Magonjwa ya ndani ya mwili

KUMWAMBIA MWENZI KUWA UNA MAGONJWA YA NGONO

magonjwa ya ngono

Maelezo ya jumla

Kuna unyanyapaa mkubwa sana na habari nyingi sana za kupotosha kuhusu magonjwa ya ngono. Kwa sababu hii inaweza kuwa ngumu sana kuyaongelea. Lakini sote tunajuan ni muhimu sana kuyaongelea ili kuyadhibiti. Magonjwa ya ngono yanawapata watu wengi, hasa vijana wanaobalehe. Kwa hiyo, unaweza kulikwepa swala hili la kuyaongelea, lakini siku moja utapaswa kufanya hivyo.
Kama umekuwa ukisita kuhusu swala hili, USIOGOPE hauko peke yako. Hatujawahi kufundishwa jinsi ya kuyaongelea magonjwa ya ngono, Lakini pia tunajua kuwa ni muhimu kuvunja ukimya uliopo. Kuondoa aibu iliyopo na kuukabili unyanyapaa, hii ni kwa sababu bila kufanya hivyo hatutoweza kupunguza maambukizi ya magonjwa ya ngono.

Ukiwa na magonjwa ya ngono fuata hatua zifuatazo;magonjwa ya ngono

  • Nenda kapime, unaweza kuwa na ugonjwa wa ngono na usijue, magonjwa mengi ya ngono hayana dalili za bayana na watu wengi huwaambukiza wengine bila kujua. Na kama umegundulika kuwa una maambukizi unaweza kufanya hili la pili.
  • Epuka dhana potofu, usiamini sana mambo unayoyasikia kuhusu magonjwa ya ngono, fanya utafiti ili uwe na uhakika kuhusu dalili, tiba na jinsi ya kumkinga mwenzi wako. Unaweza kujifunza hili hapa (Magonjwa ya ngono). Kupata taarifa sahihi ni muhimu sana
  • Amua namna ya kuwasiliana na mwenzi wako, Kama utaamua kukutana nae na kuongea nae uso kwa uso, chagua mahala unapohisi ni salama na comfortable kwa majadiliano. Kama ikiwezekana iwe karibu na mlango ili iwe rahisi kuondoka kama mwenzi wako atakasirika au kukuudhi baada ya kumwambia. Kama ukiona ni ngumu kukutana nae, unaweza kuandika ujumbe wa simu, barua pepe au hata kufanya video chat. Cha msingi ni kuchagua njia sahihi kulingana na mahusiano mliyonayo na mnapendelea njia gani.
  • Kufungua mjadala, Kufungua mjadala ndio swala gumum zaidi, Unaweza kuanza kwa kumwambia jinsi unavyomthamini na ungeweza kufanya kila kitu ili kumlinda na kisha kumwambia kuwa una ugonjwa wa ngono.  Unaweza kuanza kwa kumuuliza kama ameshawawi kuwa na ugonjwa wa ngono na kisha ukaendelea au unaweza kumwambia moja kwa moja kuwa una ugonjwa wa ngono na kisha mpe nafasi akuulize maswali. Ni kawaida kuhisi aibu, lakini baada ya kufunguka utajihisi vyema na mwenzio labda atakushukuru na kukuamini zaidi.
  • Dhibiti matarajio yako, Baada ya kumwambia mwenzi wako anaweza kukushukuru na kukutia moyo, na kukwambia kuwa bado anakupenda na kukusifu kwa kufunguka, lakini si mara zote mapokeo yatakuwa hivi. Kuna uwezekano kuwa hatokuelewa kabisaaa, anaweza asiamini (Hakuna haiwezi kuwa kweli) au anaweza kuogopa sana (tutafanya nini sisi, tumekwisha), Wakati mwingine anaweza kukuhukumu na kukutukana (ulilala na nani wewe Mal*ya? Na vitu kama hivyo) au anaweza kukukataa kabisa (sitaki kuwa na wewe tena).
    Ukipata mrejesho wa aina hii, unaweza kujisikia vibaya sana. Unaweza kujaribu kujieleza au unaweza kuamua kunyamaza, ukaondoka na kisha kumtafuta baadae uongee nae tena. Kama haukufurahishwa na mrejesho ulioupata kutoka kwake na hautaki kuonana nae. tena, sio mbaya ni uamuzi wako
  • Jipongeze, umeweza, sio kila mtu anaweza kufanya ulilofanya, jipongeze kwa kupiga hatua hii kubwa.

Ukiwa na magonjwa ya ngono kumbuka;

Kumbuka kuwa watu wengi wana magonjwa ya ngono na hawajui, kwa hiyo ni vizuri kujua na ni muhimu kumwambia mwenzi wako ili nae apime na kupata matibabu.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/sexuallytransmitteddiseases.html

Leave feedback about this

  • Quality
  • Price
  • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X