Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko
Maelezo ya jumla
Kumtelekeza mtoto (child neglect) ni aina ya unyanyasaji wa mtoto unaotokea mtu anapoamua kwa makusudi kutokumpatia mtoto chakula, maji, malazi, nguo, matibabu, au mahitaji mengine.
Kumtekekeza mtoto ni nini?
Kutojali au kumtelekeza mtoto kuna sura mbalimbali Â
- Mtoto akiruhusiwa kushuhudia mambo ya ukatili, vita au unyanyaswaji wa mzazi, ndugu au mtu mwingine
- Kumpuuza, kumtukana, au kumtishia mtoto kuwa utampiga au kumuumiza
- Kutokumpatia mtoto mazingira mazuri na salama ya kuishi, mtoto huishi kwa wasiwasi
- Kuonesha kutojali na kupuuza ustawi wa mtoto
Ni zipi dalili za mtoto aliyetelekezwa?
Dalili za kisaikolojia kwa watoto zinazosababishwa na kutelekezwa ni:
- Mtoto anapata matatizo/ugumu kujifunza akiwa shuleni
- Mtoto hali chakula vizuri, hii husababisha kupungua uzito au kushindwa kuongezeka uzito
- Matatizo ya kihisia, mtoto hujihisi kuwa hana thamani, hunyong’onyea, na huwa na wasiwasi mwingi
- Mtoto huanza tabia ya uasi na kutosikia la mtu
- Matatizo ya usingizi, mtoto halali
- Malalamiko yasiyo ya wazi ya mara kwa mara
Sababu za kumtelekeza mtoto?
Kiwango cha watoto wanaotelekezwa kimwili na kihisia ni ngumu kufafanua.
Watoto waliotelekezwa na kudhulumiwa haki yao ya utoto, huwa katika hatari kubwa ya kuwa wanyanyasaji wanapokua watu wazima.
Mambo yanayoongeza hatari ya kumtelekeza mtoto
Mambo yanayoongeza hatari ya mtoto kutelekezwa ni pamoja na:
- Magonjwa ya akili
- Umaskini
- Msongo katika familia
- Matumizi ya madawa ya kulevya-wazazi au walezi
Wakati gani utafute matibabu ya haraka?
- Mpeleke mtoto kwa mtoa huduma ya afya kama mtoto ana:
- Ana mabadiliko kwenye mwili yasiyoelezeka, yanayotia mashaka na yasiyo na sababu inayokubalika, kama majeraha , kupungua uzito, au uchovu uliopitiliza
- Mabadiliko makubwa ya tabia yasiyoelezeka
- Kama ukihisi mtoto ananyanyaswa au ametelekezwa , ni wajibu wa kila mwana jamii kuitarifu mamlaka.
Utambuzi
Mtaalamu wa afya ya akili anapaswa kuwachunguza kwa kina watoto wote wanaodhaniwa kudhulumiwa kihisia. Watoto waliotelekezwa na kudhulumiwa kisaikolojia wanapaswa kuchunguzwa kama wamepitia au kukutana na aina nyingine za unyanyasaji.
Uchaguzi wa matibabu
- Kama unafikiri mtoto yuko katika hatari ya kunyanyaswa au kutelekezwa, unapaswa kutoa taarifa polisi.
- Kama unahisi mtoto anadhulumiwa, ripoti mara moja.
- Sheria inawataka wafanyakazi wa huduma ya afya, wafanyakazi wa shule, na wataalamu wengine wanaohudumia watoto kutoa ripoti kama mtoto ananyanyaswa.
- Matibabu ya mtoto aliyetelekezwa hujumuisha tiba ya afya ya akili na lishe bora
- Inaweza kulazimu kumwondoa mtoto nyumbani kwao ili kuzuia unyanyasaji zaidi.
- Matibabu kwa wanyanyasaji yanaweza kuhusisha matibabu ya ugonjwa wa akili, pombe, au matumizi mabaya ya dawa za kulevya.
Nini cha kutarajia baada ya kumtelekeza mtoto?
- Baada ya matibabu, watoto wengi na wazazi wanaweza kuunganishwa tena baadae.
- Matokeo ya muda mrefu yanategemea:
-
- Ni kwa kiasi gani mtoto alinyanyaswa
- Ni kwa muda gani mtoto alinyanyaswa
- Mafanikio ya tiba
Matatizo yanayoweza kutokea baada ya kumtelekeza mtoto
- Kama ilivyo kwa aina zote za unyanyasaji, majeraha yanaweza kusababisha kifo.
- Matatizo mengine ya muda mrefu ni pamoja na:
-
- Kuwa mnyanyasaji atakapoku mtu mzima
- Sonona
- Kukosa kujiamini
- Tabia ya uasi
Kuzuia
- Programu za kijamii, kama vile ziara za wauguzi na wafanyakazi wa ustawi wa jamii majumbani ,zinaweza kushinikiza familia kubadili tabia au kuzuia unyanyasaji katika familia za hatari.
- Programu za shule, ili kuboresha ulezi, mawasiliano, na kujitegemea, hii inaweza kusaidia kuzuia unyanyasaji baadae na inaweza kusaidia kuwatambua watoto walionyanyaswa.
- Madarasa ya kufundisha namna njema ya ulezi wa watoto. Wanandoa wapya wanapaswa kuhimizwa kujifunza katika madarasa haya kabla ya kuwa na mtoto.
Leave feedback about this