine kutoka mwilini. Watu wanaoogelea wanaweza kubanwa misuli kama maji ni ya baridi sana au kama wamechoka.
Kukaza kwa misuli ya miguu-mwone daktari kama
Ni vizuri kutafuta usaidizi wa kitabibu haraka kama una tatizo la kukaza kwa misuli ya miguu na:
- Unaendelea kupata maumivu muda wote kwenye ndama ya mguu au mguu kwa ujumla
- Mguu ni wa moto, mwekundu au umevimba; ukibadilika rangi na kuwa wa bluu au mweupe au kama unahisi umekuwa wa baridi sana
Unachoweza kufanya wewe mwenyewe
Japo kukaza kwa msuli ya miguu huwa kunaisha kwenyewe, ukifanya mambo yafuatayo yatasaidia kupunguza karaha
- Msuli ukibana wakati wa mazoezi, ACHA. Kanda ‘’massage’’ taratibu msuli uliokaza. Kama msuli wa ndama ya mguu ndio uliokaza, unyooshe. Shika vidole vya mguu na uvivute kuelekea uelekeo wa goti ukiruhusu kifundo cha mguu kujikunja. Shikilia vidole vya mguu mpaka mkazo utakapoisha AU unaweza kutumia kitambaa kuvuta vidole kama ilivyo oneshwa hapa chini.
- Kama kukaza kwa misuli ya miguu kukitokea ukiwa kitandani, shuka usimame kisha utikise mguu wako au tembea tembea. Kama ukiona mkazo unaendelea jaribu kujinyoosha kama tulivyoelezana hapo juu
- Jaribu joto, hasa kama kukaza kwa misuli kumesababishwa na kuogelea kwenye maji ya baridi. Oga maji ya moto, kisha jifunge taulo lenye joto kuzunguka eneo lenye mkazo wa misuli. Vaa nguo au ufunike mguu kwa kutumia blanketi.
- Lakini kwa mkazo wa misuli uliosababishwa na kuitumikisha misuli kuliko ilivyo kawaida, jaribu kuweka barafu kuzunguka sehemu inayouma. Ponda barafu iliyo kwenye kifuko, ifunge kwa kitambaa chepesi kisha iweke kwenye mguu kwa angalau dakika 10.
Kuzuia kukaza kwa misuli ya miguu
Fanya zoezi la kunyoosha misuli ya ndama ya mguu. Jaribu zoezi hili ili kuondoa mkazo mguuni au lifanye kila siku ili kuzuia misuli kukaza siku nyingine. Lifanye kabla na baada ya kutumia misuli ya miguu kwa muda mrefu na kabla ya kwenda kulala kama una hatari ya misuli kukaza ukiwa umelala.
- Simama umbali sawa na mikono yako ikiwa imekujuliwa, mguu mmoja ukiwa mbele ya mwingine na mikono yako ikiwa imeshika ukuta usawa wa mabega yako.
- Hakikisha miguu yako imekaa ‘’flat’’ kwenye ardhi, egemea kwenda mbele, kunja goti la mguu wa mbele na sukuma kisigino cha mguu wa nyuma kwenda chini ardhini. Utahisi misuli ya ndama ya mguu ilijinyoosha. Rudia zoezi hili kwenye mguu mwingine.
Mwone daktari kama
Panga kumwona daktari
- Kama kukaza kwa misuli ya mguu hakuishi/hakuondoki au kama mkazo unakuwa mkali zaidi au unatokea mara kwa mara
Leave feedback about this