KUKOROTA

KUKOROTA

 • February 19, 2021
 • 0 Likes
 • 50 Views
 • 0 Comments

Maelezo ya jumla

Kukorota ni sauti kama mluzi inayotokea mtu anapokuwa anapumua kutoa hewa nje. Kifua kinaweza kuwa kimebana na unaweza kupata shida kupumua. Sababu kubwa ya kukorota ni pumu; tukio la pumu mara nyingi husababishwa na mzio unaosababishwa na kuvuta hewa yenye kizio kama vile vumbi, au kwa sababu ya msongo, hewa ya baridi au mazoezi. Sababu nyingine za kukorota ni pamoja na maambukizi ya kifua; moshi wa tumbaku; tukio kali linalosababishwa na mzio ‘’allergic reaction’ au matatizo ya moyo au mapafu.

Mwone daktari kama

Tafuta usaidizi wa kitabibu haraka sana kama:

 • Umeanza kukorota ghafla au midomo imeanza kubadilika rangi na kuwa ya bluu
 • Unajihisi uoga au wasiwasi mwingi kwa sababu ya kupata shida kupumua

Panga kumwona daktari kama

 • Ni vizuri kupanga kumwona daktari haraka kama una korota. Angalia kama unatumia madawa yanayoweza kusababisha kukorota, kama vile madawa ya kupunguza maumivu au madawa ya kudhibiti shinikizo la damu.

Unachoweza kufanya wewe mwenyewe

Ukifanya mambo yafuatayo yatasaidia kupunguza kukorota au kupunguza uwezekano wa kupata tukio la kubanwa na pumu au sababu nyingine, na kutegemeza matibabu yaliyotolewa na daktari

 • Kama unapatwa na tukio la kubanwa na pumu kuwa mtulivu, jitahidi kuwa mtulivu na vuta pumzi taratibu. Kaa katika mkao mzuri: unaweza kujisikia vizuri zaidi ukiegemea mbele na kuweka mikono yako juu ya meza au kwenye mikono ya kiti
 • Kama unatumia dawa ya pumu ya kuvuta ndani ‘’asthma inhaler’’, hakikisha unakuwa nayo wakati wote na uitumie kama ulivyoelekezwa na daktari. Unaweza kutunza au kuwa na ‘’inhaler’’ nyingine za ziada nyumbani, shuleni au kazini.
 • Kama msongo unasababisha kukorota kuongezeka, jaribu mazoezi ya kupumua ‘’deep breathing exercise’’ na mbinu za kulegeza misuli ‘’muscle relaxation technique’’ ili kudhibiti msongo. Unaweza pia kutumia mbinu hizi kukutuliza ‘’calm down’’ wakati wa tukio la pumu. BONYEZA HAPA KUJIFUNZA MBINU HIZI
 • Mazoezi ya mara kwa mara kama vile kutembea na kuogelea, kunaweza kupunguza dalili na kukuacha ukiwa na afya bora zaidi. Punguza mazoezi kama yanasababisha shida kuwa kubwa zaidi
 • Usikae kwenye eneo lenye hewa ya baridi, kama unataka kutoka nje kwenye baridi, jifunike usoni kwa kitaambaa ‘’scarf’’ ili kuipa joto hewa kabla ya kuivuta. Kama hewa imechafuliwa na vumbi, kaa ndani na funga madirisha.
 • Epuka kukaa eneo lenye moshi au mazingira yenye uchafuzi mkubwa wa hewa na yenye kizio kinachoweza kusababisha ukapata tukio la pumu. Kama unavuta sigara, ACHA.

Kuzuia

Watu wengi wenye pumu wana mzio na vumbi. Vitu vingine vinavyoweza kusababisha tukio la pumu ni kuvu ‘’mold’’, nywele na manyoya ya wanyama wa kufugwa, na kemikali za kusafisha nyumba. Fanya mambo yafuatayo kupunguza vitu vinavyoweza kuchochea kutokea kwa tukio la pumu

 • Safisha mazingira ya nyumba kwa kutumia kitambaa kilicholowanishwa ili kuondoa vumbi na punguza vitu usivyovihitaji ndani ya chumba. Usiwe na vidude vingi vya kuchezea kwa mtoto mwenye pumu. Kila baada ya wiki 2, viweke kwenye mfuko na viweke kwenye friji kwa masaa 6, au vioshe kwa maji ya moto.
 • Tumia mito ya kulalia ambayo imetengenezwa na vitambaa vilivyotengenezwa viwandani ‘’synthetic’’ badala ya kutumia za manyoya ya wanyama au pamba, zinakusanya uchafu na vumbi kwa urahisi.
 • Nunua shuka la kufunika godoro lote ‘’mattress cover’’ sio sehemu ya kichwa tu, na fua matandiko kila wiki kwenye maji ya moto angalau 600C. Safisha mapazia mara kwa mara.
 • Kama unatumia ‘’carpet’’ badilisha uweke vigae au sakafu pekee, mazuria yanatunza vumbi na kuruhusu kuvu ‘’mold’’ kukua kwa urahisi
 • Ukitaka kusafisha nyumba, vaa barakoa ‘’mask’’ inayofaa kuzuia vumbi. Kama ikiwezekana mwambie mtu mwingine akusaidie kufagia nyumba ili kuepuka vumbi
 • Hakikisha nyumba ina madirisha makubwa yanayoingiza hewa ya kutosha. Funga milango ya bafu na jikoni ili kuzuia unyevunyevu kusambaa ndani ya nyumba. Kama kuna kuvu wameanza kuota kwenye sakafu, mapazia au kwenye madirisha ya bafuni, tumia kemikali kuwaondoa ‘’bleach solution’’. Epuka kutumia kemikali kali na zenye harufu kali kusafisha nyumba.
 • Kama una mzio na nywele au manyoya ya mnyama fulani, mwondoe ndani ya nyumba, ikiwezekana asiwepo kabisa nyumbani kwako. Kama haiwezekani kumwondoa kabisa, hakikisha haingii kabisa kwenye chumba cha kulala na hakai maeneo unayokaa kwa kadri unavyoweza. Mtunze na kumsafisha vyema mnyama wa kufugwa mara kwa mara.

Mwone daktari kama

Ni vizuri kupanga kumwona daktari kama

 • Unashindwa kudhibiti dalili nyingine za pumu au kukorota hata baada ya kujaribu njia hizo hapo juu

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/003070.htm

 • Share:

Leave Your Comment